Eti jenerali wa jeshi la marekani alitembelea China akapelekwa kambi moja ya jeshi. Akiongea kiingereza na jenerali wa kichina anawatafsiria askari wake kwa kichina. Baada ya kuhutubia mambo rasmi akaamua kutoa kichekesho. Sasa akasimulia kichekesho kwa muda wa dakika tano. Generali wa kichina akaongea sentensi moja tu, askari wake wakacheka dakika tatu nzima. Huyu mmarekani akamuuliza bosi mwenzie mbona yeye amesimulia kwa dakika tano nzima yeye kaongea sentensi moja tu lakini vijana wamecheka sana? Akamwambia nimeona joke ni ndefu sana nikawaambia UMETOA KICHEKESHO, WACHEKE KWA DAKIKA TATU. NDIO WAKACHEKA