Chinua Achebe na Wole Soyinka, manguli wa FasihiaAndishi Barani Africa

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
UPANDE wa kushoto namuona Chinua Achebe, gwiji wa fasihi ya kiafrika ambaye vitabu vyake vinatumika kwenye shule na vyuo mbalimbali ulimwenguni. Lakini kwa upande wa kulia macho yangu yanatua kwa nguli mwingine kwenye sanaa ya uandishi ambaye mwaka 1986 aliweka rekodi ya kuwa mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Nobel ya fasihi. Huyo sio mwingine bali ni Wole Soyinka, Profesa aliyefundisha vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo Havard, Yale na Oxford.

Sio Soyinka tu, hata Chinua Achebe naye ni Profesa. Akifundisha katika vyuo vya Bard College, na chuo kikuu cha Brown vyote vya huko Marekani. Hatuwezi kumsahau nguli huyu raia wa Nigeria kwani Januari 1966 alichapisha kitabu kilichoitwa 'A man of the People' kilichozungumzia maovu ya serikali za kiafrika ikiwemo rushwa, utawala mbovu, n.k. Watu wengi walimuita Chinua Achebe 'nabii' kutokana na mambo aliyoyaandika kitabuni humo kwani yalikuja kutokea kweli siku chache zilizofuata. Mfano, katika kitabu hicho alieleza kuhusu kupinduliwa kwa kiongozi mmoja aliyempa jina la 'Chifu Nanga'. Lakini cha kushangaza ni kwamba siku chache tu baada ya kuachiwa kitabu hicho, Nigeria ilipata mtikisiko baada ya kufanyika kwa mapinduzi yaliyopelekea kifo cha waziri mkuu wa nchi hiyo bwana Abubakar Balewa.

Mapinduzi hayo yalikuja kuzaa vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoitwa 'Biafra War' kufuatia gavana wa jimbo la kusini mashariki linalokaliwa na waigbo wengi kutangaza kujitenga na nchi ya Nigeria ili kuanzisha taifa jipya waliloliita Biafra. Katika vita hiyo, mwandishi Wole Soyinka, alikamatwa na kutupwa miaka miwili jela kwa kile kinachodaiwa kwamba alionekana akifanya mazungumzo na kiongozi wa Biafra, bwana Chukwuemeka Ojukwu. Wakati Soyinka yupo Gerezani, Chinua Achebe yeye alikimbilia nchini Marekani akiwa na familia yake ambapo alikuja kurejea tena baada ya kumalizika kwa vita ya Biafra mwaka 1970 na kukuta nyumba yake imeharibiwa na vita.

Wakati Achebe anarudi nyumbani, Soyinka alikuwa ameenda nchini Ufaransa baada ya kuachiwa huru mwaka 1969. Akiwa Ufaransa aliandika shairi lake lililoitwa 'Poems from Prison'. Baada ya kuondoshwa kwa utawala wa Rais Yakubu Gowon, Wole Soyinka alirejea nyumbani Nigeria na kuendelea kufundisha katika chuo kikuu cha Ife. Wakati Soyinka anarejea nchini, Chinua Achebe alikwenda nchini Marekani alipoajiriwa katika chuo cha Massachusetts. Akiwa huko aliachia kitabu cha 'Morning Yet on Creation Day'. Mwaka 1976 alirejea tena Nigeria akiendelea na kazi yake ya uandishi huku akifundisha katika chuo kikuu Nigeria.

Wakati Achebe yupo Nigeria University, Wole Soyinka alikuwa akifundisha Chuo kikuu cha Ife huku akijikita zaidi katika siasa za Nigeria, akikosoa vikali rushwa katika utawala wa Rais Shehu Shagari ambaye alipinduliwa mwaka 1983 na Muhammad Buhari kuingia madarakani. Soyinka aliendelea kukosoa utawala wa kijeshi wa Buhari. Mwaka 1984 mahakama ya Nigeria ilifungia kitabu cha Soyinka kilichoitwa 'The Man Died'. Lakini miaka miwili iliyofuata alipokea tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Mwaka 1990 ulikuwa ni mwaka mbaya kwa Chinua Achebe, kwani alipata ajali ya gari akiwa huko Lagos Nigeria. Ajali hiyo ndiyo iliyopelekea nguli wa fasihi Chinua Achebe kumalizia maisha yake akiwa kwenye kiti cha magurudumu kwani alipooza sehemu ya kiunoni kushuka chini. Alipelekwa nchini Uingereza kwa matibabu na baadae kuelekea nchini Marekani. Wakati huo, mwaka 1993 Nigeria ilipata Uongozi mpya baada ya mapinduzi yaliyofanywa na Sani Abacha. Sani Abacha aliogopwa Sana nchini Nigeria, watu wengi walikimbia nchi akiwemo Wole Soyinka aliyekimbilia nchini Marekani ambapo huko alikwenda kufundisha kwenye chuo kikuu.

Wole Soyinka alirudi tena nchini Nigeria mwaka 1999, hiyo ni baada ya kufariki dikteta Sani Abacha mwaka uliotangulia. Na mwaka huo pia tulimuona Chinua Achebe akirejea Nigeria akitokea nchini Marekani, baadae akirejea tena nchini Marekani kufundisha katika chuo kikuu Cha Bard na baadae Brown University.

Tarehe 21 March 2013 Ilikuwa ni siku ya majonzi kwa Dunia nzima hasa Waafrika baada ya kufariki kwa nguli huyo wa fasihi Afrika na ulimwenguni, namaanisha Chinua Achebe aliyefariki huko Marekani akiwa na umri wa miaka 82. Achebe ameacha vitabu zaidi ya 100 huku vitabu vyake vingi vikiwa ni riwaya huku Things Fall Apart ikiwa ni riwaya yake pendwa kuliko zote ikiuza zaidi ya nakala milioni 15.

Wole Soyinka naye ana vitabu zaidi ya 100 huku vingi vikiwa ni mashairi na tamthilia ikiwemo ile tamthilia maarufu ya 'Death and the King's Horseman' iliyotoka mwaka 1975. Kwa Sasa Soyinka yupo anaendelea na uandishi, akialikwa kutoa mhadhara katika vyuo mbalimbali na ana umri wa miaka 85.

Mwisho.

Imeandikwa na
©KichwaKikuu.
 
Ukiachana na wakina chinua Achebe Vitu nilivyoviona ni wanigeria wanasafiri Sana nje Sisi kupata passport kama umepata roho mpya.Na sijui Kwa nini hutuvutani mtu akienda nje anatakiwa amvute mwenzie kama wakenya na wanaijeria. Tumaini The Genius, Tutaishia kusafiri mikoani Tu.
IMG_20191118_014650.jpeg
 
Hongera kwa uchmbuzi mzuri,nimeona kitu cha kujifunza hapa,kumbe Watu wenye uoni wa mbele hawapendwi na Serikali za Kiafrika,ndo maana wandishi hawa nguli walipata Tabu sana kama wanavyopata tabu wale jamaa wanao kesha mahakamani kila mwezi. au na wale walioko Mahabusu kwa Miaka zaidi ya 7
 
Ukiachana na wakina chinua Achebe Vitu nilivyoviona ni wanigeria wanasafiri Sana nje Sisi kupata passport kama umepata roho mpya.Na sijui Kwa nini hutuvutani mtu akienda nje anatakiwa amvute mwenzie kama wakenya na wanaijeria. Tumaini The Genius, Tutaishia kusafiri mikoani Tu.
View attachment 1267736
Sio kweli kwamba kupata passport ni kazi namimi niliaminishwa hivyo lakini nimeipata kwa week 1 bila ya kumpa yeyote pesa,nenda uhamiaji na doc zako usiskilize maneno ya vijiweni.
 
Wanaijeria walipata exposure hata Africa mashariki nako Kuna miamba ya Fasihi.Nilienda TPH kununua Riwaya ya Prof mmoja hivi nikashangaa Bei Kali kwa Nini hii Bei imekuwa kubwa?wanasema vitabu vinatoka Nairobi yaani vitabu vya Watanzania vinatokea Nairobi vinakuja Dar tunauziwa kwa Bei Kali wakati wengine wako hapo UDSM.Nilichogundua wenzetu Kenya ni wasomaji wa vitabu kuliko Watanzania so ukisikia baada ya Wanaijeria wanafuata Wakenya usishangae akatajwa na Mtanzania humo akipewa uraia wa Kenya.
 
UPANDE wa kushoto namuona Chinua Achebe, gwiji wa fasihi ya kiafrika ambaye vitabu vyake vinatumika kwenye shule na vyuo mbalimbali ulimwenguni. Lakini kwa upande wa kulia macho yangu yanatua kwa nguli mwingine kwenye sanaa ya uandishi ambaye mwaka 1986 aliweka rekodi ya kuwa mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya Nobel ya fasihi. Huyo sio mwingine bali ni Wole Soyinka, Profesa aliyefundisha vyuo vikuu mbalimbali ikiwemo Havard, Yale na Oxford.

Sio Soyinka tu, hata Chinua Achebe naye ni Profesa. Akifundisha katika vyuo vya Bard College, na chuo kikuu cha Brown vyote vya huko Marekani. Hatuwezi kumsahau nguli huyu raia wa Nigeria kwani Januari 1966 alichapisha kitabu kilichoitwa 'A man of the People' kilichozungumzia maovu ya serikali za kiafrika ikiwemo rushwa, utawala mbovu, n.k. Watu wengi walimuita Chinua Achebe 'nabii' kutokana na mambo aliyoyaandika kitabuni humo kwani yalikuja kutokea kweli siku chache zilizofuata. Mfano, katika kitabu hicho alieleza kuhusu kupinduliwa kwa kiongozi mmoja aliyempa jina la 'Chifu Nanga'. Lakini cha kushangaza ni kwamba siku chache tu baada ya kuachiwa kitabu hicho, Nigeria ilipata mtikisiko baada ya kufanyika kwa mapinduzi yaliyopelekea kifo cha waziri mkuu wa nchi hiyo bwana Abubakar Balewa.

Mapinduzi hayo yalikuja kuzaa vita ya wenyewe kwa wenyewe iliyoitwa 'Biafra War' kufuatia gavana wa jimbo la kusini mashariki linalokaliwa na waigbo wengi kutangaza kujitenga na nchi ya Nigeria ili kuanzisha taifa jipya waliloliita Biafra. Katika vita hiyo, mwandishi Wole Soyinka, alikamatwa na kutupwa miaka miwili jela kwa kile kinachodaiwa kwamba alionekana akifanya mazungumzo na kiongozi wa Biafra, bwana Chukwuemeka Ojukwu. Wakati Soyinka yupo Gerezani, Chinua Achebe yeye alikimbilia nchini Marekani akiwa na familia yake ambapo alikuja kurejea tena baada ya kumalizika kwa vita ya Biafra mwaka 1970 na kukuta nyumba yake imeharibiwa na vita.

Wakati Achebe anarudi nyumbani, Soyinka alikuwa ameenda nchini Ufaransa baada ya kuachiwa huru mwaka 1969. Akiwa Ufaransa aliandika shairi lake lililoitwa 'Poems from Prison'. Baada ya kuondoshwa kwa utawala wa Rais Yakubu Gowon, Wole Soyinka alirejea nyumbani Nigeria na kuendelea kufundisha katika chuo kikuu cha Ife. Wakati Soyinka anarejea nchini, Chinua Achebe alikwenda nchini Marekani alipoajiriwa katika chuo cha Massachusetts. Akiwa huko aliachia kitabu cha 'Morning Yet on Creation Day'. Mwaka 1976 alirejea tena Nigeria akiendelea na kazi yake ya uandishi huku akifundisha katika chuo kikuu Nigeria.

Wakati Achebe yupo Nigeria University, Wole Soyinka alikuwa akifundisha Chuo kikuu cha Ife huku akijikita zaidi katika siasa za Nigeria, akikosoa vikali rushwa katika utawala wa Rais Shehu Shagari ambaye alipinduliwa mwaka 1983 na Muhammad Buhari kuingia madarakani. Soyinka aliendelea kukosoa utawala wa kijeshi wa Buhari. Mwaka 1984 mahakama ya Nigeria ilifungia kitabu cha Soyinka kilichoitwa 'The Man Died'. Lakini miaka miwili iliyofuata alipokea tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Mwaka 1990 ulikuwa ni mwaka mbaya kwa Chinua Achebe, kwani alipata ajali ya gari akiwa huko Lagos Nigeria. Ajali hiyo ndiyo iliyopelekea nguli wa fasihi Chinua Achebe kumalizia maisha yake akiwa kwenye kiti cha magurudumu kwani alipooza sehemu ya kiunoni kushuka chini. Alipelekwa nchini Uingereza kwa matibabu na baadae kuelekea nchini Marekani. Wakati huo, mwaka 1993 Nigeria ilipata Uongozi mpya baada ya mapinduzi yaliyofanywa na Sani Abacha. Sani Abacha aliogopwa Sana nchini Nigeria, watu wengi walikimbia nchi akiwemo Wole Soyinka aliyekimbilia nchini Marekani ambapo huko alikwenda kufundisha kwenye chuo kikuu.

Wole Soyinka alirudi tena nchini Nigeria mwaka 1999, hiyo ni baada ya kufariki dikteta Sani Abacha mwaka uliotangulia. Na mwaka huo pia tulimuona Chinua Achebe akirejea Nigeria akitokea nchini Marekani, baadae akirejea tena nchini Marekani kufundisha katika chuo kikuu Cha Bard na baadae Brown University.

Tarehe 21 March 2013 Ilikuwa ni siku ya majonzi kwa Dunia nzima hasa Waafrika baada ya kufariki kwa nguli huyo wa fasihi Afrika na ulimwenguni, namaanisha Chinua Achebe aliyefariki huko Marekani akiwa na umri wa miaka 82. Achebe ameacha vitabu zaidi ya 100 huku vitabu vyake vingi vikiwa ni riwaya huku Things Fall Apart ikiwa ni riwaya yake pendwa kuliko zote ikiuza zaidi ya nakala milioni 15.

Wole Soyinka naye ana vitabu zaidi ya 100 huku vingi vikiwa ni mashairi na tamthilia ikiwemo ile tamthilia maarufu ya 'Death and the King's Horseman' iliyotoka mwaka 1975. Kwa Sasa Soyinka yupo anaendelea na uandishi, akialikwa kutoa mhadhara katika vyuo mbalimbali na ana umri wa miaka 85.

Mwisho.

Imeandikwa na
©KichwaKikuu.
Africans americaz
 
Things Fall Apart; inaanza hivi:
Okonkwo was well known throughout nine villages. As a young man of 18 years, had brought honor to his village by throwing Amalinze, the cat. Amalinze was a great wrestller who for seven years was unbeaten from all Mbaino to Umuofia. It was this man that he threw him in a fight......
 
Back
Top Bottom