CHOMBEZO: Jamani dada Martha.. LOOO!

CHOMBEZO: Jamani dada Martha.. LOOO!

SEHEMU YA 18

ILIPOISHIA
“Ngoja nimtumie ujumbe halafu ajibu, ndiyo mtaamini,” alisema mama Anna huku akiandika ujumbe wa simu…
“Baby, nimefurahi sana kwa mechi ya leo. Halafu mechi ya kuichezea nyumbani kwako kama vile ni nzuri kuliko gesti au hotelini. Nimeipenda sana.”
SONGA NAYO MBELE…
Baada ya kuandika ujumbe huo, mama Anna aliwaonesha wenzake kisha akautuma kwenda kwenye namba ya Roi ambayo aliisevu kwenye simu yake kwa jina la ‘Wa Martha.’
Ni ndani ya dakika tatu tu, meseji ikajibiwa…
“Mimi pia nimeinjoi sana baby. Da! Yaani wewe ni kiboko, umeniteka kabisa Martha. Kesho twende tena nyumbani kwangu kama leo.”
Mama Anna alipoisoma meseji hiyo akawaonesha wenzake, wakacheka mpaka kupiga mikono ‘pa…pa’…
“Mimi nawaambieni, lazima wajina wangu aachike hivihivi anaona. Nimempa biti yule kaka ambazo mwenyewe hajawahi kupewa tangu azaliwe.”
Baada ya mazungumzo yao, Martha aliingia ndani kwake na kuwaacha wenzake wakiendelea na mazungumzo.
***
Roi alikaribishwa chumbani kwa Martha kwa mabusu mfululizo huku akipewa pole kwa kazi za mchana kutwa halafu akaambiwa…
“Baby, nilikumbuka kwamba kule nyumbani kwako baada ya kufunga, funguo uliiweka kulekule au ulikuja nayo?” aliuliza Martha…
“Iko kwenye gari.”
“Nilipenda kwenda kufanya usafi baby, labda kesho sasa.”
“Kesho sawa, utakwenda. Saa ngapi?”
“Jioni, kwenye saa kumi hivi.”
***
Usiku wa siku hiyo, Martha alihisi kitu tofauti kwa Roi. Licha ya kumshikashika ili achaji lakini alionekana hana habari na kwanza alikuwa mbali…
“Sweet, mbona kama upo mbali kimawazo?” aliuliza Martha…
“Hapana, kuchoka tu na shughuli.”
“Mmh! Baby jamani! Sasa ukichoka hivyo mimi nitapataje haki yangu?”
“Kesho bwana,” alisema Roi akilala baada ya kutoka kuoga.
***
Saa kumi na mbili, Martha alimka na kuamza kumshikashika Roi sehemu mbalimbali za mwili, hasa zile zenye kuamsha joto la mahaba. Roi alimgeukia, wakapashana joto zaidi na kuingia uwanjani kusakata mechi.
Kulikucha kabisa, Martha alitoka kwa lengo la kumtengea maji ya kuoga jamaa yake ambapo alikutana na mama Anna…
“Mambo mama Anna?” alisalimia Martha…
“Poa, umeamkaje?”
“Ah! Mi mzima bwana. vipi shemeji yangu?”
“Ameamka salama, anataka kuondoka kwenda kazini kwake muda si mrefu, namwekea maji ya kuoga.”
“Sawasawa, lazima upalilie bwana. Waoaji siku hizi hakuna,” alisema mama Anna akiingia ndani kwake. Lengo lake lilikuwa ni kumtumia meseji Roi kwani alijua Martha hatarudi muda ule chumbani…
“Baby umeamkaje?” alituma meseji Mama Anna.
“Poa, vipi wewe sweet, umeamkaje?”
“Mimi mzima tu. Ni kukumisi tu.”
“Mh! Je, mimi? Yaani natamani tungelala wote.”
“Usijali baby, kuna siku. Unakwenda kazini?”
“Yeah! Ndiyo nataka kujiandaa.”
“Leo vipi, tutaonana baby wangu?”
“Muhimu, si nilikwambia muda ule mpenzi wangu!”
“Saa ngapi na wapi?”
“Nitakujibu maana…” Roi aliikata meseji hiyo na kumpa wakati mgumu mama Anna kutafuta kwa nini meseji iliishia kwenye maana…
“Maana nini tena baby?”
“Nitakwambia Martha.”
Roi alisema maana kwa sababu, jana yake, Martha wake alitaka funguo ili akafanye usafi nyumbani kwake siku hiyo jioni.
***
Roi alitoka kitandani kwenda kuoga ambapo uani alikutana na wale wapangaji wenzake na Martha akiwemo mama Anna…
“Jamani mmeamkaje?” alisalimia Roi akiwa ndani ya taulo tu, kifua wazi. Alishangaa kuwaona wanawake wote wakimtumbulia macho yeye tena waziwazi na si kwa kuibia…
“Tumeamka salama, sijui wewe?” walimjibu, lakini mama Anna akaenda mbele zaidi kwa kusema…
“Sijui wewe baby wangu.”
Wakati anamalizia kusema baby wangu, Martha alitokea, akasikia.
Ili kuonesha kwamba alisikia kitu kisicho cha kawaida, Martha alimtumbulia macho mama Anna kama anayemuuliza unasemaje wewe?
“Vipi wajina?” mama Anna alijibalaguza kiaina kwani hata yeye alihisi maneno yake yalisikika na Martha…
“Poa tu,” Martha alijibu kwa mkato sana tena akiwa ameuelekeza uso wake chini.
Wakati huo, Roi alishazama bafuni kuoga lakini naye akijua maneno ya mwanamke huyo yamesikika na Martha…
“Hawa wanawake wa uswahilini hawa. Yaani kuvumilia hawawezi kabisa,” alisema moyoni Roi akiwa ameshaanza kuoga.
***
“Baby,” Martha alimwita Roi chumbani akiwa amekaa kwenye kitanda…
“Yes baby…”
“Yule mwanamke pale uani alikuitaje?”
“Yupi?”
“Yule mama Anna.”
“Mama ni yupi kati ya wale?” Roi alijizungusha huku akijua anazungumziwa nani.
 
SEHEMU YA 19

ILIPOISHIA:
“Yes baby…”
“Yule mwanamke pale uani alikuitaje?”
“Yupi?”
“Yule mama Anna.”
“Mama ni yupi kati ya wale?”
Roi alijizungusha huku akijua anazungumziwa nani.
JIACHIE MWENYEWE SASA…
“Yule mwenye umbo namba nane!”
“Mi sikumsikia, kwani alisemaje baby?”
“Ha! Una uhakika sweet? Mi nimemsikia akikusalimia kwa kukwambia sijui wewe baby?”
“Mh! Kweli anaweza kunisalimia hivyo mimi? Mbona sifahamiani naye zaidi ya hapa kwako. Sasa mimi niwe baby wake kivipi jamani?”
“Ndiyo nimeshangaa pale baby.”
***
Roi aliondoka kwenda kwenye shughuli zake, nyuma Martha aliamua kuumiza kichwa kuhusu mama Anna.
Kuna wakati alivizia mama Anna yuko bize, akamwingia mmoja wa wapangaji wenzake...
“Mambo shosti?”
“Poa, vipi Martha?”
“Poa. Hivi, asubuhi pale wewe si ulikuwepo uani wakati mgeni wangu anakwenda kuoga?”
“Nilikuwepo ndiyo, vipi kwani?”
“Hivi, mama Anna alimsalimia vipi mgeni wangu?” aliuliza Martha huku akimkazia macho mpangaji huyo.
“Alimsalimia kawaida tu. Alimwambia salama sijui wewe hapo?”
“Kweli?”
“Kweli. Kwani wewe ulisikiaje?”
“Mimi nilisikia akisema salama sijui wewe honey.”
“Hapana, alisema sijui wewe hapo.”
“Oke basi, lakini usimwambie chochote mama Anna.”
“Sawa, wala simwambii.”
***
Jioni, saa kumi na moja, Roi ndiye aliyeanza kumtumia meseji mama Anna ambapo mchana kutwa wa siku hiyo hawakuwasiliana...
“Mzima baby?”
“Mzima sweet, wewe?”
“Mzima. Wapi hiyo?”
“Niko home, wewe?”
“Mimi nipo njiani. Unapakumbuka vizuri nyumbani kwangu?”
“Ndiyo. Kumetokea nini kwani baby wangu?”
“Unaweza kuja?”
“Sasa hivi?”
“Yes, mimi naelekea huko muda si mrefu nitakuwa nimefika.”
“Poapoa.”
Mama Anna aliwafuata wenzake, akawatonya kuhusu kuitwa na bwana wa Martha nyumbani kwake...
“Safi sana. Nenda katese mwanamke mwenzetu.”
“Sawa, baadaye basi.”
Mama Anna alibeba nguo pea moja. Alipanga atakazovaa akienda siyo atakazovaa akirudi.
Wakati anatoka, Martha alikuwa amekaa nje na wapangaji wenzake...
“Mwenzetu mtoko wa wapi huo?” aliuliza Martha.
“Kwa shemeji yako.”
“Msalimie basi, siku nyingine mlete tumwone.”
“Wewe hujatuonesha wako lakini. Sanasana huyu wa sasa unasema ni kaka yako.”
“Ee! Kaka yangu jamani. Mjue ni kaka yangu, lakini mbona huwa mnamuita shemeji wakati niliwaambia ni kaka yangu!” alisisitiza Martha.
Walicheka wote, mama Anna akatokomea zake kwa kuchukua Bajaj hadi nyumbani kwa Roi. Anashuka tu, Roi naye anaegesha gari hapo.
Waliingia sambamba ndani huku Roi akimuuliza habari za alikotoka...
“Martha hajakuuliza kitu?”
“Hapana, kwani kuna kitu?”
“Aliniuliza asubuhi vile ulivyonisalimia kwa kuniita baby.”
“Kweli?” alishtuka mama Anna...
“Kweli, lakini usijali, yaliisha palepale. Alijua alisikia vibaya.”
Wawili hao hawakutaka kupoteza muda, waliingia chumbani, wakachojoana na wakapanda kitandani kuanza mechi.
Safari hii, mama Anna aliongeza gia namba kubwa zaidi kuliko jana yake. Mfano, wakiwa uwanjani, alimtoa kitandani Roi wakatembea mpaka bafuni na kurudi huku wakiendelea kucheka, Roi akapata ushindi wa kwanza ile anafika tu kitandani. Alianguka chini kwa jinsi alivyochokeshwa.
***
Martha kule nyumbani, akakumbuka kwamba alipanga kwenda kufanya usafi nyumbani kwa Roi, hivyo alijiandaa, akatoka akipanga kwamba atakapokaribia kufika ampigie simu Roi kumwambia ampitishie funguo za nyumba
 
SEHEMU YA 20

ILIPOISHIA :
Martha kule nyumbani, akakumbuka kwamba alipanga kwenda kufanya usafi nyumbani kwa Roi, hivyo alijiandaa, akatoka akipanga kwamba atakapokaribia kufika ampigie simu Roi kumwambia ampitishie funguo za nyumba.
JIACHIE MWENYEWE SASA...
Aliwaaga wapangaji wenzake akisema anatoka mara moja...
“Jamani natoka, nitarudi lakini,” alisema Martha akiwa tayari kwenye ngazi.
“Poapoa.”
Martha alichukua usafiri wa Bajaj, akapanda hadi alipokuwa akikaribia nyumbani kwa Roi, akampigia simu...
“Uko wapi baby?”
“Niko Magomeni.”
“Mi nakaribia kwako, nipitishie funguo nifanye usafi.”
Roi moyo ulimlipuka puu! Maana alijua Martha atakumbana na mama Anna, kama si nje basi mitaa hiyo.
“Mh!” aligunia moyoni, akatafuta uongo wake...
“Funguo niliziacha nyumbani kwako mbona.”
“He! Kweli?”
“Yes! Kwenye nini?”
“Kwenye begi langu, kama siyo basi kwenye suruali niliyovaa jana. Kacheki.”
Martha alimwamuru dereva wa Bajaj ageuze amrudishe nyumbani kwake. Wakati anageuza, mama Anna alimwona mita chache, yeye alikaa kwenye kiduka jirani na kwa Roi, akauchuna, akazungusha sura.
Alipoiona Bajaj imepotea, akampigia simu mpangaji mmoja...
“Martha yuko hapo?”
“Ametoka.”
“Alisema anakwenda wapi?”
“Hajasema, kasema natoka kidogo tu. Vipi kwani?”
“Mh! Kaja mpaka nje kwa huyu jamaa yake, kageuza. Yuko na Bajaj.”
Wakati mama Anna akiendelea kuongea na mpangaji mwenzake huyo, mara simu yake ikawa inaita, kuangalia ni Roi, akakata simu hiyo na kupokea ya Roi...
“Niambie baba.”
“Uko wapi mama?”
“Niko nje kwako hapa.”
“Ha! Martha hajakuona kweli? Maana kaja hapo.”
“Nimemuona, lakini yeye hajaniona. Kwani kaja kufanya nini tena?”
“Eti alikuja kufanya usafi. Nimemdanganya kwamba funguo ipo nyumbani kwake.”
“Kwa hiyo kaifuata?”
“Kaifuata. Sasa mimi nakuja hapo dakika tano tu.”
“Poa.”
Baada ya dakika tano kweli, Roi akawa amefika nyumbani kwake, akashuka, akafungua geti na kuingiza gari ndani. Akamwingiza na mama Anna ndani, tena mpaka chumbani.
“Uzuri wake hata akija, hawezi kuliona gari ndani. Nitamwambia niko njiani bado,” alisema Roi kwa sauti ya kuibiaibia.
Martha alifika na kuangalia funguo sehemu zote alizoambiwa, hakuziona, akampigia simu...
“Baby, sijaona funguo bwana, utakuwa nazo kwenye gari, hebu angalia vizuri.”
“Ngoja niangalie.”
“Kwani uko wapi?”
“Nipo barabarani bado.”
“Poa.”
Roi alifunga milango yote, akazama chumbani ambako alimkuta mama Anna akiwa amejilaza na ameshajichojoa nguo zote. Alikuwa kama alivyozaliwa. Na kwa kujua hilo, alipomwona Roi ameingia, akajitingisha makusudi pale kitandani, Roi hoi. Alianza kuhema kimahaba.
“Si unaoga kwanza baba?” aliuliza mama Anna akiitoa sauti kwa kupitia kwenye tundu za pua.
“Yes,” Roi alisema kwa sauti nzito huku macho yako kwenye mwili wa mama Anna pale kitandani.
Roi alizivua nguo zake na kuzitupa chini kama vile hatazivaa tena katika maisha yake...
“Teh! Teh! Teh!” alichekacheka kwa kicheko cha uchu huku akimfuata mwanamke huyo pale kitandani...
“Jamani baba, si umesema unakwenda kuoga kwanza.”
“Yeah! Lakini kuna nini kama nita...nita naniihii kabla sijakwenda kuoga..? Teh! Teh!” Roi alibabaika. Hapo tayari alikuwa mwilini mwa mama Anna. Alilala na kumpapasapapasa sehemu mbalimbali za mwili.
Mama Anna naye akachangamka maana aliguswa, akapatwa na hisia za mapenzi, hasa kwa joto la Roi...
“Kwa hiyo utaoga baadaye?” aliuliza mama Anna...
“Au ngoja nikaoge sasa hivi,” alisema Roi, mama Anna akamzuia maana sasa na yeye mzuka si ulishapanda!
“Hakuna hapa, kama ungetaka ungekwenda tangu muda ule. Mimi mwenzio tayari sasa,” alisema mama Anna.
“Tayari nini?” aliuliza Roi akijifanya hajui lakini ukweli ni kwamba alikuwa anajua tayari nini.
“Kwani hujui?”
“Sijui,” alijibu Roi.
Mama Anna akapeleka mkono wake mmoja na kushika maiki akiashiria utayari wake uko wapi.
Roi naye akaunganisha hisia, wakabilingishana mpaka wote wakawa hoi, wanahema tu. Mama Anna akavuta mpira uwanjani, mchezo ukaanza kupigwa huku ushangiliaji ukiwa mkubwa kwa pande zote mbili.
Maneno yote, mama Anna aliyatumia, Roi akawa kama amepungukiwa akili, alisema yasiyosemwa.
***
Martha alipoona muda unakwenda aliamua kutoka tena akiamini, Roi alishaziona funguo na sasa atapitia nyumbani kwake ili wakutane.
Alipanda Bajaj tena mbele ya wale wapangaji wenzake.
Ile anapotea tu, yule mpangaji aliyepigiwa simu na mama Anna akamtumia meseji mama Anna...
“Martha katoka hapa tena, nahisi anakuja hukohuko.”
Mama Anna hakupata nafasi ya kuisoma meseji hiyo kwani wakati inaingia ndiyo kwanza yeye alikuwa katikati ya mashambulizi uwanjani akitafuta ushindi na alishatangaza kwamba anakaribia kuupata.
Hata alipoupata, Roi hakumwachia ili na yeye apate pointi yake moja ili kusiwe na wa kumzidi nguvu mwenzake. Mama Anna alitumia ufundi kidogo tu, Roi akawa akihangaika mpaka jasho jembamba likamchuruzika, ambapo mama Anna alilimudu kuliondosha kwa taulo.
***
Martha alifika nje ya nyumba na kumpigia simu Roi. Simu iliita kule chumbani, Roi kwa vile alishashinda, akatoka kwa mama Anna na kuiwahi...
“Du! Wajina wako anapiga,” alisema.
“Sasa. Anaweza kuwa nje?” aliuliza mama Anna...
“Inawezekana,” alisema Roi lakini hakuipokea simu hiyo.
Mama Anna naye akakumbuka, simu yake akaifuata, akakutana na ile meseji. Alipoisoma, akamwonesha Roi...
“Martha katoka hapa tena, nahisi anakuja hukohuko.”
Roi alitumbua macho pima, akasimama akiwaza, akasema...
“Kwa hiyo yupo nje hapo?”
“Ndiyo maana yake,” alijibu mama Anna.
Martha alishangaa simu ya Roi kuita bila kupokelewa kwani si kawaida yake.
Akaenda kwenye kile kiduka cha jirani...
“Dogo hujambo?” alimsalimia muuzaji.
“Sijambo.”
“Eti, huyu kaka anayekaa hapa huwa anafika muda gani?”
Tukutane siku ya Ijumaa wiki hiiiiiiiiii.
 
SEHEMU YA 21

ILIPOISHIA
“Dogo hujambo?” alimsalimia muuzaji.
“Sijambo.”
“Eti, huyu kaka anayekaa hapa huwa anafika muda gani?”
SASA ENDELEA...
“Mh! We ni nani kwani?”
“Mgeni wake.”
“Kutoka wapi?”
“Tanga.”
Muuza duka huyo alimkodolea macho Martha akiwa anaonekana haamini kama alitokea Tanga. Tanga bila hata kibegi cha nguo!!
“Kwani namba yake ya simu huna?” aliuliza muuza duka huyo.
“Nampigia hapokei. Nikasema nije hadi hapa ili kama anakuja muda huu nimsubiri kama si muda wake nikatafute gesti ya kulala.
Muuza duka huyo alijua kuna kitu kilimfanya Roi asipokee simu. Na kitu hicho si kingine ni jamaa huyo kuzama ndani na mwanamke mwingine aliyekuwa amekaa kwenye benchi nje ya duka lake.
Kwa hiyo uamuzi ulikuwa kwake. Aseme ukweli au adanganye.
Moyoni mwake aliona Roi mwenyewe alitakiwa kuwa muwazi katika mipango yake kuhusu wanawake. Si vizuri kugonganisha...
‘’Mimi nimemwona kaingia ndani muda si mrefu,’ alisema muuzaji huyo.
Martha akashangaa...
“Kwa miguu?” aliuliza.
“Na gari.”
Martha alitupia macho kwenye geti na kubaini kwamba, ni kweli gari linaweza kuwemo ndani halafu mtu aliye nje asilione...
“Aliingia na nani?”
“Mwanamke mmoja hivi. Alimsubiri kwa muda mrefu hapohapo nje.”
“Mwanamke mmoja hivi! Kavaaje?”
“Huyo mwanamke kavaa haya magauni yenu ya siku hizi, marefu mpaka miguuni, amelaza nywele kwa nyuma, mweupe kiasi, ana figa namba nane.”
Kwa haraka sana, Martha alimuweka kichwani mama Anna kwani anakumbuka ndiye aliyevaa hivyo inavyosemwa.
“Huyo ni mama Anna tu. Yaani kumbe...mh! Yaani mama Anna na Roi ni wapenzi? Mbona siamini. Wameanzaje kwanza?”
Martha aliinua simu yake akampigia mpangaji mmoja na kuzungumza naye...
“Hivi unaweza kuamini mama Anna alipotoka hapo kumbe amekuja nyumbani kwa yule mtu wangu?”
“Kweli?”
“Kabisa. Nimepewa ushahidi wote.”
“Kwa hiyo?”
“Wamo ndani na geti limefungwa.”
“Mh! Mama Anna naye bwana. Ana maana gani sasa kufanya hivyo kwa mtu wa karibu kama wewe?”
“Ndiyo hapo sasa. Mimi leo sitoki hapa getini. Nipo tayari hata kulala hapahapa,” alisema kwa uchungu Martha na kukata simu.
***
Roi na mama Anna walikuwa chumbani sasa, kitandani, wakigalagazana kwa mahaba mazito huku mwanamke huyo akilia kilio cha uongo ili kumkoleza zaidi mwanaume huyo pale kitandani.
Wote walikuwa wamelegea macho kwani kwa mama Anna yeye alishajua jinsi ya kumnasa Roi huku yeye Roi akiwa hoi bin taaban.
Simu ya mama Anna iliita mpaka ikakata, ikaita tena mpaka ikakata, ikaita tena...
“Mh! Hiyo simu itakuwa ya umuhimu kwangu,” alisema Roi na kumtaka mama Anna aipokee...
“Hakuna lolote, haina umuhimu wowote, ngoja niizime tu,” alisema mama Anna akiifuata.
Kabla hajaizima aliangalia missed calls akakuta mbili na zote ni za wapangaji wenzake, akahisi kitu. Akampigia wa kwanza...
“Vipi mama nanihii...”
“Mwenzangu, Martha yupo getini. Kasema ana ushahidi umo ndani kwa jamaa yake na hatoki mpaka kesho asubuhi.”
Palepale mama Anna alikata simu, akamwangalia Roi. Naye Roi akamuuliza...
“Vipi kwani?”
“Martha yupo getini. Lakini ishu si hiyo bali amejua mimi nimo ndani, eti ana ushahidi.”
Roi alikumbuka kwamba, atakuwa ameambiwa na muuza duka ambaye alishuhudia kila kitu...
“Mmh! Atakuwa ameambiwa na muuza duka. Loo! Sasa?”
“Hata sijui. Kwani wewe hofu yako ipo kwa kiasi gani?” mama Anna alimuuliza Roi.
“Mimi sina wasiwasi wowote ule. Nimeamua kuwa na wewe japo kibinadamu nitakuwa nimefanya makosa makubwa, kumuumiza mtu jambo ambalo silipendi katika maisha yangu,” alisema Roi kwa sauti ya upole.
Alitoka kitandani, akavaa. Mama Anna naye akatoka kitandani, akamfuata kwa nyuma yeye akiwa amejizungusha upande wa kanga. Walifika sebuleni, wakaangalia kwa nje kupitia nafasi ya matundu ya ukuta wa fensi. Walimwona Martha amesimama dukani akizungumza na muuza duka.
Sura ya Martha ilitafsiri uchungu wa maumivu ya kutendwa. Ikawa kama imejikunja, Roi akahisi huruma...
“Martha... Wajina wako anaumia sana. Sasa itabidi nikutoe kiaina. Pita mlango wa nyuma, nenda mahali hapo nyuma kuna baa, kakae.”
“Mh!” Aliguna mama Anna, akatoa wazo...
“Sawa lakini turudi chumbani, nipe haki yangu kwanza ndiyo nitoke, siwezi kutoka hivihivi wakati uliishaanza kunipandisha mzuka wangu na mzuka wangu ukinipanda mimi akili zinachanganyikiwa kabisa.”
“Kuhusu hilo tu, twende sasa hivi.”
Walikwenda chumbani ambako Roi aliikuta simu yake ikiendelea kuita kwa namba ya Martha.
Mama Anna alikimbilia moja kwa moja kwenye kitanda huku akitupa kanga chini.
Alipokuwa juu ya kitanda akakaa mkao wa mechi tayari akijua anatakiwa kutoka ndani ya nyumba hiyo lakini moyoni alihakikisha anatoa mapigo ambayo, Roi anaweza kuamua asitoke tena na Martha kama kulala nje ya geti alale tu.
Roi, kuona mkao wa mama Anna alichanganyikiwa. Kama paka aliyeona panya. Akaenda kitandani kwa staili ya kuruka kama golikipa wa timu maarufu ya Ulaya...puu!!
Je, nini kilitokea? Usikose
 
