Chinua Achebe akataa kupokea tunzo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chinua Achebe akataa kupokea tunzo!

Discussion in 'International Forum' started by Yericko Nyerere, Nov 14, 2011.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,210
  Likes Received: 3,774
  Trophy Points: 280
  Hii ni mara yake ya pili kufanya hivyo akisema matatizo yale yale yaliomfanya asikubali tuzo hiyo miaka saba iliyopita bado yamesalia.

  Chinua Achebe ni mojawapo wa magwiji wa Afrika katika utunzi wa hadithi na riwaya ambaye sifa zake zimeenea duniani kote.Kwa hiyo matamshi yake yana uzito mkubwa. Alipokataa tuzo kuu ya heshima ya kamanda wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria mnamo mwaka 2004 alilalamika kwamba nchi yake inageuzwa kuwa himaya iliyozama katika ufisadi na vurugu.

  Akiikataa kwa mara ya pili tuzo hiyo alisema matatizo yale yale bado yapo hayajashughulikiwa seuze kusuluhishwa. Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameelezea mshangao na masikitiko yake kwa uamuzi huo. Rais huyo amesema anatumai kwamba Bwana Achebe atapata fursa ya kuizuru Nigeria kutoka Marekani anakoishi na kuona jinsi serikali ya Nigeria inavyozidi kupiga hatua.
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,067
  Trophy Points: 280
  Prof Kabudi yeye anasaliti na kukubari kuwa mtumwa...watu waliosoma kwa pesa za mchicha leo wanatugeuka,ndo wasomi wetu hao
   
 3. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #3
  Nov 14, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapa Tz hatuna wasomi wenye moyo huo wao ni kujipendekeza tu kwa viongozi hata ikitokea hao viongozi wameharibu kama hawa tulionao serikalini ni aibu tupu
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Nov 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,278
  Likes Received: 19,430
  Trophy Points: 280
  kila siku wasomi wetu wanamtunuku KIKWETE udaktari ..haha si wanatumia nmasaburi badala ya kuweka maslahi ya taifa mbele
   
 5. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #5
  Nov 14, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  achebe.jpg
  [FONT=&amp]Mwandishi mashuhuri wa riwaya nchini Nigeria,Chinua Achebe amekataa kupokea mojawapo ya tuzo kubwa za heshima za Nigeria.[/FONT]
  [FONT=&amp]Hii ni mara yake ya pili kufanya hivyo akisema matatizo yale yale yaliomfanya asikubali tuzo hiyo miaka saba iliyopita bado yamesalia.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Chinua Achebe ni mojawapo wa magwiji wa Afrika katika utunzi wa hadithi na riwaya ambaye sifa zake zimeenea duniani kote.

  Kwa hiyo matamshi yake yana uzito mkubwa. Alipokataa tuzo kuu ya heshima ya kamanda wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria mnamo mwaka 2004 alilalamika kwamba nchi yake inageuzwa kuwa himaya iliyozama katika ufisadi na vurugu.
  [/FONT]
  [FONT=&amp]Akiikataa kwa mara ya pili tuzo hiyo alisema matatizo yale yale bado yapo hayajashughulikiwa seuze kusuluhishwa. Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameelezea mshangao na masikitiko yake kwa uamuzi huo. Rais huyo amesema anatumai kwamba Bwana Achebe atapata fursa ya kuizuru Nigeria kutoka Marekani anakoishi na kuona jinsi serikali ya Nigeria inavyozidi kupiga hatua.
  source-bbcswahili
  [/FONT]
   
 6. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #6
  Nov 14, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Nigeria na Achebe wao, sisi na akina Kabudi wabwabwajaji, lol, kazi tunayo. Hivi ccm huwa inawanunua kwa shilingi ngapi hata wadhalilishe taaluma zao?
   
 7. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  kwa imani kubwa kabisa naamini marehemu Seth Chachage angeweza kufanya kama Achebe.
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Wanataaluma wasioongozwa na matumbo... mpaka raha yani!
   
 9. d

  doctorwasummary Member

  #9
  Nov 15, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chinua anafikiri katika utendaji wa kazi zake. Prof. Kabudi yeye anaambiwa na wanasiasa afanye nini ili apandishwe cheo au apewe chakula. hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya Chinua na wanaojiita wasomi wa Tanzania ambao hawezi kuishi nje ya mfumo uliooza kama wa Tanzania
   
 10. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Achebe my hero, things continue to fall apart in Africa
   
 11. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #11
  Dec 13, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika, rais Jakaya Kikwete aliwatunukia watu mbali mbali wakiwamo wanaofaa na wasiofaa nishani, nchini Nigeria gwiji wa fasihi Chinua Achebe amekataa nishani kama hiyo.

  Wakati kwetu watu wanahoji kwanini kwa mfano Spika wa bunge la sasa Anna Makinda amepewa nishani wakati hafai, nchini Nigeria mambo ni tofauti. Achebe alikataa nishani ya Commander of the Federal Republic award-nishani ya rais, kwa madai kuwa mhusika hajashughulikia mambo muhimu ambayo Achebe ameataka yatekelezwe ambayo ni kupambana na ufisadi, umaskini na vurugu havijashughulikiwa. Achebe alitoa changamoto mwaka 2004 alipokataa nishani kama hii. Je ni nani ana ubavu wa kukataa nishani Tanzania ambapo nishani, shahada za kupewa na kughushi, kujuana katika ulaji na udugu ni madhambi yaliyohalalishwa. Waulize waliotoa na waliopokea nishani kama kuna mwenye udhu na ubavu wa kuhoji kama Achebe. Je Kikwete aliyeingia madarakani kupitia wizi wa EPA na Richmond ana udhu wa kuweza kutoa nishani yenye kuweza kuitwa nishani na kuheshimika? Kama anao basi anaweza kutoa nishani si kwa maana ya nishani bali kituko.

  Kwa Achebe kitu muhimu si nishani bali matendo. Kwake rais mharifu ni mharifu sawa na kibaka. Tieni akilini na mtafakuri kwa kina. Je waliopewa nishani wamepewa nishani na mamlaka yenye udhu au wamepewa dharau na aibu? Inashangaza ni kwanini Rostam Aziz na Andrew Chenge hawakupewa nishani hizi zenye maana kinyume na tunavyoelezwa. Aibu ni kwamba marehemu Mwalimu Julius Nyerere amepewa nishani hii chafu na mikono michafu iliyoitoa! Kweli simba akifariki ngozi yake yaweza kugugunwa na panya. Imetokea tena Tanzania.
  Kwa habari zaidi BONYEZA HAPA
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Dec 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  malechela amesahau greda likimaliza kuchimba barabara ni marufuku kuikanyaga?
   
 13. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #13
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  ni lini Malecela amelilia hiyo nishani? au unataka kuvutia wasomaji? si vizuri kupakaziana
   
 14. D

  Dopas JF-Expert Member

  #14
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kati ya wote waliopewa nishani, Makinda lazima atakuwa aliikimbilia haraka kabla Rais hajabadili mawazo kwani anajua kuwa hakustahili kupewa, kwani hadi sasa alichoifanyia Nchi ni udhaifu wa hali ya juu na uwezo mdogo kwa nafasi nyeti ya uSpika aliyozawadiwa.
   
 15. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #15
  Dec 13, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Usimshangae huyu na misimamo yake kwani ni mtu wa USALAMA WA TAIFA!!
   
 16. M

  Mopalmo JF-Expert Member

  #16
  Dec 13, 2011
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani ni nan asiyejua uroho wa madaraka alionao,acha kutetea uozo
   
 17. HT

  HT JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye upper case, have definitions changed? What is definition of each word?????
   
Loading...