Chenge alipuliwa upyaa...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge alipuliwa upyaa...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Mar 22, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  Wakati uchunguzi dhidi yake kuhusiana na tuhuma za kuhusishwa na rushwa itokanayo na manunuzi ya rada ya bei mbaya wakati akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ukiendelea, Mbunge wa Bariadi Mashariki, Bw. Andrew Chenge amejikuta akilipuliwa tena upya.

  Mheshimiwa Chenge ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa Serikali ya awamu ya tatu iliyokuwa ikiongozwa na Rais Benjamin Mkapa, hivi sasa anadaiwa kuwa ndiye aliyeshiriki kuianzisha kampuni inayodaiwa kuwa ya kifisadi ya Meremeta Gold.

  Aliyemlipua Mheshimiwa Chenge, ni Mbunge wa Jimbo la Karatu ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa.

  Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Dk. Slaa amedai kuwa Chenge ndiye aliyeisajili kampuni inayokabiliwa na tuhuma za kifisadi ya Meremeta Gold.

  Akadai kuwa Chenge, akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alishiriki kuianzisha kampuni hiyo ya Meremeta, kwa kwenda kuisajili katika kisiwa kilekile cha New Jersey nchini Uingereza, ambacho anadaiwa vilevile kuwa ndiko alikoficha mapesa anayotuhumiwa kuyapata kupitia dili la rada yanayofikia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja. Hata hivyo, Chenge aliwahi kuziita pesa hizo kuwa ni vijisenti.

  Katika madai hayo mapya yaliyotolewa na Dk. Slaa, ni kwamba licha ya kuwa mwanzilishi, Chenge ndiye Mkurugenzi wa kwanza wa Kampuni hilo la Meremeta, linalodaiwa kuitia losi Serikali ya Tanzania ya zaidi ya shilingi bilioni 155.

  Dk. Slaa amesema sasa, yeye na wenzie CHADEMA ambao wako kwenye `Operesheni Sangara` mkoani Kilimanjaro, wanaitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuichunguza Meremeta na kuwachukulia hatua za kisheria Chenge na wale wote wanaotuhumiwa kujihusisha na kampuni hiyo iliyowezesha kuchotwa isivyo halali kwa fedha za walipakodi wa Tanzania.

  Aidha, Dk. Slaa akasema kuwa yeye na wenzie wanafahamu kuwa tayari Rais Kikwete alishaunda Kamati ya Bomani kuchunguza sakata hilo, na kwamba kamati hiyo imeshawasilisha ripoti yake kuhusiana na suala hilo, hivyo kinachotakiwa ni kuchukuliwa kwa hatua zilizopendekezwa.

  ``Rais Kikwete aliunda Kamati ya Bomani kuchunguza. Kamati hiyo nayo ikatumia Shilingi Bilioni 1.5 kufuatilia suala hilo na mengine.

  Mwishowe ikaja na sentensi moja tu, kwamba Meremeta ichunguzwe.. . lakini hadi sasa hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa na Serikali.

  Tunaitaka iamke na kuchukua hatua hiyo ya kuichunguza, `` akadai Dk. Slaa.

  Kutokana na suala hilo, Dk. Slaa akadai kuwa CHADEMA itaendelea na Operesheni Sangara nchi nzima ili kuwahamasisha wananchi wachukie vitendo vya ufisadi wa aina ya Meremeta, ambavyo kwa bahati mbaya bado Serikali inachelewa kuvichukulia hatua stahili.

  ``Hatuwezi kuiacha Serikali inaachia mambo haya... tutapita kila kijiji cha nchi hii ili kuhamasisha wananchi wachukie vitendo vya aina hii,`` akadaiDk. Slaa.

  Kufuatia madai hayo ya Dk. Slaa, mwandishi alimsaka Mheshimiwa Chenge kwa simu yake ya mkononi leo asubuhi, mishale ya saa 4:05 ili aelezee juu ya tuhuma za kuhusishwa na Meremeta. Lakini alikataa kata kata kuzungumzia suala hilo na badala yake akajibu kwa ufupi, akisema `asante`.

  ``Asante sana... na kila la heri,`` akasema Bw. Chenge baada ya kuelezwa kila kitu kuhusiana na madai ya Dk. Slaa, kisha akakata simu.
   
 2. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  kisiwa cha NEW JERSEY au JERSEY?
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kulipuliwa upya?
   
 4. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #4
  Mar 22, 2009
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Naomba kuuliza swali la kijinga hapa!!!! Hivi mtu mwizi na fisadi kama Chenge kwa nini bado anakuwa addressed kama "Mheshimiwa"? Nafikiri heshima itokane na mchango wa mtu katika jamii lakini sio kwa kuwa tu ni mbunge. Naona taabu sana kulitumia neno hilo kwa kiumbe kama huyu mwizi na fisadi mkubwa.

  Katika kitabu cha Kuli (kwa wale waliokisoma), Majaliwa alisema haya yana mwisho!!! naomba mwenyezi Mungu aniweke hai nije nishuhudie mwisho wa serikali ya kifisadi ya CCM.

  Je kuna mwana JF anayeweza kupata nakala ya report ya tume ya Bomani juu ya Meremeta? Inawezekana report ina mengi tunayopashwa kuyajua na kwa nini serikali haijachukua hatua za kuchunguza kama tume ilivyopendekeza mpaka leo? Au ni mtindo ule ule wa kesi ya nyani kuipeleka kwa Ngedere?

  Tiba
   
 5. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #5
  Mar 22, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  yatafichuka mengi. aisee, mwisho wa mafisadi umekaribia, Mungu mwenyewe ameshuka kututetea watanzania. basi, na yeye tumwone kama kina mramba na Yona. ahamishiwe makao yake Keko. au ni kwasababu alisema "TUTATOKA WENGI" kwamba wangemfunga angejilipua kwa kuwaanika vigogo ambao hata hatutarajii kuwa ni mafisadi kumbe ni mafisadi. hao vigogo wanamwogopa kwasababu wakimgusa kumfunga tu, anawataja ili wawe kundi moja. tufanyeje sasa amewashika masikio?hahaha. kaazi kwelikweli.
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Mar 22, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  ........life is like a roll of toilet paper. The closer it gets to the end, the faster it goes.
   
 7. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #7
  Mar 22, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kuna siku itakuwa kama jua lachomoza magharibi na kutua mashariki hapo ndo itakuwa kilio na kusaga meno kwa mafisadi. Ole wao mafisadi waibao fedha zetu na kupeleka watoto na ndugu zao nje na badala hao walopelekwa kuwa creative wanaanzisha websites za kuchafua watu majina na personalities zao. Its now true even to the social unjust that "to every action there is equal and opposite reaction"

  Shame upon them!
   
 8. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #8
  Mar 23, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Umenena mkuu...!
   
Loading...