Leo hii kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Mhe. Hamad Rashid Mohamed amemuondoa Mhe. Cheyo kutokuwa tena msemaji wa upinzani katika wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi na hii inafuatia ukigeugeu wa Cheyo hadi jana akaenda kinyume na wapinzani wenzake kwa kuunga mkono bajeti ya serikali ya CCM