Mwaka 2009 , naenda nyumbani kwa baba mdogo ( ni nyumba ya baba mzazi wangu ambaye sasa ni marehemu na yeye baba mdogo pia ana share) nafukuzwa getini na kuitiwa polisi ya kwamba nasumbua, wakati nilikuwa na shida ya sh laki sita anisaidie baba mdogo ,mwanangu alikuwa mngojwa sana hakunisaidia na aliita polisi.
Sasa ni miezi imepita nyumba hiyo naimiliki kwa kuinunua toka kwake pamoja ns ofisi zake na magari yake, juzi kaja kaishia getini nilikuwa sipo nyumbani kaacha ujumbe anaumwa hanipati kwenye simu, anashida ya laki sita, leo nimemrushia sijarudisha ubaya lakini jamani Mungu mwache aitwe Mungu.
Haya maisha haya yanaweza badilika kwa sekunde, tumcheni Mungu.