Chenge,Werema: Tume imedanganya kiasi kilichopo kwenye mchanga, wajivua lawama

-KUPUNGUZA KIKI-
Ndo kunakucha sasa, tutasikia mengi sana. Na kama ndio hivyo mkulu bado ana safari ndefu sana ya kujifunza kuwa na subira, kusikiliza washauri wake na kutumia hekima na busara pia kupunguza kiki.
 
With all these qualifications what does have have to show? That is why I believe having PHD is not necessary you can produce wonders. There is more to education than being a professor.
Unweza kubahatisha mara moja lakini siyo mara nyingi
 
Si kwamba walikuwa hawalipi kabisa, la hasha hila inawezekana walikuwa wanadanganya na kulipa kidogo. Hila waliwezaje kudanganya na utathibitishaje uongo wa huko nyuma. Kumbuka kule mgodini kabla makenikia hayapakiwa kusafirishwa, wizara kupitia TMAA na ACACIA/SGS wote uchukua sampuli ili kujua kiwango kilichomo ili hiyo 4% ilipwe. Then hufungwa seal mbele ya wadau husika kwa safari ya Dar. Pia TRA ISAKA ucheki documents zote na kuwapa export permitts. Ina maana tumeshiriki wizi huo?, lakini je tuna hizo evidences za nyuma.

Evidence zipo ndugu yangu, hizo container 277 ni moja ya evidence, maana hao Acacia watakuwa wali declare kiasi cha madini yaliyomo ndani ya containers hizo, hizo exports /clearance documents zote zinaonyesha walikuwa wanasafirisha mzigo kiasi gani na wenye thamani kiasi gani, hiyo walichokuwa wana declare ni tofauti na report ya watalaam wetu, hili ni kosa . Hizi SGS/TMAA hununulika ,tusisahau hilo,ndo maana serikali imechukua hatua kwa watumishi wake wa public sector wakiwemo TMAA/na wizara ya nishati kwa ujumla kwa uzembe huo. Kwa upande wa Acacia kuchukua hatua inatakiwa tusubri kwanza evidence zote zikamilike, kama Acacia ataona hakubali na report ile basi tunaweza chukua samples zile tukarudia upimaji, kama Acacia anaonewa achukue sampe atume UK/Australia wherever na sisi tutatuma samples zile nje ya nchi lakini hatutamwambia Acacia sample zetu ziko nchi gani, halafu tulete matokeo ya sample tulinganishe, aliye violate contact/contract breach achukuliwe hatua. Uhakika ni mkubwa kuwa Acacia wanatupiga, tena sana.
 
Walioandaa ile ripoti wameifanya biashara ya kimataifa ya madini ni kama kuchukua viazi mviringo Mbeya na kuuza soko la Kariakoo.

Biashara ya madini kwa makampuni makubwa ambayo ni public, unaweza kupata taarifa zake zote za uzalishaji na uuzaji. Hawawezi kuiba kwa kudanganya uzalishaji. Kama kuna maeneo ambayo wanaweza kuiba ni kwenye mahesabu ya fedha lakini siyo kwenye uzalishaji.

Ripoti ile ya kamati ni upuuzi mtupu ambayo inaifanya nchi na wataalam wa Tanzania wadharaulike. Ripoti kama ile kuandaliwa na maprofesa, kunaleta maswali mengi kama kweli tuna maprofesa halisi au tuna maprofesa kwa sababu chuo kikuu ni lazima kiwe na maprofesa.

Kwanza inaonekana maprofesa wale hawana uelewa wowote kuhusu Dunia ya uchimbaji madini. Wangekuwa hata na uelewa wa jumla tu wa uzalishaji wa madini, wangeyakataa majibu ya maabara hiyo ya Dodoma na wangeomba analysis irudiwe.

Ile ripoti ni sawa na mtaalam wa kilimo kuandaa ripoti ya wizi wa mazao ya mahindi kwenye ekari moja, halafu akahitimisha kwa kusema mahindi yaliyoibiwa katika eka hiyo ni magunia 1000 yenye thamani ya shilingi milioni 10. Itakuwa ni record ambayo haijawahi kutokea kwa ekari moja kutoa magunia 1000.

Ile ripoti ni aibu ya karne kwa maprofea wa Tanzania lakini na sisi tunaoshabikia, tunadharaulika na wanaofahamu.

