Cheo cha Urais ni taasisi, Kwanini anyooshewe yeye tu kidole?

Urais ni taasisi huko duniani lkn hapa kwetu ni baba mwenye nyumba! kila kitu yeye!
 
USICHEZE NA TAASISI YA URAIS

Na Thadei Ole Mushi.

Kuna kitu watu hawajui, hasa Vijana!!!

Rais wa Nchi si Mtu Bali ni watu yaani Rais ni taasisi. Kazungukwa na wataalamu wote katika Sector zote.

Rais wa nchi kupitia taasisi yake ya Urais wanajua kila kitu kuhusu Raia wake yaani kila kitu. Wana taarifa zote Muhimu kwa kila Raia wa nchi hii.

Kila siku Rais anapokea taarifa muhimu kutoka pande zote za nchi kuhusu usalama wa nchi. Wanazichambua na kufanya maamuzi.

Nataka kusema nini.?

Serikali sio vichaa kumfukuza Balozi wa EU nchini. Kuna mambo mengi wameyaona kabla ya kumfukuza.

Na kidiplomasia kabla ya Kumfukuza mwakilishi wa nchi lazma watoe taarifa kwa nchi husika anakotokea huyo mwakilishi. Yaani kabla ya balozi wetu wa Uingereza hajarudishwa nchini kwa mfano lazma serikali ya Uingereza ifanye mazungumzo na serikali yetu na wakubaliane.

Kwangu mimi huu ni ujasiri mkubwa na uwezo mkubwa sana Serikali yetu imeonyesha. Kuthubutu kumkataa mwakilishi wa EU si jambo dogo na si nchi zote za Afrika zinauthubutu huu.

Kuna mambo mengi ambayo yanafanywa na Serikali na hayasemwi. Ila usicheze na Taasisi hii kabisa.

Narudia taasisi hii sio Mtu Bali ni team wana access na wewe sana kila taarifa yako wanayo. Mwecheni huyu balozi arudi kwao atakuja mwingine.... Serikali imejiridhisha na nchi yetu inabaki kuendelea kuwa Salama

Ole Mushi
0712702602
FB_IMG_1541223698094.jpeg
 
  • Thanks
Reactions: Oii
Kumbe amefukuzwa? Mbona nasikia aliitwa kujadili kuhusu mwenendo wa demokrasia na haki za binadamu huko Brussels?

Au ulikuwa wapi mkuu?Ulikuwa umetekwa au?
 
Hivi hii Habari ya Urais ni taasisi ilitoka wapi kwanini usiseme IKULU ndio taasisi ikiongozwa na Rais badala ya kuandika bango refu la vitu ambavyo havipo
 
USICHEZE NA TAASISI YA URAIS

Na Thadei Ole Mushi.

Kuna kitu watu hawajui, hasa Vijana!!!

Rais wa Nchi si Mtu Bali ni watu yaani Rais ni taasisi. Kazungukwa na wataalamu wote katika Sector zote.

Rais wa nchi kupitia taasisi yake ya Urais wanajua kila kitu kuhusu Raia wake yaani kila kitu. Wana taarifa zote Muhimu kwa kila Raia wa nchi hii.

Kila siku Rais anapokea taarifa muhimu kutoka pande zote za nchi kuhusu usalama wa nchi. Wanazichambua na kufanya maamuzi.

Nataka kusema nini.?

Serikali sio vichaa kumfukuza Balozi wa EU nchini. Kuna mambo mengi wameyaona kabla ya kumfukuza.

Na kidiplomasia kabla ya Kumfukuza mwakilishi wa nchi lazma watoe taarifa kwa nchi husika anakotokea huyo mwakilishi. Yaani kabla ya balozi wetu wa Uingereza hajarudishwa nchini kwa mfano lazma serikali ya Uingereza ifanye mazungumzo na serikali yetu na wakubaliane.

Kwangu mimi huu ni ujasiri mkubwa na uwezo mkubwa sana Serikali yetu imeonyesha. Kuthubutu kumkataa mwakilishi wa EU si jambo dogo na si nchi zote za Afrika zinauthubutu huu.

Kuna mambo mengi ambayo yanafanywa na Serikali na hayasemwi. Ila usicheze na Taasisi hii kabisa.

Narudia taasisi hii sio Mtu Bali ni team wana access na wewe sana kila taarifa yako wanayo. Mwecheni huyu balozi arudi kwao atakuja mwingine.... Serikali imejiridhisha na nchi yetu inabaki kuendelea kuwa Salama

Ole Mushi
0712702602View attachment 920000
All in All hatutaki Ushoga na Usagaji Nchini mwetu kama ni kufa njaa acha tufe! Wanao taka kufi.rwa wahamie Nchi ambazo wanatikwa!
Fatma Karume naye kawa Chizi! Eti kufi.rwa au kusagwa nako ni haki za binadamu!!
 
Katika utawala unaweza ukakasimu majukumu lakini kama kiongozi unabaki kuwajibika na matokeo ya utelekezaji wa majukumu yako yote yakiwemo yale yaliyokasimiwa. Uwajibikaji haukasimiki.
 
kwani fomu walichukua wangapi za kugombea nafasi hiyo?urais in taasisi ilikuwa zamani
 
Raisi ni jua, viongozi lowateua ni mwezi wananchi ni nyota.. Jua(raisi) asipotoa mwanga wake mwezi hauwezi kupata mwanga wa kuufanya uonekane kipindi cha usiku, vivyo basi mwezi nao usipo pata mwanga toka kwa mwezi nyota hazitoonekana sababu ya kiza.

Hitimisho:
Raisi(jua) ndo wakulaumiwa kukiwa na kiza kwa sababu hakutoa mwanga wake kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom