Chenge,Werema: Tume imedanganya kiasi kilichopo kwenye mchanga, wajivua lawama

And one of the Atorney General was Chenge, a selfish man, instead he became one of the cartels, the richest man in Tanzania within the poor. Using his position, colluding with anyone who wants to do business in Tanzania with intention of stealing from us. Advising how to steal from us without getting caught. Every case we fight we lose, he is on both side. Like the TEGETA escrow case he was paid billions, flaming the payment was for advising the company, at the same time he is our law maker, what about conflict of interest? The so called investors against the government he serve. He has inside information, he knows our weakness and he uses this information to sell us cheaply and make himself very rich indeed as if he is going to live for ever. Where he comes from tunzu, people are poor out of the poor, yet he stashed billions in foreign banks, yes the government knows all about it, but he is untouchable. He killed a woman, living young children without a mother, his purnishenent was a fine as if he killed a dog. He new this lady and the case was not investigated properly, that should have been murder and not accident. How can people be unfair? And this is the Leader in our parliament. Do we really have hope with leaders like him. No hope. Until someone come up and take on these cartels. I mean loot them out, our children and grandchildren will have no hope.
Ndo maana tulivunjika moyo katiba mpya ilivyozikwa na utawala mpya unasema sio kipaumbele chake. Binadamu wengi wakikuta system iko weak wanatake advantage na kufanya mambo ya ajabu kama wanyama. Kwa hili hata likipita tukubaliane kuwa mfumo wetu wa utawala lazima ubadilike, kuwe na kuwajibika na kuwajibishwa. Kwa hili ni udhaifu mkubwa wa mfumo wa uongozi wetu na kumuachia mtu mmoja madaraka makubwa kweli kweli na ikitokea mtu huyo ana matatizo yake basi ni majanga.
 
Nina uhakika Tume ya JPM ya Makinikia imemdanganya sana Rais na Watanzania. Nina ushahidi ufuatao:

1. Wamewaaminisha watanzania kuwa kwenye kila kontena moja tunapoteza 1 Trillion shilings badala ya 300m walizosema Acacia. Hapa wanacheza na akili zetu na za JPM kwa kutaja figure hiyo kubwa wakati wanajua wazi kuwa hayo makinikia hayakushuka kutoka mbinguni. Kuna mtaji wa awali ulitumika yaani capex, kuna gharama za uzalishaji yaani opex na za usafirishaji. Chetu ni 4% ya hiyo 1Trillion ambayo ni 4Billion tu. Ili kuleta mtikisiko wa bongo zetu wakaona waseme tunapoteza 1Trillion kwa kila kontena badala ya kusema 4Billion. Lengo lao ilikuwa nini?

2. Mfumo waliotumia kukokotoa thamani ya madini ni wa uongo, maana wame assume kuwa recovery ni 100% kitu ambacho hakiwezekani. Hata kiwanda cha sukari hakina recovery ya 100% kwenye miwa iweje madini! Kwa teknolojia ipi utapata hiyo kitu?

3. Sampling method waliyoitumia inatia mashaka, ndio maana taarifa yao haiwekwi wazi ili sisi wajuzi wa sampling tuwakosoe. Aidha Lab ya GST waliyoitumia haina ISO hivyo haikubaliki kimataifa. Utamuitaje mtu mwizi kwa lab results za GST? Watuambie lab ipi zaidi ya GST waliyotumia yenye ISO. Vinginevyo ni kudanganya umma na kuiweka nchi kwenye hatari ya kushitakiwa kimataifa.

4. Hawakujipa muda kuhoji unalali wa resuts zao. Walipaswa kujiuliza maswali yafuatayo na kujijibu, je kwa results hizi ni kweli kuwa Acacia ni mzalishaji namba moja wa dhahabu duniani? Kama ndio, kwa nini wanaficha ukweli huo kwani si ingewasaidia kuongeza hata bei ya share zao kwenye soko? Je haya madini ya ziada tuliyoyaona zaidi ya dhahabu, shaba na fedha wanayoripoti serikalini je yanaweza kuchambuliwa kwa gharama gani na faida ikawepo au haiwezekani? Je wao Acacia wanalipwa hayo madini kama sio kwa nini wanakubali kupoteza fedha hiyo? Je kama wanalipwa, hiyo fedha ya ziada inaingia kwenye akaunti gani ambayo sisi hatuijui na je inawezekana hata USA na Canada hawaijui? Je serikali kupitia TRA na TMAA wanavyokagua financiàl records za Acacia huwa hawayaoni hayo mafedha ya ziada? Je hizi findings zetu ziko in line na taarifa za explorations na Feasibility study za migodi hiyo au tumegundua kitu kipya? Nina uhakika wangejiuliza maswali hayo wangedrop hizo findings za uongo na kuokoa nchi kwenye aibu hii.

5. Tume hawakuchukua tahadhali kutoa conclusion hizo ambazo zinaituhumu Acacia kuwa ni wezi na watendaji ni wazembe. Hatari iliyopo ni impact yake kwenye jamii na kwa watuhumiwa. Ona sasa share za Acacia zimeporomoka na watendaji wamesimamishwa kazi na wanachunguzwa bila hata kusubiri ukweli halisi kujulikana. Hii ni pigo kubwa kwa watu hao. Ndio maana naunga mkono hoja ya serikali kuyanunua makontena hayo na kuyapeleka kwa marafiki zetu china kuyachakata ili tuone kama hayo madini aloyoyasema Prof Mruma yatapatikana. Yaani Tume itaumbuka mchana kweupe na serikali itapata hasara kwa kuaminishwa na hawa maprofesa waliopika data ili kupata vyeo.

Nashauri JPM awaite hao wajumbe wa tume wathibitishe mapema ukweli wa hizo data zao ili ikija kutokea tofauti wanyongwe. Ni maoni yangu, Msema Kweli Mpenzi wa Mungu.

Suala ni udanganyifu, hata yale makontena yaliyokamatwa serikali haijasema ni yake, Acacia wao wanadai katika kontena moja kuna kiasi kidogo cha dhahabu ili waweze kulipa kiasi kidogo cha mapato kwa serikali mbona hatulioni hili? Mfano katika makontena yote 277 kwa mujibu wa report yanathamani ya 1trillion ,pesa ya serikali ni 4* 1Trillion, hizi ni 40billions peza za kitanzania . Kumbuka wanasafirisha makontena kama yale kila mwezi, maana yake serikali inapoteza 480 billions , na wamekuwa wakifanya hivyo miaka 17, maana yake 480billions*17 hizi ni takribani trillions 8 za kitanzania, hizi ni pesa kidogo? hii ni pesa nyingi ambazo zinaweza badili nchi yetu kiichumu, jamani tusikatae jitihada zinazochukuliwa, wizi ni wizi Acacia wanatupiga.
 
CHENGE, WEREMA WAJIVUA LAWAMA

CHENGE-1-220x300.jpg

Na WAANDISHI WETU
Mtanzania

– DAR, DODOMA

WAKATI baadhi ya watu wa kada mbalimbali, wakiwamo wataalamu wa sheria wakisema mikataba mibovu katika sekta ya madini ni kiini cha serikali kupoteza mabilioni ya fedha kama ilivyoainishwa na Kamati ya Rais, waliopata kuwa wanasheria wakuu wa serikali, Andrew Chenge na Frederick Werema, wamelivua zigo hilo na kuzirushia mamlaka nyingine.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na MTANZANIA Jumamosi, mjini Dodoma na kwa njia ya simu, wanasheria hao wametoa kauli zinazofanana, zinazoonyesha kuwa hawahusiki katika uzembe unaosemwa sasa.

Siku tatu zilizopita Kamati ya kuchunguza kiwango cha madini kilicho katika mchanga (makinikia) unaosafirishwa nje ya nchi ilikabidhi ripoti yake, ambayo pamoja na mambo mengine, imeonyesha kuwapo kwa uzembe katika kudhibiti biashara hiyo.

Wakati Chenge na Werema wakiweka msimamo huo sasa, baadhi ya wanasheria, akiwamo Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa Issa Shivji, mapema wiki hii alindika kuwa; “Tulikosea njia tulipopitisha sheria ya madini ya mwaka 1998 iliyofanya mikataba iwe na nguvu zaidi kuliko sheria, tukajifunga pingu. Nani wa kumlaumu?”

Hoja kama hiyo pia imezungumzwa na Rais wa Chama cha Wanasheria (TLS), Tundu Lissu, ambaye amekuwa akihoji matatizo ya mikataba ya madini, miongoni mwake ikiwamo sheria ya madini ya mwaka 1998, ambayo serikali iliipeleka bungeni kwa hati ya dharura na ikapitishwa ndani ya siku moja.

Chenge alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) kuanzia mwaka 1993 mpaka 2005.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi kuwa alishuhudia mikataba yote mikubwa ya madini ambayo inalalamikiwa kwa sasa ambayo ilisainiwa kati ya mwaka 1994 mpaka 2007.

Wakati Chenge akiwa AG katika kipindi cha utiaji saini mikataba hiyo, chini ya serikali ya awamu ya tatu ya Rais Benjamin Mkapa 1995 – 2005, Jaji Frederick Werema alikuwa mtaalamu wa Sheria katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Jaji Werema alishika nafasi hiyo kati ya mwaka 1984 mpaka 2007 na baadaye kuja kuwa Mwanasheria Mkuu kati ya mwaka 2009 hadi 2014, akichukua nafasi ya Johnson Mwanyika, aliyestaafu kwa lazima.

Chenge

Alipotakiwa kuzungumzia kinachosemwa kwamba wakati akiwa AG, Serikali iliingia mikataba mibovu inayoigharimu Serikali kwa sasa, Chenge alisema: “Rais ameshatoa maoni yake, kuna marais mawili hapa? Nani alikwambia nilikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali? Mbona nyie wagonjwa gonjwa kidogo? Mnaonekana kuwa na ugonjwa.

“Unachotaka ni nini? Sina comment nawaambieni. Yawezekana ninyi hamkumbuki historia ya ripoti ya Bomani ambayo ilitoa mapendekezo ili Serikali ione uwezekano wa kufanya smelting (uchenjuaji) hapa nchini.

“Mtu akikukumbusha kwa jambo jema, atakwambia kwanini hamjafanya tangu kipindi kile, yawezekana mtu anasema requirement ya smelting ni gharama, au production haitoshelezi.

“Lakini, ukikaa kimya italeta maneno, maana madini hayo ni mali ya Watanzania, kwani wengine wanaamini tunaibiwa na wengine hawaamini. Wakizipiga zile hesabu na mimi ukaniambia ni trilioni, nakataa kwa sababu I know it, nadhani kuna mahesabu wameyakosea.”

Chenge alisema suala la madini lina mambo mengi ya kitaalamu na hata kushangaa ni kwanini kila mara amekuwa akinyooshewa kidole.

“Hili suala lina mambo mengi ya kitaalamu. Kwa hiyo, nasema uamuzi wa Serikali kuhusu madini ulikuwa ni huo tu, lakini ukiniambia nilikuwa mwanasheria mkuu, mhhh.

“Chenge anabeba mengi na huwa nawaambia Watanzania kwamba basi Chenge ana akili sana, maana watu wote wananisema mimi. Tulianza mambo ya petroli na Mwalimu, mimi nimesomeshwa mambo ya mikataba ya madini na petroli na watu hawajui, lakini mimi nayajua.

“Utakuta mtu anajidai anajua, mimi namwangalia tu kwa sababu wakati mwingine hajai kwenye kiganja changu. Sijui kuna tatizo gani, Watanzania wananisema mimi nina akili kuliko wote, lakini yote hayo unabeba, mtu mzima unabeba tu, you don’t over react.