Busara ni Rais kuteua kamati ya siri ifanye kazi hiyo upya. Kazi hiyo ikifanywa na watu huru kama ACACIA ilivyoomba aibu yetu itakuwa ni kubwa mno. Itaonekana sisi sote hatujui chochote kuhusiana na madini.
 
Jamani nisameheni, naombeni kujua professional ya change,

Tafiti hupingwa Kwa Tafiti sasa yeye kafanya tafiti gani hadi aje apinge hiyo tafiti? Naona Kuna watu wanamsapot chenge duuh watanzania wengine sijui vichwani mwao kuna vitu gan
mwanasheria aliyepata elimu yake chuo kikuu cha harvard marekani
 
Chenge alipotakiwa kuzungumzia kinachosemwa kwamba wakati akiwa Mwanasheria mkuu wa serikali, serikali iliingia mikataba mibovu inayoigharimu serikali kwa sasa, Chenge alisema

''Rais ameshatoa maoni yake , kuna marais wawili hapa?, Nani alikwambia nilikua mwanasheria mkuu wa serikali? Mbona nyie wagonjwa gonjwa kidogo? Mnaonekana kuwa na ugonjwa.

''Unachotaka ni nini? Sina comment nawaambieni. Yawezekana nyinyi hamkumbuki historia ya ripotinya bomani ambayo ilitoa mapendekezo ili serikali ione uwezekano wa kufanya smelting (uchenjuaji) hapa nchini.

''Mtu akikukumbusha kwa jambo jema, atakwambia kwa nini hamjafanya tangia kipindi kile, yawezekana mtu anasema requirement ya smelting ni gharama au production haitoshelezi.

Lakini ukikaa kimya italeta maneno, maana madini hayo ni mali ya watanzania, kwani wengine wanaamini tunaibiwa wengine hawaamini. Wakizipiga zile hesabu na mimi ukaniambia ni trilioni nakataa kwa sababu i know it ...lakini nadhani kuna mahesabu wameyakosea ''

Chenge amesema suala la madini lina mambo mengi ya kitaalamu na hata kushangaa nikwa nini kila mara amekuwa akinyooshewa kidole
''Hili swala lina mambo mengi ya kitaalamu .

Kwa hiyo nasema uamuzi wa serikali kuhusu madini ulikuwa ni huo tu, lakini ukiniambia nilikuwa mwanasheria mkuu mhh
''Chenge anabeba mengi na huwa nawaambia Watanzania kwamba basi Chenge ana akili sana, maana watu wote wananisema mimi.Tulianza mambo ya petroli na Mwalimu, mimi nimesomeshwa mambo ya mikataba ya mdini na petroli na watu hawajui lakini mimi nayajua''

Utakuta mtu anajidai anajua mimi namwangalia tu kwa sababu wakati mwigine hajai kwenye kiganja changu. Sijui kuna tatizo gani Watanzania wananisema mimi nina akilikuliko wote, lakini yote hayo unabeba, mtu mzima unabaeba tu, you don't over react

Kwa hiyo nasema Rais ameamua kuwakumbusheni hayomapendekezo ya Bomani, kwa nini hamkwenda huko ili baadae muulizane na kuona kama inawezekana au haiwezekani?''
Alisema Chenge

View attachment 515066 View attachment 515065
Hakuna sehemu ambapo Chenge amesema Raisi amedanganywa na Tume bali amesema yeye alitekeleza kazi yake kama kawaida na wataalamu walitakiwa kutekeleza wajibu wao wa kusimamia wajibu wao wa kusimamia makinikia hayabebi dhahabu zetu
 
Rais kakurupuka au wewe ndo unakurupuka?
Rais ndo katoa report au tume?
Tume iliyoundwa haikuwa na uwezo wa kupata taarifa sahihi?

Rais ana tofauti gani na wale wanaoua vibaka kwa kusikia kelele za "mwizi........mwizi....... mwizi...." pasipo hata kujua ameiba nini na kwa nani unaokota jiwe na kupiga mtu......

Huko ni kukurupuka kwa kiwango kibaya na cha kutisha...

Kwani asingetuliza akili na kujipa muda kidogo na yeye kusoma hiyo ripoti akajiridhisha kwamba kilichoripotiwa na aliowatuma ni sahihi na hakuna exaggeration yoyote ?

After all tunaambiwa kuwa kuna kamati zingine hazijampa ripoti, sasa sijui kilikuwa na haraka gani kuanza kuita watu wezi, wakwepa kodi hata.....???
 
