Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,273
Choo ni sehemu ya muhimu sana, iwe nyumbani, hotelini, ofisini, sokoni, safarini, nk. Utunzaji wa choo unahusisha usafi wake. Ukitaka kufahamu ustaarabu wa jamii angalia mpango lip wa vyoo na usafi wake.
Hata uishi kwenye nyumba yenye thamani ya mabilioni, kama choo chako ni kichafu wanaokuzunguka hawataona thamani ya nyumba watashusha thamani ya ustaarabu wako.
Wastaarabu wakijenga majengo yanayohudumia jamii, wanahakikisha kuna timu kamili ya usafi wa vyoo. Hata iwe kwa kulipia lakini mtu yeyote atakae taka huduma hii inapatikana kikamilifu ikiwa na nyenzo zote za huduma iwe maji au karatasi maalum. Pia maji na sabuni ya kunawia mikono baada ya kumaliza matumizi ya choo.