Chonde Chonde wafuatao ni Finland, Norway na Sweden

Ni aibu sana nchi tulizokuwa nazo sawa kiuchumi kusaidia nchi kubwa kama Tanzania eti vi nchi kama mkoa ndo vinasaidia Tanzania sasa UHURU ulikuwa na maana gani.

Wenzetu walishatoka kwenye kuwaza basic needs.
Haiti ilipata uhuru zaidi ya miaka 200 sasa lakini kwa sababu ya uongozi mbovu... Same to Tanzania. Miaka 60 hakuna la maana linalioendea zaidi ya ule wimbo wetu maarufu wa amani Utafikiri ni sisi tu Afrika nzima wenye amani.
 
Kama unayosema wewe ni ya kweli basi sababu za kujitoa kwao zilikuwa za uongo na kama sababu walizosema ni za kweli basi wewe hukuchimba vya kutosha kuhusu hili sakata.
 
Taa ya tahadhari umekwisha washwa na Denmark kwa kuondoka nchini. Huu ni uamuzi mgumu sana kwa nchi ambayo imetufadhili tangu uhuru. Miradi mingi sana imejengwa kwa ufadhili wa Denmark. Kumbukeni walivyoisaidia nchi hii katika elimu ikiwa ni pamoja na elimu ya watu wazima, ujenzi wa shule na vyuo, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa fani mbalimbali. Pia angalia sekta ya kilimo, maji, utawala bora, ujenzi wa barabara vijijini, budget support nk.

Tanzania kama nchi tutaathirika sana na uamuzi huu. Kuna kila sababu serikali ikajiangalia upya wapi imejikwaa. Haiwezekani kila siku tunawatukana, tunawakemea kwa mambo yetu ya hovyo na kuwaita mabeberu wakaendelea kutuvumilia.

Tukumbuke Denmark haipo peke yake katika kutoa misaada hapa nchini. Pia nchi zote za Nordic zinashirikiana na kuratibu kwa pamoja misaada yote inayoletwa nchini. Nchi hizo ni Norway, Sweden na Finland. Nchi hizi zilifika hata hatua ya kuigawana nchi hii ili kuleta uwiano wa maendeleo kama ifuatavyo; Norway - Rukwa ikiwemo Katavi na Kigoma; Denmark - Mbeya, Iringa na Ruvuma; Finland- Lindi na Mtwara; Sweden- Morogoro na baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Maeneo ambayo tunatakiwa kufanya mabadiliko ni pamoja na demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu. Tusijipe moyo kuwa tumeendelea na kwamba hatuhitaji misaada yao, hilo ni kosa la jinai! Tupunguze kijimwambafai na kutoa maneno ya matusi na kejeli. Wafadhili wetu wana moyo wa nyama wanaumizwa pia!
Hawapendi kukaa nchi zenye magaidi. Norway hawana ubalozi Somalia. Baada ya kugundua Hamza ni mwanaccm tena mlezi wa chama uvccm wamefungasha vilago.
 
Hawapendi kukaa nchi zenye magaidi. Norway hawana ubalozi Somalia. Baada ya kugundua Hamza ni mwanaccm tena mlezi wa chama uvccm wamefungasha vilago.
CCM wanapaswa kijitathmini kama wanatosha kuendana na jumuiya ya kimataifa! Haiwezekani wawakilishi wa nchi rafiki wakae kwa jirani!
 
Dernmark, wamegundua Magufuli alikuwa kichwa ila sasa hivi hamna kitu wameamua kusepa zao.
Wajirekebishe hawa wa safari za angani kila siku kama sivyo tuendelee kula hasara.
 
Si mlikuwa mnamsakama na kumpa majina mabaya JPM, kisha baada ya kuondoka mkaanza kufanya tafirija?

Kuna GIZA na UTELEZI usiomithirika utajidhihirisha siku sio nyingi ndipo mtafahamu ukweli na kutafuta namna ya kuomba msamaha kwa kusingizia wengine wenye wenye nia njema kwa nchi.
Magufuli hafai...tena angekuwepo huyo mpaka leo Denmark wangeshafunga ubalozi wao tangu wiki iliyopita.
 
Maovu mengi yaliyofanywa na utawala wa marehemu Magufuli, matokeo yake yataanza kuonekana wakati wa awamu ya 6.

Samia alichoharibu ni kuwa popo, si mnyama si ndege, si moto si baridi. Mara anasema anataka kusimamia haki, mara yeye na Magufuli ni sawa, mara anafuta kesi za kubambikia watu, mara anawabambikia watu. Kuwa na ushirikiano na mtu kama huyo ni kupoteza muda.

Wenye akili wanataka mtu aliyenyoka kifikra, kauli na kimatendo, siyo mbabaishaji. Marehemu, Dunia nzima ilikuwa inamjua ni dikteta, lakini huyu haeleweki.
Hata wewe ni dikteta katika maisha yako binafsi, familia na jamii inayokuzunguka vinginevyo usingeonesha chuki dhidi ya JPM mwenye msimamo usioyumbishwa na yeyote/chochote na anlikuwa tayari kwa athari zozote ziwe chanya au hasi.

Demokrasia ni uchochoro wa uhalifu
 
Taa ya tahadhari umekwisha washwa na Denmark kwa kuondoka nchini. Huu ni uamuzi mgumu sana kwa nchi ambayo imetufadhili tangu uhuru. Miradi mingi sana imejengwa kwa ufadhili wa Denmark. Kumbukeni walivyoisaidia nchi hii katika elimu ikiwa ni pamoja na elimu ya watu wazima, ujenzi wa shule na vyuo, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa fani mbalimbali. Pia angalia sekta ya kilimo, maji, utawala bora, ujenzi wa barabara vijijini, budget support nk.

Tanzania kama nchi tutaathirika sana na uamuzi huu. Kuna kila sababu serikali ikajiangalia upya wapi imejikwaa. Haiwezekani kila siku tunawatukana, tunawakemea kwa mambo yetu ya hovyo na kuwaita mabeberu wakaendelea kutuvumilia.

Tukumbuke Denmark haipo peke yake katika kutoa misaada hapa nchini. Pia nchi zote za Nordic zinashirikiana na kuratibu kwa pamoja misaada yote inayoletwa nchini. Nchi hizo ni Norway, Sweden na Finland. Nchi hizi zilifika hata hatua ya kuigawana nchi hii ili kuleta uwiano wa maendeleo kama ifuatavyo; Norway - Rukwa ikiwemo Katavi na Kigoma; Denmark - Mbeya, Iringa na Ruvuma; Finland- Lindi na Mtwara; Sweden- Morogoro na baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Maeneo ambayo tunatakiwa kufanya mabadiliko ni pamoja na demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu. Tusijipe moyo kuwa tumeendelea na kwamba hatuhitaji misaada yao, hilo ni kosa la jinai! Tupunguze kijimwambafai na kutoa maneno ya matusi na kejeli. Wafadhili wetu wana moyo wa nyama wanaumizwa pia!
Hizi Nchi za Scandinavian huwa always zinaenda pamoja. Na mara nyingi Denmark ndio wanakuwaga wa kwanza ku test the Water. Kwa vile amekwisha tangaza, basi hawa wengine watafuata tu.

Kikubwa kama Nchi, hatujielewi tunataka nini na tunaenda wapi....Mikataba na misaada mingi inapokelewa toka kwa Nchi zenye uwalakini Mkubwa....Sasa hawa wameshaona mbali na hawataka ugomvi na Mtu.

Tusubiri, kuna makaburi ya Watu yatakuja vukuliwa na Vizazi vijazwa na mifupa yao kucharazwa viboko....
 
Ni jambo la kusikitisha serikali kuchukulia hili jambo poa?
 
Serikali futeni kesi zote zenye mlengo wa kisiasa hasa ya Mbowe na Sabaya

1. Msilazimishe watu kuchanja chanjo ya UVIKO-19 kwa vitisho
2. Mwendesha mashitaka futa mashitaka dhidi ya Mbowe na Sabaya ili kuiponya nchi na BALAA linalokuja
3. Utawala uliopo usidhalilishe viongozi walio chini yao kwa kufungulia mashitaka ya visasi na chuki
4. Askari polisi waache dhuluma, kusingizia kesi na kufanya visasi dhidi ya wananchi wanaotoa siri ya udhaifu wao
5. Wanasiasa wasameheane hadharani kwa kushirikisha wananchi kisha wajenge nchi kwa pamoja
6. Viongozi mliopo madarakani acheni kudhalilisha viongozi wa nchi waliotangulia mtaharibikiwa vibaya sana
7. Mamlaka ya nchi iache kuingilia viongozi wa kidini na kiroho, maombi ya WIKI moja yaridhiwe na nchi kwa pamoja
8. Tanzania iko kwenye hatari ya kuvamiwa kwa sasa, wananchi, jeshi la ulinzi, uongozi wa nchi na viongozi wa dini/kiroho unganeni haraka muachane na ubishi wa mabavu ya mamlaka
9. Jeshi la polisi lindeni raia na mali zao
10. Tekelezeni miradi yote ambayo wanasiasa mliahidi kwenye uchaguzi mkichepusha kuna somo lipo mezani kuifundisha Tanzania
11. Vyama vya siasa muwasamehe CCM kwa yote mnaodhani waliwakwaza; ninyi CCM mjishushe muache kiburi mtasambaratika ijapokuwa hilo huwa hamuliamini lakini litatokea hakika
12. Mamlaka ya nchi acheni kuwabebesha mzigo wa kodi wananchi wa chini hii laana itaangusha utawala wenu
13. Tamkeni hadharani kama makao makuu ya nchi yamehamishwa kutoka Dodoma kurudi Dar Es Salaam ili wananchi waelewe na kuridhia au la tofauti na hapo kuna mvutano utaleta athari kwa uchumi. usalama na jamii itaparaganyika
14. Viongozi mlioko madarakani na wanasiasa ama wa chama tawala au upinzani jiepusheni kumtupia lawama hayati JPM kwa lolote lile ili mpendwe haitatokea, na amani itarejea mkiwa na moyo wa kusamehe na kuanza upya kila mmoja akimheshimu mwingine
15. Safari za nje ya zisizo na tija zisitishwe na viongozi watatue kero za wananchi wa chini hapo mtapata kibali bila hivyo utawala unaonekana kutoendela kusisima
16. Aina ya utatuzi wa kero za muungano unaoendelea usitishwe na wananchi washirikishwe watawashauri vizuri tu kwa manufaa ya pande mbili maana kuna fukuto miongoni mwenu....................kwa maana inaonekana minong'ono ya kutotendewa haki kila upande inafukuta kila upande ukilaumu upande mwingine, Kumbukeni Tanzania imejengwa kwa tofali za chuma kichafu na udongo wa mboji kwa hiyo mtikisiko pasipokuwa na mahusiano mazuri, kuaminiana, kusaidiana, kujengana na kuheshimiana kutaipasua vipande (Zanzibar vipande sita Pemba viwili, Unguja vinne) Tanzania bara (vipande saba Kasikazini, Kasikazini Magharibi, Pwani, Nyanda za juu kusini, Kusini, Kati na Magharibi)

*Watumishi wa Mungu, Wananchi wa chini, Vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa waandamizi wa nchi WAHESHIMIWA, WASAIDIWE, nao waondoe KIBURI giza linaweza kupungua
Mengine nakubaliana nawe, si yote!
 
Back
Top Bottom