Cheti cha kuzaliwa na cheti cha form four

R100

JF-Expert Member
Sep 11, 2014
337
81
Hivi kuna madhara gani kama jina Katika cheti cha kuzaliwa linatofautiana na cheti cha form four naombeni msaada
 
Yaan kuna madhara so kidogo hawezekan cheti chakuzaliwa kiwe tofaut na cheti ch 4four,
Inalete shida sana kweny maswala ya ajiri mikopo pia hutoweza pata
 
Naangalia majawabu maana hata mimi nipo hivyo, cheti cha kuzaliwa kina jina la urithi, nilipofika form II nikaamua kuweka jina la ubatizo hadi leo hakuna muunganiko wa hivyo vyeti viwili japo mambo yapo pouwa. Ngoja walete majibu, maana mimi jina la kwanza (first name) ktk cheti cha kuzaliwa ndilo jina la mwisho (surname) ktk cheti cha form na kuendelea
 
Cha kufanya nenda kabadili hilo Jina kweny Chet chakuzaliwa... watu wanabadili mpka siku za kuzaliwa so inawekna
 
Na je inaweza kuchukuwa mda sana kubadilishwa kwa sababu nafanya mtihani wa kidato cha sita kuanzia tarehe mbili mwezi ujao kwa sababu nahofia kwenye apply mkopo
 
Na je inaweza kuchukuwa mda sana kubadilishwa kwa sababu nafanya mtihani wa kidato cha sita kuanzia tarehe mbili mwezi ujao kwa sababu nahofia kwenye apply mkopo
badili cheti cha kuzaliwa, chukua upya ili upunguze mililongo mirefu
 
nilipata tatizo kama lako niliandikishwa shule kwa jina la ubatizo nilipofika high school nikaona tatizo nikamwona mwalimu akanielekeza inabidi jina langu la kuzaliwa na ubatizo yaunganishwe yaani Hassani-ally ili lionekane jina moja lakini wakati majina yanarudikwa ajili yakufanya mtihani wa form six lilirudi lile nililokuwa natumia laubatizo nilipomwona mwalimu wa academicakasema ningeonekana kama mtu mwingine ila kwa sababu yanahitajika majina matatu usiwe na hofu auta athirika wakati wa kuchukua passport au kufanya shuguri nyingine
 
Itabidi nikabadili jina tuu Kwa sababu nimeligundua mapema nitalishughulikia nadhani hadi ikifika kujaza bodi ya mikopo itakuwa tayari
 
Na je inaweza kuchukuwa mda sana kubadilishwa kwa sababu nafanya mtihani wa kidato cha sita kuanzia tarehe mbili mwezi ujao kwa sababu nahofia kwenye apply mkopo
Nenda katengeneze chet cha kuzaliwa gharama haizidi 15000/ ndani ya wik unakipata
 
Nawashukuru sana kwa msaada wenu kwa sababu hilo tatizo nimeligundua leo
 
Kwa anaye fahamu ofisi za RITA kwa Arusha zilipo naomba aniambie
 
Na je inaweza kuchukuwa mda sana kubadilishwa kwa sababu nafanya mtihani wa kidato cha sita kuanzia tarehe mbili mwezi ujao kwa sababu nahofia kwenye apply mkopo
Wahi kubadili vinginevyo bum utalishia kulisikiia!!!!
 
Back
Top Bottom