Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 198
- 322
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan binafsi alihudhuria ufunguzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki na kukata utepe, akisema Kituo hicho si kama tu ni kituo cha biashara, bali pia kinajumuisha maghala ya nje, biashara ya mtandaoni ya kuvuka mipaka, na usindikaji wa dhamana, na ni jukwaa la jumla la kibiashara. Anaona kuwa Kituo hicho kitaimarisha uwezo wa Tanzania wa kuunganisha masoko ya nchi za kusini na mashariki mwa Afrika, na kwamba kituo hicho pia kimeonesha mafanikio ya ushirikiano kati ya Tanzania na China.
Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki kiliwekezwa na kampuni ya China kwa dola milioni 170 za Kimarekani. Kina eneo la mita 75,000 za mraba, na takriban maduka 2,000. Kabla ya kufunguliwa rasmi, maduka 1,300 tayari yalikuwa yamenunuliwa.
Je, ni kwa nini Kituo hicho kinapendwa sana? Sababu kuu ni kupunguza muda wa mzigo kusafirishwa. Kwa mfano, zamani ilichukua siku 45 kwa kahawa kutoka Rwanda kufika nchini Kenya kupitia Dubai. Lakini sasa, kwa kupitia kituo hicho, inachukua siku saba tu.
Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Afrika Mashariki sio mfano pekee wa China na Tanzania kuimarisha ushirikiano katika usafirishaji. Wiki moja tu iliyopita, Rais Samia aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Usafirishaji cha Kwala na Bustani ya Viwanda ya China na Tanzania katika Mkoa wa Pwani nchini humo. Rais Samia alibainisha kuwa miundombinu hiyo ni muhimu kwa ushirikiano wa kikanda, kuimarisha zaidi uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na nchi jirani na kukuza mafungamano kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Afrika Mashariki.
Kituo cha Kimataifa cha Usafirishaji cha Kwala na Bustani ya Viwanda ya China na Tanzania, inayojengwa kwa ushirikiano kati ya China na Tanzania, ina eneo la zaidi ya hekta 1,000, na itakuwa injini kuu ya kuhimiza uboreshaji wa sekta ya viwanda na usafirishaji nchini Tanzania. Kituo hicho kinatarajia kuvutia uwekezaji zaidi ya dola bilioni 3 za Kimarekani, na kutoa ajira 300,000.
Miradi hiyo inatokana na uhusiano wa kirafiki wa muda mrefu kati ya China na Tanzania, pia ni matokeo mengine muhimu ya nchi hizo mbili katika kukuza ushirikiano kufuatia pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.