China iliweza kuondokana na kasumba ya kuajiriwa kwa kuweka mazingira mazuri ya ujasiriamali

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
Fadhili Mpunji

VCG111375664277.jpg

Changamoto ya ajira kwa vijana katika nchi nyingi za Afrika ni jambo ambalo linazungumzwa sana na wanasiasa na watunga sera. Karibu kila nchi ya Afrika ina tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana, tofauti ni kwamba ukubwa wa tatizo hilo unatofautiana kwa kila nchi, na kila nchi inatumia njia zinazoendana na mazingira yake kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Tatizo la ajira katika nchi nyingi za Afrika hasa katika nchi za Afrika mashariki linatokana na kasumba ya elimu ya kikoloni, ambayo ilimwandaa mwafrika kuwa mtumishi wa umma au mwajiriwa kwenye mashirika ya serikali au makampuni ya kigeni. Mtazamo huu uliwafanya wengi wapiganie elimu itakayowawezesha kuajiriwa kwa namna hiyo. Wale walioshindwa kupata ajira za namna hiyo, walionekana kama ni watu wa daraja la pili.

Mtazamo huu kwa sasa unaonekana kubadilika, vijana wengi hasa katika miji mikubwa ya Afrika Mashariki iwe ni Nairobi, Dar es salaam au Kampala, moyo wa ujasiriamali na kujiajiri unaonekana kushika kasi. Hata hivyo kutokana na kasumba ya muda mrefu, bado watunga sera, wazazi na hata jamii, haiwatazami wale wanaojiajiri kwa jicho sawa na wale walioajiriwa kwenye utumishi wa umma. Na wale wanaotoa sauti ya kutaka vijana wajiajiri, ni wale walioshindwa kazi ya kuwatafutia ajira vijana, na wao pia ni mfano mbaya kwa kuwa wao wenyewe ni waajiriwa na si waliojiari.

Kasumba ya kuajiriwa ilikuwepo nchini China kabla ya China kuanza sera ya mageuzi na kufungua mlango. Lakini kutokana na maendeleo ya kasi ya uchumi, muundo wa ajira nchini China umebadilika sana. Hata hivyo changamoto ya ajira kwa vijana ni changamoto ambayo kila mwaka inafuatiliwa sana. Kila mwaka karibu vijana milioni 10 wanaohitimu elimu ya vyuo wanaingia kwenye soko la ajira. Ni sehemu ndogo sana ya watu hao wanaweza kuajiriwa na serikali, walio wengi wanaajiriwa na makampuni binafsi ya wengine wanajiajiri. Kwa sasa takwimu zinaonesha kuwa ukosefu wa ajira mijini nchini China ni wastani wa asilimia 5.5, kwenye miji midogo na maeneo ya vijijini kiwango hicho ni zaidi ya asilimia 13. Kwa hiyo China pia licha ya kuwa haina tatizo kubwa la ukosefu wa ajira, nayo ina shinikizo la nafasi za ajira kwa vijana.

Kutokana na changamoto hii kila mwaka suala la nafasi za ajira huwa linapewa kipaumbele na serikali, na kila mwaka waziri mkuu wa China anapowasilisha ripoti ya kazi ya serikali kwenye bunge la umma, suala la ajira huwa ni moja ya vipaumbele. Hii haina maana kuwa serikali ndio inawaajiri wahitimu wote, bali inaratibu suala zima la ajira kwa kuhusisha sekta binafsi na kuweka mazingira rafiki kwa wale wanaotaka kuwa wajasiriamali.

Kwa China linapozungumzwa suala la nafasi za ajira na umuhimu wake kwa utulivu wa jamii, sekta binafsi inathaminiwa katika kushughulikia changamoto hiyo na inachukuliwa kwa umakini mkubwa. Kwa hiyo serikali kuweka mazingira mazuri ya ujasiriamali ni moja ya njia za kushughulikia tatizo la ajira.

Uzoefu unaoweza kuigwa kutoka kwa China, ni kuwa ni jambo lisilowezakana kwa serikali kuwa mwajiri wa wahitimu wote au wa vijana waliokosa ajira. Lakini pia suala la vijana kujiajiri linapozungumzwa, linatakiwa kuendana na kazi ya kuweka mazingira wezeshi kwa wale wanaopenda kujiajiri. Tayari vijana wengi wa nchi za Afrika mashariki wameonesha moyo wa ujasiriamali na kuchapa kazi, endapo mazingira wezeshi yataendelea kuboreshwa bila shaka wengi wataweza kujiajiri.
 
Back
Top Bottom