“Kwa hiyo, nasema Rais ameamua kuwakumbusheni hayo mapendekezo ya Bomani, kwanini hamkwenda huko ili baadaye muulizane na kuona kama inawezekana au haiwezekani?” alisema Chenge.

Wakati Chenge akisema hayo, kumbukumbu zinaonesha kuwa, mikataba mikubwa ni Bulyanhulu, ambao ulisainiwa Agosti 5, 1994, Golden Pride ulioko Nzega Juni 25, 1997.

Mingine ni Geita Gold Mine uliopo Geita, ambao ulisainiwa Juni 24, 1999, North Mara uliopo Tarime (Juni 24, 1999), Tulawaka uliopo Biharamulo (Desemba 29, 2003), Buzwagi uliopo Kahama (Februari 17, 2007).

Werema

Kwa upande wake Werema, akizungumza kwa njia ya simu na MTANZANIA Jumamosi, alisema haoni kama kuna tatizo la kisheria katika mikataba ya madini, isipokuwa kuna watu ambao walikuwa hawafanyi kazi yao sawasawa.

Werema, ambaye alionyesha kushangazwa na watu wanaoilalamikia sheria ya madini ya mwaka 1998, baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa ripoti ya makontena yenye mchanga wa dhahabu yanayoonyesha kuwa na kiwango kikubwa cha madini tofauti na kinachotajwa na wawekezaji, aliyafananisha malalamiko hayo na mashtaka ambayo yanataka kudhoofisha hoja ya baadhi ya watumishi kutowajibika sawasawa.

“Suala la sheria mbovu za madini ni general accusation, sheria ya madini ipo na ilikuwa inafanyiwa marekebisho na wakati wangu ilifanyiwa marekebisho mara moja mwaka 2009, sasa anayetuhumu lazima aeleze msingi wa tuhuma zake ni nini? hii tunayoizungumzia hapa ni practice.

“Nadhani tatizo lililopo ni wataalamu ambao wanalipwa fedha nyingi kwa ajili ya kupima hayo madini yaliyopo katika makontena na walikuwa hawafanyi kazi sawa sawa na tulikuwa tunasema kila siku ni vizuri kila mtu afanye kazi yake kwa ufasaha,” alisema Werema.

Alisema vipimo vya michanga ya dhahabu vilikuwa vinapimwa na wataalamu na si wanasheria kama wanavyozungumza watu.

“Hili la mchanga ni kilio cha muda mrefu, lakini kwa hali ya kawaida tu lazima jamii ijue, mfano mimi ni mwanasheria, ukiniletea kontena la mchanga wa dhahabu hapo siwezi kujua kilichopo bila kumshirikisha mtaalamu, nadhani hilo ni funzo kwa sababu haya yaliyotokea ni tatizo la wataalamu,” alisema Werema.

Alisema kama vipimo vilivyotumiwa na kamati ni vile vile ambavyo vilikuwa vikitumiwa na wataalamu katika shughuli zao za kila siku, ni wazi kuna tatizo na wahusika watapaswa wafidie hasara.

Alisisitiza kuwa, sheria ya madini ilitungwa na kundi la wataalamu wa sheria nchini ambao walizunguka katika nchi za Afrika na Uingereza kuangalia sheria zinazohusu mambo hayo zinasemaje, ili nchi iweze kutengeneza sheria zake.

Alisema kuna haja ya watendaji kuwa makini na waangalifu wanapokuwa wanafanya kazi na wataalamu kuhusu masuala yanayohusu maslahi ya Taifa.

MTANZANIA Jumamosi pia limezungumza na mmoja wa maofisa wa ngazi za juu ambaye alipata kufanya kazi katika Wizara ya Nishati na Madini, ambaye hata hivyo ameikosoa Ripoti ya Kamati iliyoundwa na Rais Magufuli.

Ofisa huyo, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini kwa hoja kwamba kazi yake itaharibika, alisema kamati hiyo haikueleza ukweli juu ya usafirishwaji wa madini hayo pamoja na muda uliotumika kuanza kusafirisha mchanga huo kwenda nje ya nchi kwa ajili ya uchenjuaji.

