China yanyonga hadharani wanasiasa 26

Marekani je??
 
Hao hao unaosema wana demokrasia kipindi wanatafuta maendeleo ya nchi zao hawaku implement democracy walivamia Africa ,Asia wakachapa bakora na kunyonga watu mpaka walipopata maendeleo makubwa ndio waka implement democracy

Sasa nyie mpo fukara developing country kamwe hamtoendelea na democracy ..
 
Hizo sheria zikifika humu majizi mengi yatanyongwa!Ingependeza kama zingekuepo haya mafisadi yasingekuepo.
 
Bila kujali chama, wanasiasa wachache sana wanaweza kupona hii kitu. Lakini hii picha na hii habari sio vya hivi karibuni, nimejaribu kufuatilia vyanzo vya kuaminika haipo. Hiyopicha inahusishwa na habari tofauti.
 
Mi nahisi nchi zetu za ki Africa zi adopt hii system mijitu inakomba na kufilisi nchi kwa mgongo wa siasa uchwara na uongozi , maendeleo yanadumaa baadhi mijitu inaneemeka na kuota vitambi................Mamilioni wanasuffer hadi kufa kwa njaa , maradhi na umasikini wa kutupwa..........hivi jamani sisi na nchi zetu hizi na resources zote tulizonazo unafikiri leo hii tungekuwa ni wa kutukanwa kama mbwa na hawa wageni , kutumikishwa kama watumwa kwenye miradi yao , kukimbilia ulaya ................tutaendelea kulalamika kuwa tunanyonywa miaka 1000 aisee lakini chanzo kikubwa ni sisi wenyewe , mi ninahisi sheria kali kama hizi ndio zitasaidia kuongeza trustfulness na usimamizi bora wa mapato na rasilimali za umma
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] unaogopa kifo sio?
 
Kwa kifupi, nchi inayotekeleza adhabu ya kifo hadharani bado haijaingia kwenye jamii ya wastaarabu. Utajiri si kitu mbele ya kukosa ustaarabu. Inaniwia taabu sana kuamini kuwa China ya leo hii inaweza kuendekeza mfumo wa kishenzi kiasi hicho. Walioendelea zaidi, hiyo adhabu yenyewe walishaiondoa kwenye msamiati wao. Na haijawahi kuwa suluhisho ukiachilia mbali unafiki unaoambatana na utekelezaji wake.
 
Marekani ana utu? Uingereza ana utu?
 
Halafu Sasa Cha ajabu nchi zenye udikteta ndo zinazongoza kwa umaskini ukilinganisha na hao wenye demokrasia.

Zama hizi kuwabana watu ni kama kulifungia Bomu ndani ya Nyumba mda wowote linaweza kulipuka,watu wakishachoka hamna wa kuwazuia hata kwa Risasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…