Chenge aandaa chakula Bariadi, Magufuli akacha kukila

Qualcomm

Senior Member
Nov 27, 2013
177
225
Katika hali inayoonyesha kuyakwepa mafisadi papa, Magufuli amekacha kula chakula kilichokuwa kimeandaliwa na mtemi Chenge kule Bariadi. Tukio hilo limetokea leo wakati Magufuli alipohutubia Bariadi na baada ya kumaliza mkutano alikaribishwa chakula nyumbani kwa Chenge, lakini akakataa katakata na ikamulazimu atembee siku nzima bila kula chakula. Watu wa ndani wanasema Magufuli hayupo tayari kushirikiana na mafiasdi hata kidogo.

91df29c2188163d14258762fd67b4a44.jpg
Dr.Magufuli akihutubia Umati wa watu - Bariadi​
 

MUSIGAJI

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
1,695
2,000
Ahaaa mwaka huu ccm Lowasa kawashika hasa.ebu naomba ujibu maswali haya.
1.Tangu Magufuri aanze mikutano ya campaign mikoa kadhaa sasa je Amefika nyumbani mwa.wagombea ubunge wangapi kwa ajili ya kushiriki chakula?Taja jina la mgombea ubunge na jimbo husika.

2.Unasema Magufuri amekataa chakula nyumbani mwa chenge hivyo kashinda na njaa je utaratibu wa chakula cha mgombea chama kimetoa maelekezo mgombea baada ya Kampeni atakuaa anaenda kula kwa mbunge?

Humu kuna watu na akili zao kijana sawa?siku zingine husirudie
 

Johne

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
328
170
Kwani wote si wanaCCM chenge kapitishwa na nani na magufuli kapitishwa na nani? hapo haijawasaidia mana itawaongezea wapinzani kura
 

Kitumbo

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
550
195
Wasingempa fomu ya ubunge Chenge ccm,ningewaamini hawa mafisadi ccm.Pesa za kampeni ya Magufuli zimetoka kwa mafisadi
Shida ipo kwa wananchi. Watu wa Chenge huwaambii kitu juu ya yake na hata upinzani hawawezi kumuondoa pale kwa sanduku la kura...
 

Johne

JF-Expert Member
Dec 31, 2013
328
170
Shida ipo kwa wananchi. Watu wa Chenge huwaambii juu ya fisadi wao na hakuna hata upinzani wanaoweza kumuondoa pale kwa sanduku la kura...


sio mwaka huu atang'oka kiulaini hata hutaamini ukawa tumejipanga kisayansi tumejumlisha mbinu za ccm na ukawa tunatumia mamluki wa ukawa na wanaccm yani mwaka huu ngoma inogile
 

Kitumbo

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
550
195
sio mwaka huu atang'oka kiulaini hata hutaamini ukawa tumejipanga kisayansi tumejumlisha mbinu za ccm na ukawa tunatumia mamluki wa ukawa na wanaccm yani mwaka huu ngoma inogile
Hili likifanikiwa itakuwa heshima kubwa kwa wapiga kura tanzania
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom