China Viongozi Wazembe hutwangwa Risasi hapa Kutumbuliwa tu eti wanasema Udikteta!

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,552
Nadhani ni watanzania wengi hasa sie wa hali ya chini tunaona ni kama Jpm ameletwa na mungu!kwa jinsi ilipokua imefikia na yeye kuingia na kasi yake kweli ni muujiza.

Tumeshuhudia jana ofisi ya bunge ikisalimisha Tsh bilion 6,pesa ambazo tayari zimeelekezwa kwenye madawati nchi nzima!Kwa kipindi kifupi kawabana mafisadi wengi,anachukia uzembe,anaokoa mabilioni yalokua yanaishia kwenye matumbo ya wachache,anabomoa nertwork nyingi za wizi na ukwepaji kodi.

Anachukua hatua kali kwa viongozi wazembe halafu baadhi ya watu wanasema ooh dikteta ..hata nchi nyingi zilizoendelea zilifanya haya na zaidi ya haya.

Hongera sana Mh Rais nadhani sasa wataelewa vizuri falsafa yako ya HAPA KaZI TU mungu akulinde watanzania tulio wengi tupo pamoja nawe kwa maombi na dua.
 
Ipitishwe sheria kila anayetumbuliwa acharazwe viboko 30 ili wapate akili zaidi. Kwanza Magufuli mpole sana, ilitakiwa huyo Kilango awekwe ndani kabisa
 
ibanezafrica

Kichwa chako cha habari si ukweli.

Tuwekee ushahidi wa kiongozi yoyote wa China aliyepigwa risasi kwa uzembe.

Nijuavyo China wanasheria ya kuua kwa kupiga risasi kwa viongozi au yeyote yule kwa makosa mengi tu, yakiwemo ya ubadhirifu wa mali za umma, wizi wa mali za umma, rushwa, mihadarati, kuuwa, kuweka watumwa.

Hilo ulisemalo la uzembe sijawahi kusikia na ndiyo kwanza leo nnalisoma kwako. Tafadhali weka ushahidi na kama hauna futa kichwa chako cha habari kwani utakuwa ni uongo.
 
Magufuli hana strategy yeyote ya kuongoza nchi anataka kutawala hapo ndio atakapoisoma namba yake mwenyewe china tangu mwaka 47 wanaua wabadhrifu na wala rushwa hadi sasa bado wanaua kwa hiyo njia ya kuuwa kudharilisha sio jibu sahihi na la mwisho, na ndicho magufuli anaelezwa kwama udikteta haujawahi shinda
 
ibanezafrica

Kichwa chako cha habari si ukweli.

Tuwekee ushahidi wa kiongozi yoyote wa China aliyepigwa risasi kwa uzembe.

Nijuavyo China wanasheria ya kuua kwa kupiga risasi kwa viongozi au yeyote yule kwa makosa mengi tu, yakiwemo ya ubadhirifu wa mali za umma, wizi wa mali za umma, rushwa, mihadarati, kuuwa, kuweka watumwa.

Hilo ulisemalo la uzembe sijawahi kusikia na ndiyo kwanza leo nnalisoma kwako. Tafadhali weka ushahidi na kama hauna futa kichwa chako cha habari kwani utakuwa ni uongo.

Umekuja kumtetea mzaramo???
 
Ndugu hebu Jaribu u Google jina hili Hyon Yong-Choi Bbc Swahili uone kilichompata waziri huyu wa ulinzi kwa kuonyesha uzembe pale tu aliposinzia rais akihutubia...huyu bwana amepigwa na kombora la kutungulia ndege! Mbele ya mamia ya maafisa wa jeshi na mifano ipo mingi muda tu sina ila angalia mitandaoni ujiridhishe
 
Hiyo haikuwa China, inasemekana ilitokea Korea Kaskazini. Nasema inasemekana kwa kuwa hizo zinaweza kuwa ni story za kupika za media za kimagharibi kwani hao wa Korea ya Kaskazini wanawahenyesha sana magharibi.

Korea Kaskazini na China ni nchi tofauti kabisa.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Back
Top Bottom