Namjua Andrew John Chenge vya kutosha. Ingawa sikumkuta pale UDSM, nilimkuta chamani CCM tangu katikati ya 1980's nilipojiunga na CCM na kuendelea kuwa naye hadi leo. Kaka yangu Chenge nimewahi kufa nya naye kazi mbalimbali za kisheria wakati huo nikiwa Serikalini, yeye akiwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Hata kazi za kichama, tuliwahi mara kadhaa kufanya kazi pamoja ili kufanikisha hili au lile. Kwa nimjuavyo, Chenge ni mtu wa kawaida. Ni muoga kama wengi wetu. Hachelewi kujaa mashaka juu ya hatua za kisheria na kinidhamu juu yake na kadhalika. Chenge hana ushupavu, uhodari, usmart wala uthubutu anaopewa kwenye media.
Kwa Serikali, Chenge ni mdogo kama chembe ya haradari. Chenge, kama alivyo Lowassa na Rostam ni wazito midomoni lakini wepesi kisiasa, kisheria na kimaisha. Chenge anadekezwa na kupewa upenyo tu. Nitawapa mfano mdogo. Katika mambo anayohusishwa nayo ya makinikia, Chenge anayatoka kirahisi kwakuwa kuna upenyo.
Mambo yanayomhusisha ni mambo yaliyotokana na Uanasheria wake Mkuu wa Serikali. Alikuwa Mshauri. Alikuwa akitoa ushauri juu ya mambo hayo ya madini. Hivi, ushauri ni jambo la lazima kukubaliwa? Hivi, aliyeshauriwa hakuwa katika nafasi ya kukataa? Huu ndiyo upenyo ninaousema. Kwanini yasingetafutwa mambo direct yaliyomhusu na kumhusisha nayo?
Amini nawaambia, Chenge ni mwepesi kama unyoya. Mbele ya Serikali, na vyombo vyake, hakuna mbishi,jasiri wala smart. Lakini, Chenge anadekezwa, anabebwa na anatengenezewa upenyo kila mara anapotajwa kwenye kashfa za kifisadi. Hana upekee wowote wala si nyoka kama anavyotamba kila mara.
Bastola ya nini tena jamani!?
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam