CHEYO anajisalimisha CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHEYO anajisalimisha CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kyindokyakombe, Jul 7, 2012.

 1. K

  Kyindokyakombe Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Namshauri CHEYO-UDP anachokifanya BUNGENI kwa sasa ni ujinga kwani anajitahidi kuisemea na kujisogeza zaidi upande wa CCM kulikO UPINZANI.REJEA jinsi alivyooneshwa kukerwa na suala la LEMA alivyosema WAZIRI MKUU PINDA alidanganya BUNGE.MGOMO wa MADAKTARI anajifanya kuwashambulia madaktari na upinzani huku akielewa kwamba madaktari wanatetea HUDUMA ZA AFYA ziboreshwe.Pia ile ishu ya ZITO kusainisha WABUNGE wasaini saini 70 za kutokuwa na IMANI na WAZIRI MKUU yeye alikataa kusaini.USHAURI atoke UPINZANI sasa ahamie CCM rasmi kuliko kuwa KIGEUGEU.Mwisho mnaotokea shinyanga kuweni na MSIMAMO SHIBUDA naye asikie.
   
 2. Mbelwa Germano

  Mbelwa Germano JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 789
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mfumo wa vyama vingi si tu mwanzo wa mapambazuko ya demokrasia na maendeleo nchini bali vyama makini ndio chimbuko la mabadiliko nchini. Cheyo ya chama chake wamekosa strategies za kujenga chama na kuleta ushindani wa kisiasa nchini...binafsi sijui hata jina la katibu wa UDP, agenda wanayosimamia ni nini? Na nikiri kwa kusema huyu mzee ni mbinafsi sana na sio kwa sababu ya kuunga mkono vyama vingine vya upinzani NO! ubinafsi ukaanza katika kuimarisha chama chake kama Mwenyekiti wa chama.

  Nilitegemea kwa uzoefu wake wa kisiasa wa muda mrefu ungelisaida sana chama chake kujijenga kama chama makini na ushandani Tanzania.
   
 3. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45

  Huna haja ya kupoteza muda wako Sisiem hatuhitaji zembereto kama hili, sisi ni watu wa msimamo tukisema hapana ni hapana na hakuna wakutugeuza, watu wa falsafa za kigagagigikoko hatuwahitaji tunataka watu kama Dr. Nape
   
 4. zaleo

  zaleo JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,733
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  SIo wote walioko kwenye vyama vya upinzani ni wapinzani. Wapo walio wapinzani kwelikweli lakini wapo walio wapinzani wa wapinzani na wametumwa hukohuko kuwadhibiti. Ili kumnasa samaki lazima uende kwenye maji anamoishi samaki huyo.Usimshangae Cheyo kwa kuwa umemuona, wapo kibao! Kama unadhani nadanganya waulize Lamwai, yule aliyekuwa mwenezi wa CCM yule wa Temeke, halafu yule walimokuwa wamepanga TLP Argentina kuwataja wachache sana. Bora wanaojionyesha wazi wajulikane mapema kuwa sio wenzenu.
   
 5. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Cheyo ana kashfa Swaziland (alianzisha kiwanda cha ku-recycle glass kwa mkopo wa USD 250,000 toka Stanbic bank kwa udhamini wa serikali ya huko miaka ya 90 lakini akatokomea na pesa zote akarudi bongo). Kipindi kile hakukuwa na makubaliano ya kubadilishana watuhumiwa - japo leo yapo - kati ya Tanzania na Swaziland. Cheyo leo hii akikanyaga ardhi ya swaziland tu jela itakuwa nyumbani kwake for the rest of his life. Na alipokuja huku alianzisha kampuni ya ujenzi na akapewa kujenga kijiji cha michezo - karibu na uwanja wa Taifa DSM, akala hela na hakujenga (siamini kama hicho kijiji kimeshakamilika kujengwa hadi leo). Kwa mantiki hiyo usitegemee Cheyo aipinge nyinyiem inayomlinda. Cheyo nae ni fisadi tu.
   