Lakini ukikaa kimya italeta maneno, maana madini hayo ni mali ya watanzania, kwani wengine wanaamini tunaibiwa wengine hawaamini. Wakizipiga zile hesabu na mimi ukaniambia ni trilioni nakataa kwa sababu i know it ...lakini nadhani kuna mahesabu wameyakosea ''


I do not believe kama ni mali ya watanzania, ni mali ya joka la makengeza na genge lake na ndiyo maana anashupalia kuwaambia watanzania hawajui kiwango cha madini kilichomo
 
KAKURUPUKA kwa mara nyingine tena! Lini atajifunza huyu ili aachane na kukurupuka!?
Kama preaidaa alituaminisha tuangalie kipindi cha shilawadu kwa lengo la kumlinda bashite sishangai hili la mchanga. Posibility ya taarifa kupikwa ni kubwa sana
 
Rais ana tofauti gani na wale wanaoua vibaka kwa kusikia kelele za "mwizi........mwizi....... mwizi...." pasipo hata kujua ameiba nini na kwa nani unaokota jiwe na kupiga mtu......

Huko ni kukurupuka kwa kiwango kibaya na cha kutisha...

Kwani asingetuliza akili na kujipa muda kidogo na yeye kusoma hiyo ripoti akajiridhisha kwamba kilichoripotiwa na aliowatuma ni sahihi na hakuna exaggeration yoyote ?

After all tunaambiwa kuwa kuna kamati zingine hazijampa ripoti, sasa sijui kilikuwa na haraka gani kuanza kuita watu wezi, wakwepa kodi hata.....???
Do you even know who you are?
Jitafakari ndio uone kama umeandika sawasawa achilia mbali uhuru wa kujieleza
 
Tusahau kuwa uchumi wa viwanda. Hat a wawekezaji wameshatusoma kuwa Tanzania siyo pa kuwekeza miradi ya high finance. Mimi nilionas hili tangu Barrick walipoamua kutenganisha miradi Yao yaliyo Tanzania n.a. kuyaundia Barrick Africa n.a. baadae Acacia. Hawakuta share ya Barrick ziwe zinaporomoka kutokana n.a. maamuzi ya serikali ya tanzania. Kama wangekuwa hawajafanya hivyo, ungekuta Leo share za Barrick zimeathiriwa. Kuna wakati hata walitaka wawauzie China miradi yao ya tanzania. Sitashangaa wakiamua kuirudia hiyo azma
 
Tusahau kuwa uchumi wa viwanda. Hat a wawekezaji wameshatusoma kuwa Tanzania siyo pa kuwekeza miradi ya high finance. Mimi nilionas hili tangu Barrick walipoamua kutenganisha miradi Yao yaliyo Tanzania n.a. kuyaundia Barrick Africa n.a. baadae Acacia. Hawakuta share ya Barrick ziwe zinaporomoka kutokana n.a. maamuzi ya serikali ya tanzania. Kama wangekuwa hawajafanya hivyo, ungekuta Leo share za Barrick zimeathiriwa. Kuna wakati hata walitaka wawauzie China miradi yao ya tanzania. Sitashangaa wakiamua kuirudia hiyo azma

Kwa hiyo wewe unaona sawa mtu akiija kuwekeza Tanzania kwa faida yake mwenyewe. Anachukuwa madini yetu miaka yote anadeclare hasara lakini kuondoka haondoki. Hata kama sisi wajinga wa aina gani, unaona share zake zinapanda, huku watoto wetu hawana hata viti vya kukalia, faida gani hiyo? Haisemwi tu, hii migodi imeleta madhara badala ya faida kwa Wananchi. Unajuwa ya kuwa walikuwa hata wanaoperate migodi yao kupata maximum profit hawangalii hata maisha ya wananchi wanaoishi kwenye karibu na migodi hii. Watanzania wengi wamepata cancer za kuhusiana na chemical zinazotoka kwenye migodi hii. Kwa kuwa wengi wao ni masikini hawana sauti ya kupaza kwenye mitandao, sisi tunaona ni sawa tu. Afrika ni masikini na maisha yetu ni duni Pamoja na kuwa na madini. Faida yake ni nini basi, wafunge firago waondoke kuliko kutufanya sisi mabwege. Share zao zikitelemuka, ama zikipanda zinakusaidia nini wewe, na mchanga wanaiba? Congo leo ingekuwa nchi tajiri sana wangempata kiongozi bora, aangalia Kabila vile ameichezea nchi kama Mali yake binafsi. Shida ni Viongozi wetu mikataba mibovu, nashindwa hata kuwaita Viongozi.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom