Hapo juu kuna viboksi vinne, na majibu yake ni kama ifuatavyo;-
1. kiboksi cha juu upande wa kushoto jibu lake ni 3.5
2. kiboksi cha juu upande wa kulia jibu lake ni 4.5
3. kiboksi cha chini upande wa kushoto jibu lake ni 9.5
4. kiboksi cha chini upande wa kulia jibu lake ni 3.5
Mchanganuo wa majibu yangu ni kama ifuatavyo;-
Kwenda kulia (kwa ulalo)
3.5+4.5=8
9.5-3.5=6
Kwenda chini (kwa wima)
3.5+9.5=13
4.5+3.5=8
Njia:-
Hatua ya 1:
Unavipa viboksi hivyo herufi mfano a, b, c na d.
Hatua ya 2:
Unatengeneza milinganyo minne (four equations)
Hatua ya 3:
Unakokotoa milinganyo sahili kutafuta thamani ya hizo herufi nne (simultaneous equations with four unknowns).
Hatua ya mwisho:
Unaagiza Tusker ya baridiiiii......