“Kama utakumbuka, mwaka 2007, Tume ya Jaji Bomani iliundwa kwa ajili ya kuchunguza mikataba ya madini pamoja na sera ya sekta hiyo. Katika kufanya kazi tume hiyo, iliangalia sera na sheria na mwisho yakawasilishwa mapendekezo yake serikalini kwa utekelezaji.

“Mwaka 2008, mchakato ukaanza wa kubadili sera na mwaka 2009 sera hiyo ikapatikana na mwaka 2010, tukapata sheria mpya.

“Sera hiyo ilisema tuongeze thamani ya madini kwa kujenga smelting area kwa ajili ya kuchenjua mchanga hapa nchini na wakati huo huo, wawekezaji waelimishwe ili wajue namna ya kuomba leseni za uwekezaji huo na namna zitakavyotolewa.

“Kuhusu hoja ya ile kamati, kwamba tumekuwa tukiibiwa madini yetu kwa miaka mingi, kamati hiyo haiko sahihi, kwa sababu migodi inayotoa huo mchanga ni Buzwagi na Bulyanhulu.

“Mgodi wa Buzwagi walianza kusafirisha mchanga nje ya nchi mwaka 2008 na Bulyanhulu wao walianza mapema mwaka 2002 kama sikosei. Kwa hiyo, wanaposema tumeibiwa kwa miaka 19, sikubaliani nao,” alisema ofisa huyo.

Mwanzoni mwa wiki, moja ya kamati zilizoundwa na Rais Dk. Magufuli, iliwasilisha ripoti yake ya uchunguzi wa mchanga wa madini uliokuwa kwenye makontena yanayosafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya uchenjuaji.

Baada ya ripoti hiyo kuwasilishwa mbele ya Rais Dk. Magufuli, kiongozi huyo aliwachukulia hatua baadhi ya watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini walioonekana kushindwa kutimiza wajibu wao na kuisababishia hasara Serikali, kwa kuwa fedha nyingi zilikuwa zikipotea kupitia usafirishaji huo.
 
Suala ni udanganyifu, hata yale makontena yaliyokamatwa serikali haijasema ni yake, Acacia wao wanadai katika kontena moja kuna kiasi kidogo cha dhahabu ili waweze kulipa kiasi kidogo cha mapato kwa serikali mbona hatulioni hili? Mfano katika makontena yote 277 kwa mujibu wa report yanathamani ya 1trillion ,pesa ya serikali ni 4* 1Trillion, hizi ni 40billions peza za kitanzania . Kumbuka wanasafirisha makontena kama yale kila mwezi, maana yake serikali inapoteza 480 billions , na wamekuwa wakifanya hivyo miaka 17, maana yake 480billions*17 hizi ni takribani trillions 8 za kitanzania, hizi ni pesa kidogo? hii ni pesa nyingi ambazo zinaweza badili nchi yetu kiichumu, jamani tusikatae jitihada zinazochukuliwa, wizi ni wizi Acacia wanatupiga.
Si kwamba walikuwa hawalipi kabisa, la hasha hila inawezekana walikuwa wanadanganya na kulipa kidogo. Hila waliwezaje kudanganya na utathibitishaje uongo wa huko nyuma. Kumbuka kule mgodini kabla makenikia hayapakiwa kusafirishwa, wizara kupitia TMAA na ACACIA/SGS wote uchukua sampuli ili kujua kiwango kilichomo ili hiyo 4% ilipwe. Then hufungwa seal mbele ya wadau husika kwa safari ya Dar. Pia TRA ISAKA ucheki documents zote na kuwapa export permitts. Ina maana tumeshiriki wizi huo?, lakini je tuna hizo evidences za nyuma.
 
Shida ni mikataba inayowekwa kwa sheria ambazo zinapitishwa bungeni na wabunge walio wengi kwa hati ya dharula,kupitishwa kwa stahili hii kutatugharimu sana.

Mkataba wowote ni lazima uwe na kipengere cha kuvunja,huwa hakiwekwi 7bu sheria kuhusu mikataba hupitishwa kwa pupa,tena na watu wengi ambao wanamudu 3Ks.

Tufike wakati bunge litunge sheria lisiletewe sheria ili kuidhinisha.

Utaratibu wa wabunge kupewa bahasha ili wapitishe jambo fulani uachwe mara moja.
 
Wamefanya kosa 1990s na bado watafanya makosa kwenye gesi usishangae by 2030s watakuja kuongelea mikataba ya gesi hapa ambayo waliipitisha saa 5 za usiku.
 
Ikiwa rais ailidanganywa inaonyesha washauri wanamuogopa.....

Watanzania tuna ugonjwa wa woga. Mtu mmoja anakuwa na power ya kuwafunika Watanzania millions 50. Mkapa mpaka akajigawia migodi, tunamwangalia tu. Migodi ukamushinda akaubwaga kama vile Nchi ni Mali yake binafsi.
 
Bora hata chenge amejibu kihuni huni. Werema ndio hajui kitu kabisa au haelewi watu wanacholalamikia. Watu tunalalamikia mikataba mibovu ambayo inawapa wachimba madini haki nyingi za mgawanyo wa mapato yatokanayo na madini, yeye anaongelea content ya dhahabu kwenye mchanga.

Yeye werema haoni shida kwenye mkataba yeye anaona kwenye content ya dhahabu kwenye mchanga, what if kama content ikawa sawa na jinsi wataalam walivyoona, maana yake kwake hakuna shida tena.

Mkurugenzi wa Acacia mwenyewe amekiri kua mikataba haikua sawa iliwapendelea sana wawekezaji alafu yeye anaona hakuna shida.
20170527_180057.png

Acacia boss Brad Gordon: The mining industry can be its own worst enemy
 
View attachment 515311
Acacia boss Brad Gordon: The mining industry can be its own worst enemy

Mtu akishiba hamuoni mwenye njaa. HUYU bwana ameshiba, Rais aangalie utajiri wake asiuhamishe kwa ndugu na jamaa. Hakuna wa Afadhari wezi wezi tu.
 
Abdulkarim Hamisi Mruma Ph.D., FCA, M.Sc. (Geology), B.Sc. (Geology)
Advisor of Tanzanian Geology,Ruby Creek Resources, Inc.

Background*
Dr. Abdulkarim Hamisi Mruma, Ph.D., FCA, M.Sc. (Geology), B.Sc. (Geology), serves as an Advisor of Tanzanian Geology at Ruby Creek Resources, Inc. Dr. Mruma serves as Chief Executive Officer of the Geological Survey of Tanzania, Ministry of Energy and Minerals. He serves as Professor of Geology of University of Dares Salaam. He has been Vice Chairman of the Association of Geological Survey of Africa since 2004. He served as Head of the Department of Geology at the University of Dares Salaam from 1994 to 2004. Other positions he held include: National Coordinator, International Geological Correlation Programs; External Examiner, Department of Geology of the University of Nairobi in Kenya and the University of Makerere in Uganda. He serves as Board Member of Williamson Diamonds Limited, Diamond Mine at Mwadui. He served as Director of Tanzanian Royalty Exploration Corp. (formerly, Tan Range Exploration Corp.) from January 01, 2011 to February 2016. He served as a Director of Douglas Lake Minerals Inc., from August 4, 2008 to July 3, 2009. He serves as a Member of Technical Committee at Douglas Lake Minerals Inc. He has published over thirty international publications, mainly in the fields of structural geology, precambrian geology, stratigraphy and mineral deposits. He has consulted on and authored more than twenty technical reports in the fields of resource Assessments and engineering geology. He is a Member of the Geological Society of Africa and the Tanzania Geological Society. He is a graduate of the University of Dar-es Salaam.

Mwenyekiti wa Tume ya makenikia
 
Chenge atasema hajaenda Havard University.
 
Muhongo alipotumbuliwa,wapuuz wasiojua mambo walishangilia sana hawakujua tatizo ni mkataba ambao Serikali ya Ccm ilikurupuka kama kawaida yao,na Muhongo alikuwa kama msimamiz wa Mkataba huo hivyo hakuwa na mamlaka ya kuutengua,yetu macho na masikio ni mengi tutayashuhudia nyuma ya pazia
 
Muhongo, Sospeter, Prof.
Fellow of AAS since (2006), (Field) Geology/ Earth Sciences
Born in 1954, Tanzania

Prof Sospeter Muhongo, a distinguished scholar, is the Minister of Energy and Minerals of the United Republic of Tanzania and a Nominated Member of Parliament.

He is, “Officier, Ordre des Palmes Académiques”, an Honorary Fellow of the Geological Society of America (HonFGSA), an Honorary Fellow of the Geological Society of London (HonFGS), an Honorary Research Fellow of the Chinese Academy of Geological Sciences (HonFCAGS), a Fellow of the Academy of Sciences for the Developing World (FTWAS), a Fellow of the Geological Society of Africa (FGSAf), a Fellow of the African Academy of Sciences (FAAS) and a Fellow of the Tanzania Academy of Sciences (FTAAS).

He is the first recipient (2004) of the Prof Robert Shackleton (UK) Award for Outstanding Research on the Precambrian Geology of Africa. He is the Vice President of the Commission of the Geological Map of the World (CGMW). He is a Full Professor of Geology at the University of Dar Es Salaam, Tanzania and an Honorary Professor of Geology at the University of Pretoria, South Africa. Prof Muhongo was the Chair of the Jury for the African Union (AU) Kwame Nkrumah Scientific Awards – Continental Awards for Outstanding Scientists 2011 Edition.

He is a member of the Executive Board of the African Inter-Parliamentary Forum on Science, Technology and Innovation (AIPF-STI). He is effectively involved in various high-level regional (Africa) and global STI strategic policy processes (e.g. Africa-Europe STI partnerships). He is a Member of the International Experts Group (Global Science Forum) of OECD and has occupied numerous important national, regional and international professional positions dealing with STI, earth resources, science policy and science diplomacy. Prof Muhongo was nominated by his country to be a candidate (2009) for the post of the Director General of UNESCO.

He is Editor-in-Chief of the Journal of African Earth Sciences (Elsevier), Associate Editor of Precambrian Research (Elsevier) and a member of several editorial boards of science journals and bulletins. He is the Senior Editor of the published book (2009) on, “Science, Technology and Innovation for Socio-Economic Development: Success Stories from Africa.”

Prof Muhongo has published over 200 research papers in international journals of high impact factors. He has co-authored widely used geological and mineral maps of Africa, East Africa and Tanzania. He has delivered more than 300 invited keynote speeches around the world at international conferences. He has undertaken over 100 contracted scientific research projects, and consultancy services in the mineral industry, environmental issues and STI policy matters.

Over the past two decades, Prof Muhongo has co-organized over 100 expert group meetings and international earth sciences, STI and science policy conferences, including those on “Science with Africa (Rapporteur-General)” which are hosted by the United Nations Economic Commission for Africa (UNECA), the African Union Commission (AUC) and their partners. Prof Muhongo has developed a special interest in the application of STI for sustainable growth and socio-economic development of the global society.

- See more at: AAS Fellows in Tanzania
 
With all these qualifications what does have have to show? That is why I believe having PHD is not necessary you can produce wonders. There is more to education than being a professor.
 
Hili tambala la Mbowe linaloitwa Tanzania daima baada ya kuhujumu Vita ya dawa za kulevya sasa wanataka wahujumu tena Vita zidi ya kuibiwa madini watanzania !!!!
Serikali ya Ccm ndiyo inahujumu Wananchi wake na si Gazet la Mbowe,kwa akili yako Gazeti la Mbowe ndilo liliingia mkataba na Wawekezaji!
 
Back
Top Bottom