voda ni majambazi siku hizi wanakataa hatari.sasa ni mpango wa kuhama
Lakini ni nani anayewapa kichwa hawa Vodacom hadi kuthubutu kutufanyia uhalifu mkubwa namna hii bila hata ya kuonyeshewa kidole? Ni wapi wanapata jeuri ya kuwanyanyasa na kuwaibia wananchi ki hivyo? Ukitafakari kwa makini utagundua udhaifu wetu ndiyo unaosababisha tuwe watumwa katika nchi yetu wenyewe.
Unatarajia nini katika kampuni ambayo viongozi waandamizi tena wenye maamuzi ndiyo wenye hisa?
Ni lazima watanzania tuelewe sasa kwamba mchawi wa ustawi wetu yumo miongoni mwetu na ni mwenzetu. Inasikitisha lakini ndiyo ukweli wenyewe!
Iko wapi ile tume ya maadili na kazi zake ni zipi kama si kuwadhibiti viongozi manyang'au waliosheheni serikalini wengi wzo wakiwa pia viongozi wa CCM?
La kushangaza zaidi ni kuwepo kwa Tume ya mawasiliano ambayo kwangu mimi ni walewale; jora moja, mashono tu tofauti!
Binafsi nimewaacha kabisa wezi hao walioikamata sehemu nyeti serikali hii na kufanya lolote bila ya kuguswa! Niliamua kuachana nao baada ya kukatwa fedha kabla sijaongea kila nilipoongeza salio na nilipowapigia sikupata ufafanuzi wa kuniridhisha. Unaweka 5,000/= asubuhi unakuta salio la 500/=! Mara ya mwisho niliamua kukata shauri na kuhama kabisa baada ya kununua muda wa maongezi kwa ajili ya kununua unlimited bundle ya internet kwa wiki, nilinunua 12,500/= ambapo nilipokea msg ya kuthibitisha manunuzi hayo, nikacheki salio ni kweli wamekata. Lakini kila nilipojiunganiliambiwa sina salio la kutosha; ndipo nilipozinduka kucheki salio ambalo lilisomeka Tsh. 1,800/= kila nilipopiga namba 100 nilizunguushwa na kuelekezwa kwenye namba wanayochaji 100 kila unapozungumza nao, huko nako unakatwa hela kisha unaambiwa wahudumu 'wako bize' piga baadae ukicheki salio linazidi kwishana usipokuwa makini utakatwa fedha karibu nusu yaile unayoifuatilia!
Jamani, tuungane sasa tuseme mwisho wa wizi huu wa hawa washirika wa kina Lowasa, RA, na vibaka wengine ndani ya magwanda ya kijani na njano.