 6. MsemajiUkweli

  MsemajiUkweli JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 5, 2012
  Messages: 8,918
  Likes Received: 12,134
  Trophy Points: 280  Kuna hatari Tanzania kutawaliwa tena na watu wenye Mawazo na fikra za kidikteta. Udikteta wa fikra na mawazo tuliuondoa baada ya nchi kuingia katika siasa ya vyama vingi miaka kama 20 iliyopita(2 july 1992).

  Kwa sasa tumeanza kuona watu wenye mawazo kama hayo wakianza kumea. Mmojawapo ni wewe katika hii thread.
  Kama unampa ushauri Mh. John Cheyo, hiyo inakubalika. Lakini usitake mawazo yako yawe ndiyo sahihi na kusema anachokifanya bungeni ni ujinga wakati yuko bungeni kwa matakwa ya wananchi wa jimbo lake.
  kwa mawazo yako upinzani wa kweli ni kupinga kila kitu kifanywacho na serikali iliyoko madarakani. Ndugu yangu, haya ni mawazo mgando na yanatawaliwa na fikra za kidikteta.
  Msingi mkuu wa demokrasia ni kila mtu kuwa na haki sawa kifikra na kimatendo.

  Halafu unatoa ushauri kwa watu watokao Shinyanga wawe na msimamo. Msimamo upi?, au wawe na msimamo wa kimawazo kama yako (The dictatorship mentality). Who are you?
  I can't say you have wrong thinking in democratic world but I can say, you have corrupted thinking.

  Please, try to think bigger.
  Ubarikiwe na mawazo yako.
   
 7. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Cheyo hawezi hamia CCM kwani anajua hawezi pata ubunge. Ataendelea kuitumia UDP kuendeleza agenda zake binafsi pasipo kujali chama. He is a washed up politician.
   
 8. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kwa maoni yangu tatizo ni watawala ambao wametengeneza taratibu mbovu kwa manufaa yao. Ktk demokrasia ya vyama vingi,vyama vinaruhusiwa kufanya ushirikiano kisheria. Vyama shirika vinakua na jambo la msingi linalovifanya vishirikiane. Kwa hiyo isingekua ajabu leo Cheyo kushirikiana na CCM ama chama kingine. Tatizo hapa siyo hivyo. Na mbaya zaidi kanuni za bunge zinaviweka vyama vya upinzani kundi moja. Jambo ambalo siyo sahihi! Kuhusu mzee Cheyo ni wazi kwamba amefirisika kisiasa na sasa maisha yake ya kisiasa yanategemea CCM.
   
 9. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,635
  Likes Received: 4,745
  Trophy Points: 280
  Chezea njaa wewe!
   
 10. kupelwa

  kupelwa JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 874
  Likes Received: 139
  Trophy Points: 60
  wakati akina freeman mbowe waunda kambi rasmi ya upinzani bungeni, cuf nccr, tlp, na udp walilalamika sana.Lakini ndo hapo wadau mthibitishe kuwa CDM ni chama makini.Vyama vyote vya upinzani ambavyo havikuunda upinzani rasmi vina mapungufu mengi makubwa.Cuf inandoa na MAGAMBA,kila siku kuitetea serikali, UDP ni mfu, kinaendeshwa na wilaya moja ya bariadi.Nccr kinaendeshwa na mkoa mmoja napo kafulila kakalia kuti bovu, na mwenyekiti kapata hisani yakuwa ccmC, mzee wa kiracha , yeye hadharani alikuwa akimpigia kampeni JK huku akiwa anamgombea urais kwnye chama chake.Demokrasia ya nchi yetu namna inavyositawi, ina changamoto nyingi mno,mojawapo ni udhaifu wa itikadi,dira , sera,muono,na program sahihi zenye mwongozo sahihi wa kisiasa.Vyama vingi ni vichumia tumbo,na masilahi binafsi.Mzee mapesa ni mbunge mmoja pekee yake kutoka bariadi.Je ikatokea akaangushwa, unategemea ataishije?.ndo mikakati ya baadaye serikali imekumbuke kumpa hisani.Pia, babu huyo serikali ilimsaidia nyumba yake isipigwe mnada kule masaki.Unategemea, aisaliti magamba na serikali yake?, thubutu, hawezi, lazima alipe fadhila.
   
Loading...