Hujui usemalo na inawezekana huujui uwezo wa mchina kiteknolojia kwamba ana uwezo wa kutengeneza kuanzia vitu vidogo sana kama toothpick na office pin, mpaka vitu vikubwa kama sattelite za kwenda anga za juu, super computers, meli, ndege n.k. Wigo wako inavyoelekea umeishia kwenye redio, simu, viatu na makomeo; vitu ambavyo hutengenezwa kwa ubora hafifu unaoagizwa na wafanyabiashara wetu ili wapate faida maradufu. Na kwa sababu hapa kwetu huingia bwerere bila ukaguzi wa viwango vinavyokubalika kimataifa au kitaifa (kama vipo), matokeo yake ni kuzagaa kwa bidhaa hafifu sokoni. Bidhaa za kichina anazouza kwenye soko la ulaya na marekani, zina viwango vinavyokubalika kwenye nchi hizo, na mara nyingine zina viwango vya juu zaidi kwa sababu nchi hizo huviweka kwa bidhaa za mchina kwa makusudi ili bidhaa zake zisifurike kwenye nchi hizo; pamoja na hayo, bado bidhaa za mchina zipo katika nchi zote za ulaya na marekani. Ok; umesema mchina ni mzee wa feki, nitajie bidhaa tatu au zaidi za viwandani ambazo zimeundwa Tanzania (siyo zimeunganishwa), ukiacha bidhaa za kilimo na mifugo zilizoongezwa thamani kama sigara, nguo, juisi, biskuti, sukari n.k.