SEHEMU YA 22


ILIPOISHIA:Alipokuwa juu ya kitanda akakaa mkao wa mechi tayari akijua anatakiwa kutoka ndani ya nyumba hiyo lakini moyoni alihakikisha anatoa mapigo ambayo, Roi anaweza kuamua asitoke tena na Martha kama kulala nje ya geti alale tu.
Roi, kuona mkao wa mama Anna alichanganyikiwa. Kama paka aliyeona panya. Akaenda kitandani kwa staili ya kuruka kama golikipa wa timu maarufu ya Ulaya...puu!!
SHUKA NAYO HAPA...
Palepale alianza kuserebuka na mchezo huku mama Anna akimwangalia kwa hisia kali kama vile alikuwa akitumbuliwa jipu.
Mama Anna aliamua kujilegeza kabisa hivyo alitoa ushirikiano wa hali ya juu bila kuonesha dalili hata ya chembe kwamba kuna jambo hakubaliani na Roi...
“E...eti baby,” aliita Roi...
“Niambie baba...”
“Unaweza kuhama pale?”
“Kuhamia wapi baba angu?”
“Nitakaposema mimi?”
“Naweza ndiyo mume wangu.”
Roi kuitwa mume ndiyo kabisa, akajikuta anawewesekea uwanjani na kelele za mahaba kama vile yeye ndiye mama Anna.
***
Kule nje, Martha alitawala benchi la nje ya duka, mawazo yake yalikuwa usahihi wa mama Anna kuwepo au kutokuwepo ndani ya nyumba ya Roi...
“Ina maana kumbe niliposema nilimsikia mama Anna akimwita Roi baby nilikuwa sahihi? Lakini hawa walikutana wapi mpaka wakafahamiana?
“Kwa pale nyumbani hapana, haiwezekani. Lini kwanza? Na ilikuaje? Siku zote, Roi anakuwepo wakati ambao na mimi nipo, akitoka kurudi usiku...
“Halafu pia mbona si muda mrefu, Roi kaja kwangu! Hawa huenda wanajuana kabla ya hapa. Itakuwa hivyo, wanajuana kabla ya hapa,” aliwaza moyoni Martha akijihisi unyonge f’lani hivi.
“Lakini wewe Mangi utakuwa unamjua vizuri sana huyu kama anayeishi hapa. Hivi, ni mwadilifu kiasi gani?” Martha alimuuliza muuza duka...
“Nani, Evender?” muuza duka aliuliza naye...
“Kwani huyu kaka mwenye nyumba hii anaitwa Evender?”
“Ndiyo.”
“Mh! Siyo Roi?”
“Mh! Mi silijui jina la Roi, namjua kama Evender.”
Martha alianza kuingiwa na wasiwasi zaidi. Akahisi huenda Roi kujiita Roi alimwingiza mkenge. Na kama ni kweli halafu mpaka wameingia kwenye uhusiano hakusema ukweli wa jina lake, Martha alianza kuona kumbe alikutana na mwanaume tapeli...
“Labda ni jina la mtaani,” alisema Martha na kuomba Mungu iwe hivyo.
Mara mzee mmoja mteja aliwasili dukani hapo na kumwangalia sana usoni Martha...
“We binti kama nakufahamu,” alisema mzee huyo...
“Mimi sikufahamu.”
“We siye mdogo wake Benard?”
Ni kweli, Martha ana kaka yake anaitwa Benard. Ni machepele ile mbaya...
“Kweli Benard ni kaka yangu,” alisema Martha...
“Sasa je? Sasa Benard ni rafiki wa mtoto wangu, Mawazo. Akili zao kama sawasawa. Mimi nilikuona siku moja tu pale Kituo cha Polisi Urafiki wakati kaka yako na Mawazo walipowekwa ndani...”
“Kweli, nimekumbuka,” alisema Martha akiwa amemkumbuka mzee huyo ambaye umri ulikwenda sana...
“Haya! Mimi naishi nyumba ile ya tatu kutoka hapa. Hapa umefuata nini sasa?” aliuliza mzee huyo huku mkono wake mmoja ulioshika noti ya shilingi mia tano ukiwa umeshaingia kwenye dirisha la kuhudumiwa dukani hapo...
“Nina shida na kaka mmoja anaishi nyumba hiyo yenye geti jekundu,” alisema Martha huku macho yake yakielekea kwenye nyumba ya Roi...
“Nani, Ismaili?” aliuliza mzee huyo.
“Kwani anaitwa Ismaili?”
“Ee... ndiyo jina lake,” alisisitiza mzee huyo huku na yeye macho yake yakitua kwenye geti la nyumba hiyo.
Martha na muuza duka wote wakabaki wametumbua macho...
“Au wewe unamsema mwingine?” aliuliza Martha...
“Jamani! Kwani kwenye nyumba hiyo kunaishi watu wangapi? Si mmoja tu, kijana kijana hivi...mweupe, ana gari lina rangi ya kijiko cha chai ‘silva’.”
“Ee...” alikubali Martha...
“Ndiyo, anaitwa Ismaili. We alikwambia anaitwaje?”
“Mimi namjua kwa jina la Roi...”
“Mh! Roi tangu lini? Yule anaitwa Ismail Twalib Mussa.”
“Mimi namjua kwa jina la Evander,” alidakia kijana muuza duka.
“Hakuna bwana. Anaitwa Ismail.”
Mara, gari jeusi lilifika na kupaki getini kwa Roi, wakashuka wanaume wawili, wakiwa wamevaa suti nyeusi. Wakatembea kuelekea pale dukani. Wakasalimia wote kisha mmoja wao akauliza...
“Jamani tuna shida na Edo...anaishi kwenye nyumba hii,” alisema akionesha kidole nyumba ya Roi...
“Sisi hatujamwona...kwenye simu vipi?” alidakia mzee huyo...
“Simu yake inaita tu hapokei,” alisema mmoja wa wanaume hao huku wakirudi ndani ya gari na kuondoka zao...
“Sasa hawa jamaa wanasema anaitwa Edo...mimi najua anaitwa Ismaili...wewe unasema unamjua kwa jina la Roi...huyu muuza duka anasema anaitwa Evender. Huyu kijana si kawaida,” alisema mzee huyo akionekana kushangaa, akamwangalia Martha...
“Kwani wewe binti, unamfahamu kivipi?” mzee huyo alimuuliza Martha huku akimshika mkono na kwenda naye kando...
“Mimi ni jamaa yangu babu...”
“Jamaa yako?”
“Ndiyo babu, kwani vipi?”
“Ha! Sasa mbona watu mtaani pote hapa wanajua ni kijana mwathirika.”
“Mwathirika?” aliuliza kwa sauti Martha, macho yakapoteza uwezo wa kuona, akaanguka chini.
***
Kule chumbani, sasa Roi alikuwa akikaribia ushindi wa pili na alishatangaza nia. Mama Anna alikuwa amemkaribisha kwa shangwe huku akimuuliza anataka kumhamishia sehemu gani katika Jiji la Dar es Salaam...
“Si...sinza ku...na kufaa...”
“Sawa, tena Kwaremi...Kwaremi ndiyo kwenyewe,” alisema mama Anna huku mikono yake yote ikiwa mgongoni mwa Roi akimpa joto ambapo mlio wa geti kubwa la nje kugogwa ulisikika kwa nguvu...
“Mungu wangu, atakuwa nani amejitoa ufahamu mpaka kuamua kugonga geti langu?” alijihoji Roi akiwa anatafuta namna ya kutoka kwa mama Anna.
Itaendelea
 
SEHEMU YA 23


ILIPOISHIA:
“Mungu wangu, atakuwa nani amejitoa ufahamu mpaka kuamua kugonga geti langu?” alijihoji Roi akiwa anatafuta namna ya kutoka kwa mama Anna.
JIACHIE MWENYEWE SASA...
Roi alijitoa, akavaa bukta na kwenda sebuleni. Lakini akili ikamwambia kwamba amalizane na mama Anna kwanza, atoke kisha yeye amfungulie Martha wayaongee na kuyamaliza...
“Atanielewa tu,” alisema moyoni Roi.
Alirudi chumbani, kweli alimalizana na mama Anna na akamtoa huku mwanamke huyo akiamini kwamba, Roi hatamudu kukutana kimwili tena na Martha labda mpaka waende kwake au kama watalala hapohapo, basi usiku sana.
Wakati Roi anamtoa mama Anna, alimuahidi kwamba, atampa pesa kwa ajili ya kupanga chumba Sinza kama walivyokubaliana.
“Poa baby,” alikubali mama Anna akiwa anatoka geti la uani ambalo lipo ubavuni mwa nyumba hiyo na kutokomea upande wa pili kwa nyuma.
Roi alirudi chumbani na kumpigia simu Martha.
Martha akiwa bado dukani baada ya kugonga sana geti, alishangaa kuona simu ya Roi, akaipokea haraka sana huku akisema moyoni...
“Utadhani alikufa sasa amefufuka. Ngoja nimsikilize. Si ajabu anajua mimi nipo nyumbani, hajui kama nipo getini kwake...”
“Haloo...”alipokea Martha...
“Ee, nilikuwa sebuleni, simu ilikuwa kwenye chaja chumbani. Si unajua sijabeba chaja kuja nayo huko...”
“Roi,” aliita Martha...
“Sema...”
“Una uhakika upo sebuleni?”
“Kha! Sasa nipo wapi kama si sebuleni? Au wewe upo sebuleni kwangu?”
“Mimi nipo nje kwako hapa. Na nimeambiwa mengi sana kuhusu wewe.”
“Mengi kama?”
“Wewe unajijua. Unajua uko wapi na nani! Kama kweli upo sebuleni toka unifungulie geti.”
“Poa,” alijibu Roi na kukata simu huku moyoni akisema...
“Haya ndiyo mambo nisiyoyataka. Anaanzaje kunikontroo wakati anajua mimi si mume wake?”
Martha, alikwenda getini na kupiga kambi hapo akisubiri kufunguliwa. Yeye alijua Roi hawezi kufungua na kama atafungua kweli basi atakuwa ameongozana na mama Anna.
Alishangaa geti limefunguliwa, Roi akiwa ndani ya bukta tu, tena akionesha hana wasiwasi wowote ule...
“Unajua nikiwa hapa nyumbani sipendagi kuacha geti wazi. Si unajua naishi mwenyewe?” alisema Roi akimbusu Martha ambaye alikuwa mbali sana kimawazo...
“Ina maana maneno ya muuza duka si ya kweli?” alijiuliza Martha akiwa hajui akubali au akatae.
Walizama mpaka sebuleni, Roi akakaa hapo kisha akamwambia Martha kama amefika kufanya usafi, aanze na chumbani.
Martha alisimama, akaenda chumbani. Lakini akashika mlango wa chumba cha kwanza, akaufungua, hakuona mtu, akashika mlango wa chumba cha pili, hakuona mtu, akaenda jikoni, hola. Akaenda stoo, hakuna kitu, akaenda chooni na bafuni hakukuwa na dalili ya kuwepo mtu...
“Mh! Basi yule kijana ni mwongo mkubwa. Afadhali hata ningemwona mwanamke, hata kama si mama Anna kuliko kutokuwa na mtu yeyote yule,” alisema moyoni Martha akiingia chumbani.
Sebuleni, Roi alikuwa kwenye kompyuta mpakato akibofyabofya huku akijivunia ushindi wake kwa mama Anna.
Martha alifanya usafi sehemu mbalimbali za nyumba hiyo hadi akafika sebuleni, kisha uani.
Alipofika uani, kwa mara ya kwanza alibaini kuwepo kwa mlango mdogo ambao mtu anaweza kutoka nje. Lakini ulikuwa umetiwa kufuli...
“Aa...aaaaa! mama Anna alikuwepo, ametokea mlango huu. Sasa nimejua,” alisema moyoni Martha huku hasira za wivu zikimpanda kama mwanamke.
Ili aujue ukweli alimfuata Roi sebuleni na kumwambia ampe funguo za mlango huo ili akatupe taka nje...
Kwa kujikaza sana, Martha alisema...
“Baby, naomba funguo za mlango wa uani. Nataka kutupa takataka.”
Roi naye alijua kimenuka au kitanuka, kwamba Martha atajua nini kiliendelea...
“Ooh! Baby, ule mlango tangu nimehamia nyumba hii haujawahi kufunguliwa na wala sijawahi kuona funguo yake. Pia kwa sababu ni uchochoroni sijawahi kutaka kuufungua,” alisema Roi kwa macho makavu kabisa.
Martha alikubaliana na utetezi wa Roi, moyo wake ukarejea katika hali yake ya kawaida.
***
Mama Anna alipotoka hapo, moja kwa moja alikwenda nyumbani na kuwasimulia wale mashoga zake, wapangaji wenzake kilichojiri nyumbani kwa Roi. Walicheka sana na kumshauri...
“Wewe usiwe mjinga. Pesa za kupanga za nini? Usipokee. Unachotakiwa kufanya wewe ni kung’ang’ania kuishi kule kwake. Mwambie wewe utakuwa unaishi kule yeye na Martha waishi hapa. Kwa hiyo akitoka kazini anakufuata kule. Mnajirusha halafu midamida anakuja huku,” alisema mmoja wa wanawake hao.
Mama Anna alikubaliana na ushauri huo kwani kwake aliuona kama ni wa kuweza kumfikuisha kwenye ndoa kabisa na kumpiku Martha.
***
Martha na Roi waliwasili nyumbani hapo, usiku wa saa tatu. Waliwakuta wapangaji wapo nje bado wakipiga domo licha ya kibaridi cha mbali.
Macho ya Martha yalitua kwenye sura ya mama Anna, akakasirika kwa mbali. Kilichomshtua zaidi Martha na gauni alilovaa mama Anna muda huo ndiyo lilelile ambalo aliambiwa na muuza duka kwamba, mwanamke aliyeingia na Roi ndani alikuwa amevaa...
“Inawezekana kweli mama Anna alikuwa amekwenda kula kwa Roi lakini labda hakukaa sana akatoka ila yule kijana wa dukani hakumwona ndiyo maana alijua bado yupo,” alisema moyoni Martha...
“Jamani za leo?” alisalimia Roi akiwa nyuma ya Martha wakiingia ndani...
“Nzuri tu za kwako shemeji?”
“Salama za kazi shemeji?”
“Salama za kazi honey,” alijibu mama Anna kwa sauti ya chini...
Je, nini kilitokea?
 
SEHEMU YA 24

ILIPOISHIA:“Wewe usiwe mjinga. Pesa za kupanga za nini? Usipokee. Unachotakiwa kufanya wewe ni kung’ang’ania kuishi kule kwake. Mwambie wewe utakuwa unaishi kule yeye na Martha waishi hapa. Kwa hiyo akitoka kazini anakufuata kule. Mnajirusha halafu midamida anakuja huku,” alisema mmoja wa wanawake hao.
SASA ENDELEA MWENYEWE...
Mama Anna alikubaliana na ushauri huo kwani kwake aliuona kama ni wa kuweza kumfikisha kwenye ndoa kabisa na kumpiku Martha.
***
Martha na Roi waliwasili nyumbani hapo, usiku wa saa tatu. Waliwakuta wapangaji wapo nje bado wakipiga domo licha ya kibaridi cha mbali.
Macho ya Martha yalitua kwenye sura ya mama Anna, akakasirika kwa mbali. Kilichomshtua zaidi Martha ni gauni alilovaa mama Anna muda huo ndiyo lilelile ambalo aliambiwa na muuza duka kwamba, mwanamke aliyeingia na Roi ndani alikuwa amevaa...
“Inawezekana kweli mama Anna alikuwa amekwenda kule kwa Roi lakini labda hakukaa sana akatoka ila yule kijana wa dukani hakumwona ndiyo maana alijua bado yupo,” alisema moyoni Martha...
“Jamani za leo?” alisalimia Roi akiwa nyuma ya Martha wakiingia ndani...
“Nzuri tu za kwako shemeji?”
“Salama za kazi shemeji?”
“Salama za kazi honey?” alijibu mama Anna kwa sauti ya chini kiasi kwamba, Martha alijua amezungumza kitu kwa sauti ya chini ambayo hakuisikia hali iliyompa dukuduku kubwa sana...
“Baby,” Martha alimuita Roi wakiwa wameshazama ndani kwao...
“Yes! Niambie...”
“Mimi nahisi huyu mwanamke huyu...mama Anna ana jambo na wewe lakini sijalijua. Ila nalifanyia kazi.”
“Jambo kama lipi?”
“Kuna jambo. Mfano, hapo wakati tunaingia wenzake wamekusalimia. Hata yeye amekusalimia, lakini kuna maneno f’lani ameyasema naamini siyo salamu na ameyasema kwa sauti ya chini sana.”
“Mh! Mimi sijui kwa kweli. Labda ana mambo yake mwenyewe,” alijibu Roi huku moyoni akiujua ukweli.
***
Ilikuwa saa nne usiku, Martha akiwa anapiga pasi sebuleni, Roi yuko chumbani. Nje, usawa wa dirisha la sebuleni kwa Martha, alikaa mama Anna peke yake. Alikuwa akichati na Roi kule chumbani.
Alichokishangaa Martha, simu ya Roi ilipotoa mlio wa meseji, baada ya dakika kadhaa, simu ya mama Anna kule nje nayo ilitoa mlio wa meseji.
Martha alishtuka, hasa baada ya kubaini kuwa, milio hiyo ya meseji ilikuwa ikipokezana kusikika. Kwamba, unapolia wa simu ya Roi, baada ya muda unadakia wa simu ya mama Anna...
“Mh!” aliguna Martha, akaacha kupiga pasi, akasimama kusikilizia kwa umakini zaidi...
“Titiri...titiri...” huo ulikuwa mlio wa simu ya Roi...
“Titiiiti...” huo ulikuwa mlio wa simu ya mama Anna.
Martha aliingia chumbani, akampiga jicho moja Roi, akamwona akiweka simu juu ya dressing table...
“Baby, nataka kumpigia simu bro, lakini kumbe simu yangu sijaweka salio, niazime ya kwako nimpigie,” alisema Martha...
“Mh! Hata yangu haina salio, chukua elfu mbili hii ukanunue vocha,” aliwahi kusema Roi, Martha akaanza kushtuka. Aliamini Roi alikuwa akichati na mama Anna nje.
Alikwenda dukani kununua vocha, wakati anarudi alisimama chini ya mti wenye giza na kumwangalia mama Anna anavyoongea na simu huku akicheka...
“Teh! Teh! Mimi ni mashine baby...tena nakwambiaje? Siku akijua naamini patachimbika. Lakini mimi wala simuogopi,” alisema mama Anna huku akicheka.
Akaendelea...
“Duu! Baby, mfano pale kwako. Mimi miguu yote ilinyong’onyea, nikajua tumekwisha! Loo!”
Martha alipojitokeza, mama Anna alishtuka, akapunguza sauti huku akisema...
“Basi tufanye kesho baby wangu, usiku mwema.”
Martha alipita bila kusema kitu kwa mama Anna, akazama ndani na kumpa Roi vocha ya buku, akabaki na ya buku kuingiza kwenye simu yake.
***
Ilikuwa saa saba usiku, Martha alichelewa kupata usingizi kwa mawazo kuhusu kutaka uhakika wa kuwepo kwa mawasiliano kati ya mama Anna na jamaa yake, Roi...
“Hivi kama ni kweli nichukue hatua gani?” alijiuliza moyoni Martha...
“Na yale mazungumzo ya kwenye simu ya mama Anna muda ule mbona ni kama alikuwa akiwasiliana na Roi?”
Ghafla alipata wazo, alitoka kitandani huku macho yake yakitua kwa Roi. Alipobaini anauchapa usingizi mzito, aliifuata simu yake, akaichukua na kwenda nayo sebuleni.
Aliikuta simu hiyo haina ‘password’ kwa hiyo akaingia ndani moja kwa moja kwenye kiboksi cha meseji...
“Baby, unajua wakati tunaongea ghafla akatokea demu wako, ndiyo maana nikakuaga.”
Meseji hiyo ilitoka kwa mama Anna kwenda kwa Roi. Martha aliishiwa nguvu, nusura aanguke. Akaendelea kusoma nyingine...
“Basi usiku mwema baby. Nimekumisije jamani!”
Roi naye akajibu...
“Mimi je? Natamani kesho ifike haraka tukutane unikate kiu yangu. Lala salama mpenzi wangu nikupendaye.”
Martha alisimama, akamwomba Mungu kwanza kisha akajipa moyo na ujasiri wa hali ya juu. Akatuma meseji kwa mama Anna...
“Baby...”
Ingawa ilikuwa usiku sana, Martha akaamini atajibiwa, lakini hakujibiwa, akatuma nyingine...
“Jamani baby, naomba nije kwako basi, nimekumisi kweli mwenzio.”
Dakika zilikatika, hakupata jibu. Akazifuta meseji zake hizo mbili na kuamua kurudi chumbani kulala. Alitamani sana kumwamsha Roi ili ambane kuhusu meseji hizo lakini akajivumilia. Aliirudisha simu mahali alipoichukua na kulala.
***
Kulikucha, Martha aliamka na kuanza kufanya kazi za ndani lakini siku hiyo hakumwamsha Roi mpaka alipoamka mwenyewe.
Roi, kabla hajatoka kitandani, aliichukua simu na kuangalia meseji, akakutana na meseji ya mama Anna ikiomba radhi...
“Baby samahani, ulipotuma meseji usiku nilikuwa nimelala fofofo mwenzako. Halafu uliposema umenimisi unataka kuja ulikuwa unamaanisha au utani tu? Bibiye ungemwachaje kitandani peke yake?”
Je, nini kilitokea?
 
SEHEMU YA 25

ILIPOISHIA :
“Baby samahani, ulipotuma meseji usiku nilikuwa nimelala fofofo mwenzako. Halafu uliposema umenimisi unataka kuja ulikuwa unamaanisha au utani tu? Bibiye ungemwachaje kitandani peke yake?”
SASA JIACHIE MWENYEWE…
Roi alishtuka sana. Akaangalia kama alituma meseji amesahau, hakuona meseji yoyote. Akahisi huenda meseji hiyo ya mama Anna ilimfikia yeye kwa bahati mbaya tu, akamuuliza…
“Sweet, meseji hii ya nani?”
Akajibiwa…
“Ya nani kwani darling. We unadhani inaweza kuwa ya nani zaidi yako jamani? Au unanituhumu kwamba nina mchepuko?”
“Mh!” Roi aliguna kwanza. Akakaa kitandani na kufikicha macho. Bado aliamini mama Anna anajitetea tu…
“Mimi nilikutumia meseji wewe ya kukutaka nije kwako?”
“Ndiyo. Kwani si imekuja kwa namba yako baby! Acha hizo bwana.”
Roi alitoka kitandani, akasimama na kujishika kichwa. Mapigo ya moyo yakamwenda kwa kasi ya ajabu.
Aliizima simu, akaenda kuoga. Aliporudi alivaa kisha akamuaga Martha kwamba anaondoka…
“Baadaye baby.”
“Poa sweetheart,” Martha alimjibu kama hakuna lolote jambo ambalo lilizidi kumchanganya Roi.
Hatua kumi hazikufika baada ya kutoka na gari, Roi alimtumia meseji mama Anna akimtaka akae sehemu nzuri anataka kumpigia simu…
“Piga tu baby, niko chumbani bado nimelala. Kwani we umeshatoka kwenda kazini?”
Roi hakujibu meseji ya kuulizwa kama ameshatoka kwenda kazini. Alichofanya yeye alimvutia uzi moja kwa moja…
“Yes baby, niambie,” alipokea mama Anna kwa sauti iliyojaa kudeka kimahaba…
“Hivi ulichosema ni kweli au utani?” aliuliza Roi…
“Kwamba?”
“Kwamba nilikutumia meseji ya kutaka nije kwako?”
“Khaa! Jamani! Sasa …kwanza nikuulize baby, kwani jana ulilewa?”
“Sikulewa. Hata wewe unajua sikulewa.”
“Sasa kwa nini usijue kama ulinitumia meseji mimi mke wako?”
“Sijatuma meseji ya hivyo kwako. Imeingia saa ngapi?”
“Mh! Hujatuma? Ilikuwa usiku kama saa saba hivi.”
“Kweli?”
“Kweli baby.”
“Meseji ngapi?”
“Mbili.”
“Zilisemaje?”
“Ya kwanza uliita baby…ya pili ukasema jamani baby, naomba nije kwako basi, nimekumisi kweli mwenzio.”
Roi alikosa nguvu, kidogo aiingize gari kwenye mtaro. Ni Mungu tu alimsaidia…
“Mimi siamini mpaka nizione hizo meseji kama kweli zimetoka kwenye namba yangu ya simu.”
“Ina maana huamini?”
“Siamini.”
“Nije ofisini kwako muda huu?”
“Itakuwa vizuri aisee. Njoo,” alisema Roi.
Roi alimwelekeza mama Anna ofisini kwake akimsisitizia kwamba aende na Bajaj, yeye atalipa.
***
Mama Anna naye alianza kuingiwa na wasiwasi. Alijua kama Roi hakutuma meseji zile basi aliyetuma ni Martha. Alitungua taulo, akavaa, akatoka kwenda uani kwa sababu mbili. Kwanza akamwone Martha anafananaje! Sura yake inasema kwamba kuna donge moyoni au kawaida. Pia, akaoge tayari kwa kwenda mjini kazini kwa Roi.
Hakumwona Martha zaidi ya wale wapangaji wenzake wawili…
“Jamani kimenuka,” alisema Martha.
“Ki nini?”
“Martha alichukua simu ya jamaa yake usiku akanitumia meseji mimi.”
Wale walishtuka sana…
“Kwa hiyo wewe ukajibu nini?”
“Sikujibu, nilikuwa nimelala.”
“Loo! Sasa?”
“Hata sijui, naoga nakwenda kazini kwake muda huuhuu.”
Mama Anna mpaka anaondoka, hakuonana na Martha. Alifuata maelekezo mpaka akafika ofisini kwa Roi.
Kitu cha kwanza, Roi aliomba simu ya mama Anna na kuangalia meseji. Kweli zilitoka kwenye simu yake…
“Daa! Hatari. Hizi alituma Martha kweli. Na kama alituma yeye ina maana kwamba aliziona meseji zote za awali ambazo mimi nilikutumia,” alisema Roi akiwa tayari na macho mekundu.
“Sasa itakuaje?” alihoji mama Anna…
“Hamna jinsi.”
“Jinsi ipo.”
“Ipi?”
“Akikuuliza mwambie mimi ni dada yako.”
“Ah! Kwa zile meseji halafu niseme wewe ni dada yangu, inakuja kweli?”
“Inakuja. Huna utetezi mwingine kwa siku ya leo. Lakini pia si ulisema unataka kumwacha Martha uwe na mimi tu, yameishia wapi mpaka unakuwa mwoga?” aliuliza mama Anna kwa sauti iliyojaa ujasiri wa hali ya juu.
“Ni kweli, lakini si katika mtindo wa kukuta meseji zako kwenye simu yangu. Nilitaka iwe amani tu.”
“Ameshakuta sasa, itakuaje?”
“Hata sijui.”
“Ndiyo ujue sasa. Mimi nakushauri jambo moja mpenzi wangu.”
“Lipi hilo baby?”
“Mimi na Martha wajina wangu, nani unampenda zaidi?”
“Martha wewe.”
“Basi mtumie meseji kwamba umeamua kuwa na mimi, hivyo jioni utakwenda kuchukua nguo zako tu.”
“Mh! Atakuibulia ugomvi wewe.”
“Mimi nipo tayari.”
Wakati wakizungumza hayo, mara Martha akaingia…
Je, nini kilitokea?
 
SEHEMU YA 26

ILIPOISHIA :“Mimi na Martha wajina wangu, nani unampenda zaidi?”
“Martha wewe.”
“Basi mtumie meseji kwamba umeamua kuwa na mimi, hivyo jioni utakwenda kuchukua nguo zako tu.”
“Mh! Atakuibulia ugomvi wewe.”
“Mimi nipo tayari.”
Wakati wakizungumza hayo, mara Martha akaingia...
SASA TAMBAA NAYO MWENYEWE...
“Anhaaa! Mungu kweli mkubwa. Leo nimeamini. Kumbe hii ndiyo biashara yenu siyo?” aliuliza Martha kwa sauti yenye kujiamini...
“Hebu kaa kwanza hapo,” alisema Roi huku akitetemeka. Mama Anna alitetemeka lakini si sana.
Martha alivuta kiti, akakaa na kusema...
“Unasemaje wewe mwanaume mwenye majina mengi. Maana nimesikia una majina kama matatu hivi wewe peke yako. Kila mtu mtaani anakufahamu kwa jina lake.”
Roi alishtuka kusikia hivyo. Kwani ni kweli mtaani ana majina mengi...
“Mh!” aliguna Roi huku akimtumbulia macho ya aibu Martha. Lakini hakujibu hoja ya kuwa na majina mengi.
“Sikia nikwambie baby wangu Martha. Huyu si mpenzi wangu, ni sista‘angu ila sijawahi kukwambia,” alianza kusema Roi...
“Mimi dada yako mimi?” mama Anna alikuja juu kumuuliza Roi...
“Aaa! Jamani dada Martha...looo! yaani unanikataa kaka yako hivihivi naona jamani?”
“We wajina...sikia, mimi si dada yake wala yeye si kaka yangu. Mipango yetu ni kufunga ndoa. Huyu si wa kumtegemea wewe kwani mapenzi yake ameyahamishia kwangu...we ulie tu,” alisema mama Anna kwa macho yaliyokosa aibu.
Martha alidondoka palepale, akapoteza fahamu, hali ikawa tete. Roi huku akiogopa, alimtupia lawama mama Anna...
“Unaona sasa? Kwani kulikuwa na ulazima gani wa kumwambia wewe. Si ningemwambia mimi mwenyewe...
“Na haikuwa lazima kumwambia sasa hivi, hata nyumbani ningemwambia...”
“Baby, mimi tatizo langu sipendi kukatishakatisha. Niko moja kwa moja sana. Nisamehe kwa hilo. Ndiyo maana nilikuuliza awali unampenda nani. Mtu akifiwa hakuna haja ya kufichaficha, ni kumwambia tu ili kama kulia alie,” alisema mama Anna.
Roi na mama Anna walimzoa Martha na kumkimbiza hospitali ambako alilazwa. Mama Anna aliwapa taarifa wale wapangaji wengine kuhusu kuugua ghafla kwa mwenzao huyo.
***
Ilikuwa saa kumi na mbili jioni, Martha alikuwa kwake baada ya kutoka hospitali. Wapangaji wenzake waliingia kumpa pole kasoro mama Anna tu ambaye muda huo alikuwa nyumbani kwa Roi...
“Pole mwaya! Yaani tuliposikia umelazwa tukashangaa sana. Da! Sasa tatizo lilikuwa wapi Martha?” mpangaji mmoja alimuuliza...
“Jamani ni hadithi ndefu sana. lakini kifupi nilikuwa sijui kama jamaa yangu anatoka na mama Anna. Nilihisi wakati f’lani nikafuatilia, jana usiku nikanasa meseji zao za mahaba.
“Leo asubuhi nikasema niende kazini kwake kufika namkuta mama Anna ndani. Yeye jamaa yangu akasema mama ni dada yake, japo nilijua ni uongo, lakini mama Anna mwenyewe akanipasulia kwamba wao si ndugu bali ni wachumba na wanatarajia kufunga ndoa hivi karibuni,” alitiririka Martha...
***
Kule nyumbani kwa Roi, mama Anna alimtaka Roi amruhusu awaite wale wapangaji wenzake wawili ili awatambulishe rasmi kwake...
“Aaaa...eeee...oke, waite basi,” alisema Roi ambapo awali alianza kwa kutaka kukataa.
“Mbona baby kama unasita? Au mipango yetu imekufa nini?” aliuliza mama Anna...
“Aaa! Noo...iko palepale. Basi waite.”
Mama Anna alimpigia simu mmoja wa wapangaji wenzake, akampa maelekezo ya namna ya kufika hapo.
Wakati wanaondoka, wakamuaga Martha...
“Basi twendeni wote na mimi nataka kupeleka nguo za Roi.”
Wale ilibidi wamjulishe mama Anna kwanza ambapo naye alikubali bila kumuuliza Roi...
“Aje tu, hakikisheni amebeba hizo nguo za Roi ili asije kupata kisingizio kingine baadaye,” alisema mama Anna.
Wakati anazungumza hivyo, Roi ndiyo akasikia na kuhoji ni nini, mama Anna akamwambia, Roi akatingisha kichwa tu kukubaliana naye.
Kutoka moyoni mwake, Martha alishakubaliana na hali iliyotokea, akajilaumu sana kwa uamuzi wake wa kung’ang’ania yeye na Roi wasiwe kaka na dada na badala yake wawe wapenzi...
“Ningeusikiliza moyo siku zile haya maumivu yalikuwa yanakwepeka,” alisema moyoni wakiwa wanakaribia nyumbani kwa Roi yeye akiwa kiongozi maana alishafika.
Waliingia ndani watatu, wale wapangaji wawili na Martha.
Mama Anna aliwakaribisha kwa mbwembwe akijifanya mama mwenye nyumba huku Roi akionekana kukosa amani...
Karibuni jamani...karibuni sana,” alikaribisha mama Anna kwa sauti ya ‘mimi ndiye mmiliki halali wa mwanaume huyu’, yaani Roi sasa.
“Tunashukuru sana,” waliitikia wale wapangaji wawili kasoro Martha ambaye yeye alifikia kuweka begi chini kisha akamwambia Roi...
“Ungeangalia kama nguo zako zote zipo maana nimehakikisha siachi nguo yako hata moja.”
“Naamini zote zipo bila hata ya kuhakikisha,” alisema Roi kwa sauti iliyojaa dharau, mkono mmoja ulipita kiunoni kwa mama Anna huku mkono mwingine ukishughulika na rimoti ya televisheni.
Bila kukaa, Martha akageuza kutoka lakini kabla hajafika mlangoni, ikasikika hodi...
“Hodi,” hodi hiyo ilipigwa huku aliyepiga akisukuma mlango kuingia sebuleni.
Roi alishtuka sana, akatumbua macho huku akisimama na kusema...
“Mama Neema...mbona umekuja bila taarifa mke wangu? Umeona sasa umenikuta katika mazingira tata. Lakini kifupi hapa hakuna mwanamke wangu mama Neema.”
Je, nini kilitokea?
 
SEHEMU YA 27

Kauli ya Roi ilimshtua sana mama Anna, Martha mwenyewe na wale wapangaji wawili…
“Ha! Mpenzi wangu, kumbe wewe una mke?” aliuliza mama Anna kwa sauti yenye mshtuko…
“Wewe. Mimi ni mpenzi wako tangu lini? Acha uzushi? Eti Martha, huyu mama Anna ni mpenzi wangu?” Roi aliomba huruma ya Martha ili kuokoa ndoa yake.
Mama Neema ni mke wa Roi. Alikwenda masomoni Uingereza kwa mwaka mmoja na muda huo ndiyo alikuwa amerudi rasmi. Neema alipelekwa kusoma kwa babu yake.
“Mi mwenyewe nimeshangaa. Kwani we mama Anna, Roi ni mpenzi wako?” aliuliza Martha huku akianza kujisikia furaha kwa anguko la mwanamke huyo aliyempindua yeye.
Mama Neema alifika kukaa kwenye kochi kubwa huku akimshangaa mume wake na ugeni ule. Alitaka kujua…
“Baba Neema hawa wote ni akina nani na wamefuata nini hapa nyumbani?”
“Mama Neema wewe ndiyo kwanza umefika. Ungetulia kwanza basi. Umekuja na begi hilo moja tu?”
“Nina mizigo mingi ipo kwenye gari nje,” alijibu mama Neema kwa sauti iliyojaa hasira.
Roi alisimama na kutoka nje. Alishusha shehena ya mizigo huku moyo ukiwa kasi. Alijua kimenuka…
“Eti nyie ni akina nani?” mama Neema aliwauliza kwa mpigo huku akimwangalia mmoja mmoja.
“Mimi naitwa Martha. Ni rafiki wa Roi,” alisema Martha huku akiogopa. Mama Neema akamwangalia mama Anna kama anayesema ‘na wewe?’
“Mimi naitwa mama Anna. Roi nii…niii…mimi sikujua kama Roi ana mke.”
“Nimekuuliza wewe nani, siyo Roi ana mke au hana,” alikuja juu mama Neema huku akionekana kutaka kusimama kumfuata mama Anna…
“Mimi pia ni rafiki yake wa karibu tu,” alijibu haraka mama Anna.
Wale wapangaji wengine walijitambulisha kwa haraka huku wakisimama kutaka kuondoka. Mizigo iliingia ndani, Roi alisaidiwa na vijana wa mtaani.
Mama Neema aliwazuia wote kutoka mpaka Roi arudi na kuzungumza naye kuhusu wao. Walikaa kinyonge.
Baada ya utulivu, Roi alirejea na kukaa…
“Baba Neema naomba utambulisho wa hawa watu wote humu ndani,” alisema mama Neema kwa sauti yenye hasira…
“Wote ni marafiki zangu. Wametoka kumoja na wataondoka pamoja.”
“Kwa nini huyu alikaa jirani na wewe kiasi kile?”
“Nani, huyu? Huyu aliamua tu.”
“Lakini mwenyewe si alisema we ni mpenzi wake?” alihoji mama Neema.
Roi alitulia akiashiria hana cha kujibu…
“Nyie malaya, nawaomba muondoke sasa hivi la sivyo nitampiga mtu risasi,” alisema mama Neema.
Akina Martha walitoka mbio, mlangoni waliminyana kila mmoja akitaka kuwa wa kwanza kutoka nje.
Wakiwa nje ya geti kuu, mama Anna alimuomba msamaha Martha…
“Martha ndugu yangu. Mi naomba nisamehe sana. Ni kweli nilikuingilia kwenye penzi lako. Sikujua kama Roi yuko vile. Nisamehe sana ndugu yangu. Nimejifunza kwamba, kila binadamu na riziki yake. Roi alikuwa riziki yako. Mimi nikaingilia kati,” alisema mama Anna huku akimwangalia Martha…
“Mh! Yaani wewe unamwomba samahani mwenzako kwa sababu kule kumeharibika siyo? Kwa nini usingemwomba sahamani jana au juzi?” mmoja wa wale wapangaji aliingilia kati…
“Eti!” mwenzake alidakia.
Walimnanga mama Anna kama si wao waliokuwa wakimuunga mkono na kumficha Martha kwamba wanajua.
“Sikiliza mama Anna. Kwanza sipokei msamaha wako. Pili, uache unafiki wako. Kilichokufanya uniombe msamaha ni baada ya kujua Roi kumbe ana mke. Usingejua je? Yaani we mwanamke mimi nimekushangaa sana. Umekuwa ukinila hivihivi najiona,” alisema kwa ukali Martha…
“Siyo hivyo Martha. Jamani msinielewe vibaya. Mambo mengine yanafanyika ili mtu ujifunze. Naamini hata kilichotokea nyumbani kwa Roi kimekuwa cha makusudi ili mimi nijifunze. Please nisamehe sana Martha,” alisema mama Anna kwa sauti ya unyonge huku akimtangulia mbele na kuonesha ishara ya kutaka kupiga magoti huku akifunga mikono…
“Oke, sawa. Sasa niambie ukweli…”
“Niko tayari Martha,” alisema mama Anna…
“Wewe na Roi mmeanzia wapi na lini mpaka mkawa wapenzi?”
Japokuwa mama Anna alikuwa tayari kujibu maswali kama alivyosema mwenyewe, lakini swali hilo lilikuwa gumu sana kwake. Ikabidi adanganye…
“Sikia Martha. Mimi na Roi tunajuana zamani sana. Tena sana. Kwa hiyo alipokuja kwako ikawa kama tunakumbushia tu,” alisema mama Anna…
“Muongo huyu Martha. Alichukua namba za simu palepale nyumbani. Siku ile wakati shemeji anatoka kuoga ndiyo akachukua, wakaanza mawasiliano. Na alisema nia yake mpaka akupindue,” alisema mmoja wa wale wapangaji.
“Sawa jamani. Martha ni kweli walichosema hawa. Mimi nilijua nikikwambia hivyo utazidi kuumia wakati mtu mwenyewe haunaye tena. Nisamehe sana.”
Martha aliamua kumsamehe mama Anna huku akimwonya kutorudia tabia hiyo kwa watu wengine kwani si njema…
“Yaani kama utakuja kumfanyia hivi mtu mwingine yeyote yule, ujue maisha yako yatakuwa mabaya sana mama Anna. Nakwambia mimi,” alisema Martha.
Wale wapangaji wengine pia wakamzodoa mama Anna na kumwambia ana tabia mbaya. Hata wao wamejifunza kuwa naye mbali. Hata hivyo, mama Anna aliahidi kubadilika kanzia siku hiyo.
MWISHO.
SIMULIZI TAMU NYINGINE ZINAKUJA
 
Back
Top Bottom