Wasegesege
Senior Member
- Oct 22, 2009
- 107
- 10
Wakuu nimepata tetesi kutoka e-group moja kwamba Chenge amhukumiwa miaka mitatu jela au faini ya 700,000 pesa ya tanzania (which is less that $500)
Je ni kweli? na kama ni kweli hii ina maana gani kwake kama Mbunge na watu wa bariadi?
Is the hukumu fair?
Acid
Hebu jamani watu ambao ni wataalamu wa Sheria wanisaidie hapa. Mhe. Chenge ameonekana ana hatia na kahukumiwa kifungo cha Miaka mitatu (3) au kulipa faini ya Tshs laki saba [700,000/-] kwa TAFSIRI YANGU ANAITUMIKIA MIAKA 3 KWA KULIPA FAINI YA TSHS 700,000
Sasa hoja yangu:
kwa mujibu wa Ibara ya 67.-(2) (c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kama ilivyorekebishwa mwaka 2005 kinasema nanukuu:
"(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu;"
mwisho wa nukuu.
Sasa Mhe. Chenge amehukumiwa kifungo cha Miaka 3 na badala yake amelipa faini, yaani Hakimu kasema unakwenda Miaka 3 jela ama ulipe faini, kwa maana hiyo iwapo angekosa kuwa na fedha Tshs, 700,000 angekwenda gerezani kutumikia adhabu ya miaka 3.
Sasa wanasheria na wataalamu wa Katiba hapa mnasemaje Chenge bado ni Mbunge halali wa Bariadi? au siyo Mbunge halali?
Hebu tusaidieni hapo.
Duuh.......ok lakini nathani sheria ndio imesema. Mana trafick kesi ndio zilivyo (fine/ kifungo)
Adhabu nyingine haza lengo la kumkomesha mshtakiwa.
Kwanini asingepewa adhabu ya kulipa bilioni saba ili aende jela?
This country bwana!!!!!
Maajabu makubwa ya nchi yetu DanganyikaThese are the two major WONDERS OF THE LAW
1. It justfy its existance by honouring lies I.e you must lie or cheat to escape. Maana yake kama umeua inabidi usema sikuua na uking'ang'anizwa sema sikukusudia. Utaadhibiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia.
2. It always goes contrary to the majority expectation. Wengi walidhani mzee wa vijisenti ataenda jela kwa kuua lakini la! Na wengi walidhani Liyumba atapigwa faini lakini kaishia jela.
Hiyo ndiyo katiba yetu ukiua faini, ukibaka kifungo cha maisha na kutumia madaraka vibaya na kuisababishia serikali hasara unafungwa jela.
Nakubaliana na wewe kwa mjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 67 kifungu cha pili (c) kama ninavyofukuu hapa 67.-(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-Bariadi wana mbunge batili!
Nakubaliana na wewe kwa mjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 67 kifungu cha pili (c) kama ninavyofukuu hapa "67.-(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) Ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au".
Nakubaliana na wewe kwa mjibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ibara ya 67 kifungu cha pili (c) kama ninavyofukuu hapa 67.-(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) Ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu; au.