Chonde Chonde wafuatao ni Finland, Norway na Sweden

Taa ya tahadhari umekwisha washwa na Denmark kwa kuondoka nchini. Huu ni uamuzi mgumu sana kwa nchi ambayo imetufadhili tangu uhuru. Miradi mingi sana imejengwa kwa ufadhili wa Denmark. Kumbukeni walivyoisaidia nchi hii katika elimu ikiwa ni pamoja na elimu ya watu wazima, ujenzi wa shule na vyuo, kutoa mafunzo kwa wataalamu wa fani mbalimbali. Pia angalia sekta ya kilimo, maji, utawala bora, ujenzi wa barabara vijijini, budget support nk.

Tanzania kama nchi tutaathirika sana na uamuzi huu. Kuna kila sababu serikali ikajiangalia upya wapi imejikwaa. Haiwezekani kila siku tunawatukana, tunawakemea kwa mambo yetu ya hovyo na kuwaita mabeberu wakaendelea kutuvumilia.

Tukumbuke Denmark haipo peke yake katika kutoa misaada hapa nchini. Pia nchi zote za Nordic zinashirikiana na kuratibu kwa pamoja misaada yote inayoletwa nchini. Nchi hizo ni Norway, Sweden na Finland. Nchi hizi zilifika hata hatua ya kuigawana nchi hii ili kuleta uwiano wa maendeleo kama ifuatavyo; Norway - Rukwa ikiwemo Katavi na Kigoma; Denmark - Mbeya, Iringa na Ruvuma; Finland- Lindi na Mtwara; Sweden- Morogoro na baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Maeneo ambayo tunatakiwa kufanya mabadiliko ni pamoja na demokrasia, utawala wa sheria na haki za binadamu. Tusijipe moyo kuwa tumeendelea na kwamba hatuhitaji misaada yao, hilo ni kosa la jinai! Tupunguze kijimwambafai na kutoa maneno ya matusi na kejeli. Wafadhili wetu wana moyo wa nyama wanaumizwa pia!
Wakilegezewa mimacho kidogo wataahirisha maamuzi! IGP endelea kukandamiza demokrasia mama atawalainisha kwa mimacho mlegezo!!!
 
Tutawamiss
DANIDA, FINIDA na NORAD. Misaada Yao inaonekana.
 
Back
Top Bottom