Chenge,Werema: Tume imedanganya kiasi kilichopo kwenye mchanga, wajivua lawama

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,884
Chenge alipotakiwa kuzungumzia kinachosemwa kwamba wakati akiwa Mwanasheria mkuu wa serikali, serikali iliingia mikataba mibovu inayoigharimu serikali kwa sasa, Chenge alisema

''Rais ameshatoa maoni yake , kuna marais wawili hapa?, Nani alikwambia nilikua mwanasheria mkuu wa serikali? Mbona nyie wagonjwa gonjwa kidogo? Mnaonekana kuwa na ugonjwa.

''Unachotaka ni nini? Sina comment nawaambieni. Yawezekana nyinyi hamkumbuki historia ya ripotinya bomani ambayo ilitoa mapendekezo ili serikali ione uwezekano wa kufanya smelting (uchenjuaji) hapa nchini.

''Mtu akikukumbusha kwa jambo jema, atakwambia kwa nini hamjafanya tangia kipindi kile, yawezekana mtu anasema requirement ya smelting ni gharama au production haitoshelezi.

Lakini ukikaa kimya italeta maneno, maana madini hayo ni mali ya watanzania, kwani wengine wanaamini tunaibiwa wengine hawaamini. Wakizipiga zile hesabu na mimi ukaniambia ni trilioni nakataa kwa sababu i know it ...lakini nadhani kuna mahesabu wameyakosea ''

Chenge amesema suala la madini lina mambo mengi ya kitaalamu na hata kushangaa nikwa nini kila mara amekuwa akinyooshewa kidole
''Hili swala lina mambo mengi ya kitaalamu .

Kwa hiyo nasema uamuzi wa serikali kuhusu madini ulikuwa ni huo tu, lakini ukiniambia nilikuwa mwanasheria mkuu mhh
''Chenge anabeba mengi na huwa nawaambia Watanzania kwamba basi Chenge ana akili sana, maana watu wote wananisema mimi.Tulianza mambo ya petroli na Mwalimu, mimi nimesomeshwa mambo ya mikataba ya mdini na petroli na watu hawajui lakini mimi nayajua''

Utakuta mtu anajidai anajua mimi namwangalia tu kwa sababu wakati mwigine hajai kwenye kiganja changu. Sijui kuna tatizo gani Watanzania wananisema mimi nina akilikuliko wote, lakini yote hayo unabeba, mtu mzima unabaeba tu, you don't over react

Kwa hiyo nasema Rais ameamua kuwakumbusheni hayomapendekezo ya Bomani, kwa nini hamkwenda huko ili baadae muulizane na kuona kama inawezekana au haiwezekani?''
Alisema Chenge

New-Doc-2017-05-27_21.jpg
New-Doc-2017-05-27_11.jpg
 
image.png
View attachment 515111 Haya mambo ni kuyatazama kwa umakini sana.Wazungu huwa hawaibi "kijingajinga",wanaiba kwa umakini sana,tena wanakuibia kwa wizi wa "kisheria" ulioupitisha mwenyewe bungeni.

Unaposema mikataba ya madini yote,basi unamzungumzia Andrew Chenge na Mzee Mwakalukwa!!Hawa lazima maoni yao uwe makini nayo sana,maana wamekula sana 10% za hawa wawekezaji wakati wa kuandaa na ku-sign mikataba hii.

1998,wakati bunge la kina JPM,Chenge,Mkapa na JK wakipitisha sheria za madini kwa hati ya dharura,Tundu Lissu alikuwa "korokoroni" kwa kuipinga miswaada hiyo,CCM walipitisha mikataba hii kwa uwingi wao na kura za "NDIOOOOOOO"

Hivi mdivyo walivyofanya kwenye mikataba ya mafuta na gesi...Mpaka leo licha ya kuuwa watu na kupeleka jeshi Mtwara,hakuna lolote la maana kuhusiana na gesi.

Hii ni "Political Milage" ya kina Polepole na team yao,lakini itakumbana na upinzani wa ndani ya mfumo na chama.Huwezi laumu wizi wa madini bila kumkamata Chenge,Mkapa na Yona.Lissu aliwaambia miaka na miaka wakafumba macho

Mzungu sio mjinga kiasi hiki...Licha ya Chief Mangungo kutojua kusoma wala kuandika,bado Wajerumani chini ya Carl Peters walimsainisha "mkataba" wa kuuza himaya yake...ili waichukue "kwa uhalali wa mkataba"...Kama 1880's Mzungu alituibia kwa "mkataba",unafikiri leo ataiba "kijingajinga"??

Mikataba hii itawasomba kina Mwandosya enzi akiwa Katibu Mkuu Nishati,kina Chenge kama wanasheria na wasimamiaji wa mikataba...Kama ni wizi,basi hawa CCM na kina Polepole wawe wakwanza kuanza kufumua toka ndani ya chama chao...Vinginevyo ni yaleyale ya kutujaza hasira ili wapate ahueni ya kisiasa!!Tutafakari kwa pamoja!!!
 
Jamani nisameheni, naombeni kujua professional ya change,

Tafiti hupingwa Kwa Tafiti sasa yeye kafanya tafiti gani hadi aje apinge hiyo tafiti? Naona Kuna watu wanamsapot chenge duuh watanzania wengine sijui vichwani mwao kuna vitu gan
 
Back
Top Bottom