China yaonesha hadharani ndege mpya za kivita

China yaonesha hadharani ndege mpya za kivita

Life2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,387
Reaction score
4,880
_92205214_j20zhuhaipair.jpg

China imeonyesha hadharani ndege zake mpya za kivita aina ya J-20 ambazo zina uwezo wa kujificha na kukosa kuonekana kwenye mitambo ya rada.

Ndege mbili za aina hiyo zilipaa angani kwa sekunde 60 wakati wa maonesho ya ndege ya Zhuhai katika mkoa wa Guangdong.

Maonesho hayo huwa makubwa zaidi nchini humo na huwakutanisha waundaji na wanunuzi wa ndege.

Ndege hizo zinatazamwa na wengi kama ishara ya hamu ya Beijing kuboresha na kuimarisha uwezo wake kijeshi.

Rais wa China Xi Jinping anataka kuimarisha majeshi ya nchi yake huku taifa hilo likiendelea kudhihirisha ubabe sana kuhusu umiliki wa maeneo ya bahari Kusini na Mashariki mwa China.

Ndege hizo za J-20 zimeundwa na kampuni ya Chengdu Aircraft Industries Group, ambayo ni kampuni tanzu ya shirika la ndege la China ambalo kwa Kiingereza hufahamika kama Aviation Industry Corporation of China.

Baadhi wamelinganisha ndege hizo na ndege aina ya F-22 Raptor za Lockheed Martin.

Mchanganuzi wa masuala ya ndege Bradley Perret amesema ndege hiyo "bila shaka ni hatua kubwa katika uwezo wa kivita wa China".

Ndege ya kwanza kabisa ya kubeba mizigo mizito ambayo imetengenezewa nchini China, ndege ya Y-20, pia imezinduliwa katika maonesho hayo.

Ndyingine zinazotarajiwa ni ndege kubwa ya AG-600 ya kusaidia katika uokoaji na kushika doria baharini.

Aidha, ndege ya kivita ya kuangusha mabomu kwa jina Xian H-6K na helikopta ya kutekeleza mashambulizi ya Changhe Z-10K zitazinduliwa.

Chanzo: BBC
 
wazee wa fake
Hujui usemalo na inawezekana huujui uwezo wa mchina kiteknolojia kwamba ana uwezo wa kutengeneza kuanzia vitu vidogo sana kama toothpick na office pin, mpaka vitu vikubwa kama sattelite za kwenda anga za juu, super computers, meli, ndege n.k. Wigo wako inavyoelekea umeishia kwenye redio, simu, viatu na makomeo; vitu ambavyo hutengenezwa kwa ubora hafifu unaoagizwa na wafanyabiashara wetu ili wapate faida maradufu. Na kwa sababu hapa kwetu huingia bwerere bila ukaguzi wa viwango vinavyokubalika kimataifa au kitaifa (kama vipo), matokeo yake ni kuzagaa kwa bidhaa hafifu sokoni. Bidhaa za kichina anazouza kwenye soko la ulaya na marekani, zina viwango vinavyokubalika kwenye nchi hizo, na mara nyingine zina viwango vya juu zaidi kwa sababu nchi hizo huviweka kwa bidhaa za mchina kwa makusudi ili bidhaa zake zisifurike kwenye nchi hizo; pamoja na hayo, bado bidhaa za mchina zipo katika nchi zote za ulaya na marekani. Ok; umesema mchina ni mzee wa feki, nitajie bidhaa tatu au zaidi za viwandani ambazo zimeundwa Tanzania (siyo zimeunganishwa), ukiacha bidhaa za kilimo na mifugo zilizoongezwa thamani kama sigara, nguo, juisi, biskuti, sukari n.k.
 
sio kwamba hajui asemalo ni ukweli mtupu kwamba wachina ni mabingwa wa kucopy, fanya utafiti mkuu wame copy kuanzia magari mifano michache BWM mini cooper, ROLLS ROYCE ya muingereza n.k na kuyapa majina ya kwao.
kwa upande wa vifaa vya kijeshi mfano wame copy Mig 35 ya mrusi, last time i checked urusi wamekataa kuwauzia the most effective anti aircraft system zinazojulikana kama S-400 kwa madai ya warusi wenyewe kuwa the system is too sophisticated for "reverse engineering " ambayo wachina wanaitumia kwa kununua product chache then kujaribu kuzi study kwa muda na kisha kuja na model zao ambazo ndio fake.
Yote kwa yote i appriciate jamaa coz they have done a lot in the past 6 decades or so, ni mfano wa kuigwa na mataifa yanayoendelea.
 
Natamani na si tungekuwa wezi kama wa china !
Sisi Wizi wetu cjui ukojeukoje siuelewi kabisa;
Wizi wetu umesahau sendals nje, hujaanua nguo usiku watu wanazipitia.
Hata kama kucopy technological equipment bidhaa kutoka nje, hivyo viwanda vya kutengeneza copies tunavyo? Jibu hatuna so We are the failures in everything.
 
Photocopy ya F-22 Reptor..wachina wezi sana aseee.
Watakua may b wamekop nje tyu hyo ndege haiifikii na wala haitoweza kuifikia F22...injini zenyewe za ndege zimetoka Russia tena injin za 4th gen aircraft half hyo ndege sidhan km ina uwezo wa kuSupercruise without using an afterburner Coz ya injin zilizotumika hvyo inaifanya iwe vulnerable kwa Heat seeking missiles.... Tuje kwenye rada, hpa ndo kabisa hawagusi Coz rada ya F22 inakudetect wewe wakt yenyewe inakua hard to detect(hii ni kutokana na maonyesho ya anga waliofanya NATO mwaka Jana km sikosei, zile Rafael za France ambazo zina powerful radar na zile Typhoon za Europe pamoja na Gripen za Sweden bila kusahau F15E,F16V,nk.... Zilishindwa kuidetect F22 but f22 iliweza kuzidetect bila ya wao kujua km wameonwa, na hii ilielezwa na maPilot kwenye hayo mazoezi unaweza kutafuta jata YouTube kwa maelezo zaid)....Pia kwenye hii radar ya F22 rudia ile incident ya Iran ambapo ndege yake ilitaka kuilipua drone ya kimarekan F22 ikatumwa kuiIntercept hyo ndege, chaajabu F22 ilifika mpk ilipo ndege ya Iran ikaizunguka juu chin juu chin pamoja na kuangalia silaha ilizonazo ilivyomaliza ikaipa warning ndege ya Iran iondoke eneo hilo.(kiufup hpa tunaweza sema kwamba radar za ndege ya Iran zilikua jammed na F22 raptor)
 
Attachments

  • Screenshot_2016-11-02-20-30-07.png
    Screenshot_2016-11-02-20-30-07.png
    44.3 KB · Views: 49
  • PhotoGrid_1478107906533.jpg
    PhotoGrid_1478107906533.jpg
    87.4 KB · Views: 53
Copy and paste katika mambo ya kijeshi ni vitu vya kawaida sana, ndo maana tuna vitengo vya wapelelezi. Moja ya kazi kubwa ya vitengo vya upelelezi ni pamoja na kufuatilia na kujua mwenzako ana nini kipya na kama ni kizuri na kuna uwezekano wa kuiba technology yake unaiba tu, kuiba tech ya mwenzako ina faida mbili, kwanza inakupa uwezo wa kutengeneza kinga dhizi ya hiyo tech pili ibakuwezesha kutengeneza vitu vyako kwa tech mpya uliyoiiba, si urusi si marekani zite zinafanyiana hivyo, ndo maana msamiati wa udukuzi umeshika chati sana.
Ukiona nchi imeanza kufanya safari za anga yenyewe na imeanza kujitegemea katika kutengeneza vifaa vya kijeshi jua hayo ni mafanikio makubwa mno, china mpaka sasa anamiliki kituo cha anga cha kwake peke yake na amefanikiwa kuwapeleka wanasayansi wake huko, hiyo copy and pasting basi inamsaidia sana maana ni nchi mbili tu zilizokuwa na uwezo wa kugharamia safari za wana anga kwenda kwenye obit ambazo ni urusi na marekani, na sasa china imekuwa ya tatu...mtakazana amecopy lakini mnasahau kama kucopy ni maendeleo pia,
 
Hata hiyo Y-20 ya kubebea mizigo wamejitahidi sana,punde wataanza kutengeza comercial airline kama zile boeing 777
 
Watakua may b wamekop nje tyu hyo ndege haiifikii na wala haitoweza kuifikia F22...injini zenyewe za ndege zimetoka Russia tena injin za 4th gen aircraft half hyo ndege sidhan km ina uwezo wa kuSupercruise without using an afterburner Coz ya injin zilizotumika hvyo inaifanya iwe vulnerable kwa Heat seeking missiles.... Tuje kwenye rada, hpa ndo kabisa hawagusi Coz rada ya F22 inakudetect wewe wakt yenyewe inakua hard to detect(hii ni kutokana na maonyesho ya anga waliofanya NATO mwaka Jana km sikosei, zile Rafael za France ambazo zina powerful radar na zile Typhoon za Europe pamoja na Gripen za Sweden bila kusahau F15E,F16V,nk.... Zilishindwa kuidetect F22 but f22 iliweza kuzidetect bila ya wao kujua km wameonwa, na hii ilielezwa na maPilot kwenye hayo mazoezi unaweza kutafuta jata YouTube kwa maelezo zaid)....Pia kwenye hii radar ya F22 rudia ile incident ya Iran ambapo ndege yake ilitaka kuilipua drone ya kimarekan F22 ikatumwa kuiIntercept hyo ndege, chaajabu F22 ilifika mpk ilipo ndege ya Iran ikaizunguka juu chin juu chin pamoja na kuangalia silaha ilizonazo ilivyomaliza ikaipa warning ndege ya Iran iondoke eneo hilo.(kiufup hpa tunaweza sema kwamba radar za ndege ya Iran zilikua jammed na F22 raptor)
Nimekusoma vyema sana mkuu.Pia kwa sasa US walishasign contract kwa ajili ya kutengeneza B-21 steath bomber kwa ajili ya ku replace B-1 lencer na B-52.Contract inagherimu kiasi cha $80billion,Mwaka 2020 zitakuwa ready for combat.
 
Hata hiyo Y-20 ya kubebea mizigo wamejitahidi sana,punde wataanza kutengeza comercial airline kama zile boeing 777
Unasifia copying.Walivyo wapuuzi na sasa waluishacopy na zile B-2 Steath..Washaanza kutengeneza za kwao..Poor wachina.
 
Back
Top Bottom