*JOHN MZEE WA KULENGA*
*Sehemu ya 06*
John aliendelea kuwa mzee wa totozi, mara kwa mara kila wikiendi ilikuwa ni lazima kutoka na kwenda sehemu mbalimbali kwa ajili ya kutafuta mademu.
Ilikuwa ni hivyo, aliwachukua washikaji zake na kuondoka kuelekea Jangwani Sea Breez (kabla haijavamiwa na watoto wa uswahilini) kutafuta mademu tu. Huko, alikuwa akiwapata wengi kutoka Mbezi Beach ambao walikwenda huko kuogelea au hata kufanya mambo mengine.
Kwa John na washikaji zake kila walipokuwa wakienda, hawakurudi mikono mitupu, walirudi na mademu waliokuwa wakihitaji lifti au hata namba za simu ambazo walizifanyia kazi ipasavyo.
Wikiendi ya siku hiyo waliamua kwenda huko kama kawaida. Muda wote ndani ya gari walikuwa wakizungumzia kuhusu wanawake tu, ni nani alikuwa fundi, yupi alikuwa mtamu zaidi ya wengine.
“Jamani kuna yule demu anaitwa Farida mnamkumbuka?” aliuliza Idrisa, mmoja wa marafiki zake.
“Yupi?”
“Yupi?” aliuliza John huku akiendesha gari.
“Yule demu kama Mpemba hivi! Nilimpata siku ile kule Kigamboni,” alijibu jamaa.
“Yeah! Yule ana mwili kidogo na tako la kuvutia?”
“Yeah huyohuyo!”
“Amefanyaje?”
“Yule demu mtamu ile kinoma!” alisema Idrisa kitu kilichomfanya John kupunguza mwendo kwani alihisi kwa stori walizokuwa wakipiga, wangeweza kupata ajali.
“Acha masihara!”
“Sure! Yule demu ni noma. Mpemba wa kwanza anayejua mambo. Dogo anapiga blowjob za maana aisee,” alisema Idrisa.
“Duuh! Vipi kuhusu anal, anaperform?” aliuliza Dotto, rafiki mwingine wa John.
“Hahaha! We jamaa fala sana,” alisema Idrisa na wote kuanza kucheka.
Waliendelea kupiga stori za mademu tu, kila mmoja alikuwa bize kuwazungumzia wanawake ambao alitembea nao. John naye hakutaka kubaki nyuma, aliwahadithia wenzake jinsi alivyokuwa akiwafunua wanawake mbalimbali mtaani, huko WhatsApp na Instagram.
Kila mmoja humo ndani alikuwa balaa, hakukuwa na mtu wa masihara, huko kwenyewe walipokuwa wakienda kila mmoja alijua kabisa alikuwa akienda kupata totozi za maana, achana na zile za uswahilini ambazo walizipiga sana.
Baada ya dakika kadhaa gari likaanza kuingia ndani ya eneo la Jangwani Sea Breez, wakateremka na kuanza kuelekea ndani.
Njiani kila mmoja alikuwa akikodoa macho, kulikuwa na watoto wakali ile kinoma, watowo wa kishua, wazuri, wenye mchanganyiko wa rangi ambao waliwaacha hoi.
Walikwenda mpaka sehemu ya vinywaji na kutulia, wakaagiza vinywaji na kuanza kunywa. Macho yao hayakutulia, bado walikuwa wakiangalia huko na kule mpaka macho ya Idrisa yalipotua kwa msichana mmoja mrembo, mtoto wa Kihindi ambaye alikuwa amekaa pembeni peke yake akinywa juisi.
“Oya! Mnamuona yule mtoto?” aliuliza Idrisa huku akiwaonyeshea wenzake.
“Mmh! Kazuri! Ila mimi na Wahindi, hapana! Nimepiga wengi halafu hawana maajabu!” alisema Idrisa.
“Mimi namfuata! Nataka nimuonje hata mmoja, nawaonaga tu kwenye muvi,” alisema Idrisa.
“Kumbuka kauli mbiu yetu!”
“HAKUNA DEMU MGUMU DUNIANI!” alisema Idrisa na kupeana tano.
Idrisa akaondoka na kuelekea kwa msichana yule, alijiamini, kauli mbiu yao iliwapa nguvu ya kumpata mwanamke yeyote waliyekuwa wakimtaka. Alipomfikia, akakaa pembeni yake na kuanza kuzungumza naye.
“Umejitenga sana, unaonekana mpweke mno! Akshey kakusaliti nini?” aliuliza Idrisa huku akimwangalia msichana huyo mrembo ambaye alibaki akitabasamu tu.
“Why Akshey?” (kwa nini Akshey)
“Is the only name I know. Tell me what the hell is going on,” (ni jina pekee ninalolijua. Niambie kitu gani kinaendelea?) aliuliza Idrisa.
“Men! I hate ya’ll,” (wanaume. Nawachukia wote) alisema msichana huyo.
“Including me?” (pamoja na mimi?) aliuliza.
“Yes! Ya’ll the same,” (ndiyo! Nyie wote mpo sawa) alisema msichana huyo na Idrisa kuanza kucheka kicheko cha chini.
“Ok! My name is Idrisa!” (Sawa! Naitwa Idrisa) alisema kijana huyo huku akimpa mkono.
“Shannia.”
Wakaanza kuongea, Idrisa alikuwa mkali kwa watoto kama hao, alijua kuzungumza, hata kama msichana alikuwa na mawazo tele, alijua ni kwa namna gani alitakiwa kumuondolea mawazo na kumfanya kujisikia mtu mwenye furaha kuliko wote duniani.
Alibaki akiongea naye, alimwambia mambo mengi kuhusu wanawaume, mambo ambayo hakuwa akiyajua lakini kwenye hayo yote alimwambia kitu kimoja cha muhimu sana kwamba kama kuna mchezaji fulani alifanya kitu fulani, hakutakiwa kuuchukia mchezo wa mpira wa miguu bali alitakiwa kumchukia mchezaji husika.
“Unamaanisha nini?”
“Hutakiwi kuyachukia mapenzi, mchukie yule aliyekufanya ulie,” alisema Idrisa huku akiendelea kujifanya mshauri wa mapenzi bora kuliko wote katika dunia hii.
Wakati yeye akiendelea kuongea, macho ya John yalikuwa huku na kule, alikuwa akiwinda, hakuwahi kuondoka mtupu hapo Jangwani Sea Breez, alijua kuwachukua wanawake wa kila aina na muda huo alikuwa mahali hapo huku akiendelea na mawindo yake.
Kwa kuwa alihitaji kujua ni nani ambaye alikuwa hapo, akaingia kwenye makundi yake ya WhatsApp na kuandika kwamba alikuwa mahali hapo, kama kulikuwa na mtu karibu basi watafutane kama kuzoeana.
“Nitafute! Nipo humohumo!” alipokea meseji kutoka kwa Penina.
Kwanza akashtuka, hakuamini alichokuwa akikisoma, haraka sana akasimama kutoka alipokuwa na kuondoka, akaenda sehemu fulani iliyojificha kidogo ili hata kama Penina alikuwa hapo asimuone, huko akaanza kuchati naye.
“Una uhakika upo hapa?” aliuliza.
“Kwa nini nikudanganye! Nipo! Ila nitafute, sina muda wa kumtafuta mwanaume,” aliandika msichana huyo.
Hiyo ilikuwa kazi aliyopewa, hakutaka kupiteza muda, haraka sana akaanza kumtafuta msichana huyo. Alitembea kila kona, alikuwa makini kabisa, picha zake zilikuwa kwenye simu, aliziangalia ili asimpotee pindi atakapomuona mahali fulani.
Alimtafuta na kumtafuta lakini hakufanikiwa kumuona, akaamua kumuandikia meseji kwamba hakumuona, alihitaji kumwambia ni mahali gani alipokuwa.
“Mbona mimi nakuona?”
“Unaniona! Acha utani! Upo wapi Penina?”
“Hahaha!”
“Unanitania, right?”
“Kweli tena! SI umevaa fulana nyeupe ya kubana mwili na jinsi ya bluu, chini una raba nyeupe?”
“Exactly! Sasa upo wapi?”
“Ndiyo unitafute!” alisema msichana huyo.
Ilikuwa ni kazi kubwa lakini hakutaka kukubali, kwa mwanamke, alikuwa tayari kufanya kitu chochote kile lakini si kuona akimkosa. Alimtafuta sana msichana huyo, alitamani sana kuonana naye na leo hii alimwambia kwamba alikuwa mahali hapo, kwa nini asijitoe na kumtafuta kwa nguvu zote kama alitafuta kazi.
Baada ya dakika kama kumi macho yake yakatua kwa msichana aliyekaa mbali na wenzake, alimuona kwa nyuma, kwa jinsi alivyofunga nywele zake, alizibana kwa staili ya aina yake, hakutaka kusubiri, akaanza kumsogelea.
Alipolifikia kundi la wanawake wale, akamshika bega kwa nyuma na msichana huyo kugeuka. Kila mmoja aliyekuwa mahali hapo alibaki akimshangaa John, hawakumuelewa alikuwa nani na kwa nini alimfuata Penina na kumshika bega kwa nyuma.
“Nimekubamba!” alisema John huku akitoa tabasamu pana.
“Mr Johnny!”
“Yeah! Thats me...” (yeah! Ndiye mimi) alisema John na Penina kusimama kisha kumkumbatia.
Wasichana wale waliendelea kushangaa. John naye alipenda sifa, alimng’ang’ania msichana huyo vilivyo lakini kila alipoiga macho yake kwa marafiki zake waliokuwa pale, walikuwa mademu wakali ile kinoma.
“Jamani huyu anaitwa John,” alimtambulisha Penina kwa marafiki zake.
“Tunafurahi kumfahamu!”
“Ila na mimi nataka kuwajua pia, watambulishe bhasi! Yaani wote ni warembo, hivi mlichaguana kuwa marafiki na wale wabaya mkaacha wajichague wenyewe kwa wenyewe?” aliuliza John, kwa jinsi alivyosikika tu alikuwa mchangamfu kupita kawaida, wote wakaanza kucheka.
“Hahaha!” naye Penina akaanza kucheka, halafu akaanza kuwatambulisha.
“Huyu anaitwa Esta, yule Amanda, yule kule Nasria na yule wa mwisho anaitwa Pamela! Aya sema unamtaka nani,” alisema Penina.
“Mimi nawataka wote!”
“Eti unawataka wote! Fala sana wewe.”
“Kwani kuna dhambi jamani? Mbona King Mswati anaoa kila mwaka....”
“Sasa si yeye!”
“Basi nasilimu! Nakuwa Muislamu halafu naoa wake wanne, hapo pia mtanikataa?” aliuliza John.
Muda wote alikuwa mtu wa kuzungumza. Mahali hapo alitawala jukwaa la kuongea, aliongea kama chiriku kiasi kwamba mpaka wasichana hao wakafurahia uwepo wake mahali hapo.
Alimsahau kabisa Penina, wasichana wengine waliokuwa mahali hapo walikichanganya kichwa chake kupita kawaida. Hasa yule Nasria, mtoto chotara, alikuwa mrembo ile mbaya na kanguo alikokavaa kalikafanya kitovu chake kuwa nje, basi John akazidi kupagawa.
Kwa jinsi John alivyoonekana, Penina alijua hali ya hewa ingebadilika kwani wale marafiki zake walionekana kupagawa mno kwake.
Akamchukua na kuondoka naye pembeni, alimpenda mwanaume huyo na hakutaka kuona akichukuliwa na marafiki zake. Pale pembeni wakaanza kupiga stori, John hakutaka kuchelewa, alimwambia Penina jinsi alivyokuwa akimuelewa, kwake alikuwa msichana wa kipekee kupita kawaida.
“Mh! Wanaume nyie!” alisema Penina.
“Sure! Penina! Ninakupenda mno, tatizo lenu mnataka kudanganywa, ukweli hamtaki kuusikia,” alisema John huku akicheka.
“Eti tunapenda kudanganywa. Aya hebu nidanganye!”
“Ninatamani sana kula mtoto wa kishua, nyama hiyo sijawahi kuila,” alisema John.
“Hahaha! Sasa nani wa kishua!”
“Wewe hapo! Hebu jiangalie kwanza. Hivi huwa unapaka lotion gani?”
“YA kawaida tu!”
“Nyie mnaosema ya kawaida ni zile za kutoka Dubai moja kwa moja. Hahaha!”
“Chizi wewe!” alisema Penina.
“Kwa hiyo?”
“Kuhusu?”
“Kucheza!”
“Kucheza nini?”
“Kuch Kuch Hotae...”
“Fala sana wewe!”
“Serious! Penina, hebu tutafute sehemu tuongee kidogo!”
“Kwani hapa hapafai?”
“Nope! Nasikia aibu!”
“Eti nasikia aibu! Wewe unataka wapi?”
“Ndani ya gari langu!”
“Mh!”
“Pleaseeee...”
Hiyo ndiyo ilionekana kuwa sehemu maalumu ya wawili hao kukaa na kuzungumza pamoja. Hakukuwa na tatizo lolote lile, Penina akakubali na kwenda naye huko, wakaingia ndani na kukaa kiti cha nyuma.
Kwa jinsi msichana huyo alivyokuwa, John aliona kabisa hiyo ilikuwa siku yake, alitakiwa kumla msichana huyo kwa kuwa kipindi kirefu sana alimfuatilia lakini hakupata bahati ya kuonana naye.
“Leo ninataka kuamini!” alisema John.
“Kuamini nini?”
“Kama kweli ni Tundu la Mdomo wa Chupa kweli au unanizingua tu,” alisema John na Penina kuanza kucheka.
John hakutaka kulemba, hakuwa na nafasi ya kuongea naye sana, akajisogeza kwa msichana huyo na kutaka kuubusu mdomo wake, akaupeleka pembeni.
“Unataka kufanya nini?” aliuliza Penina.
“Kwani nilikwambiaje?”
“Hebu acha utani! Haiwezi kutokea, unakumbuka nilikwambiaje?” aliuliza msichana huyo.
“Penina! Hata kuonja ladha ya mate yako unanibania kweli?”
“Huanza na mate...baadaye utasema nina kifua kizuri unataka kukiona, utaendelea hivyohivyo mpaka chini na mwisho wa siku unanibanjua humuhumu,” alisema Penina.
“Hahaha! Mtoto mhuni sana wewe! Yote umeyajulia wapi?”
“Kwani mimi siwajui nyie! Kwa leo, hapana kwa kweli,” alisema Penina.
Aliongea kama utani lakini alimaanisha. Ni kweli ilishindikana kama alivyomwambia japokuwa naye John alijidai kung’ang’ania mno.
Hakukuwa kilichofanyika mpaka walipoteremka na kuelekea kule walipokuwa marafiki zake na kuanza kupiga nao stori, muda wa kuondoka ulipofika, John akainuka na kuondoka naye.
Kila mmoja mahali hapo alimwangalia Penina, walihitaji kujua zaidi kuhusu mwanaume huyo kwani alionekana kuwa tofauti, alikuwa mchangamfu kupita kawaida.
“Jamani! Mbona mnamuulizia sana?” aliuliza Penina.
“Tunamtaka. Naomba namba yake,” alisema Esta.
“Na mimi pia. Wale wanaume wa vile ndiyo tunawatafuta,” alisema Nasria kitu kilichomchanganya sana Penina, yaani kwake John alionekana kama bati lakini cha kushangaza, kwa wenzake hao alionekana kuwa almasi, kama angeleta masihara, hao marafiki zake wangemchukua huyo John, hata kama hakutaka kuwa naye, hao marafiki zake wakamfanya kuanza kuvutiwa naye.
“Mh! Niwape namba! Haiwezekani! Sitoi namba. Ila ana nini yule mwanaume? Au ana kitu ambacho mimi sijakiona na wenzangu wamekiona? Hapana, siwezi kukubali, hebu nimuonje kwanza,” alijisemea Penina huku akiwaambia marafiki zake kwamba hawezi kutoa namba za John.
*Je, nini kitaendelea?*
Sent using
Jamii Forums mobile app