Chemsha Bongo 001

Hahaha mkuu una makasiriko mda wote

Sisi watu smart huwa hatupendi kuona watu wanapoteza muda kwa mambo ya kijinga. Nyie Taifa lenu linaangamia mpo tu huko mnaulizana maswali ya kijinga.badala ya hata mtuulize sisi tuliofanikiwa kimaisha tumefanikiwaje. Mnaulizana habari za sayari na mwezini? Halafu unataka niwachekee?
 
Hahaha mkuu una makasiriko mda wote

Sisi watu smart huwa hatupendi kuona watu wanapoteza muda kwa mambo ya kijinga. Nyie Taifa lenu linaangamia mpo tu huko mnaulizana maswali ya kijinga.badala ya hata mtuulize sisi tuliofanikiwa kimaisha tumefanikiwaje. Mnaulizana habari za sayari na mwezini? Halafu unataka niwachekee?
 
Taifa linaangamia wapi bwashee?
 
Sheikh wangu kama hujaweza ona wapi basi tayari tatizo ni kubwa kuliko nlivyodhania. Nyie endeleeni kukariri kwenda mwezini na ratiba zake.
Kwa hiyo mkuu tuufuatie ule uzi wako wa mwanamke wako kuloa mda wote tu? Ndio hakuta kuwa na tatizo bwashee?
 
Shukrani expert wangu,kikubwa tunapata elimu
 
Haya naona mlima umekuwa mgumu kuukwea

here we go....

1. Albert Einstain
2. Thomas Edison
3. Mahtam Gandhi
4. Socrates
5. Conficuos
6. Friedrich
 
CHEMSHA BONGO 004

1. Vita ya kwanza ya dunia ilianza mwaka gani na kuisha mwaka gani?

2. Ni miji gani iliangamizwa na bomu la atomiki mwaka 1945

3. Ni taifa gani la kwanza duniani kutuma mwanadamu angani

4. Ni mwaka gani dola la Ottoman lilivunjika na kuundwa taifa la Uturuki

5. Ni kiongozi gani alibadilisha Uchina kuwa jamhuri mwaka 1949
 
Naam ni mwendo wa kupata maarifa kupitia chemsha bongo

here we go....

1. Vita ya kwanza ya dunia ilianza 1914 na kumalizika 1918

2.Miji iliyoangamizwa na atomiki ni Nagasaki na Hiroshima nchini Japan

3. Umoja wa kisovieti (USSR] Mwaka 1961 ulituma mwanadamu wa kwanza Angani

4. Dola ya Ottoman ilivunjika mwaka 1923 na kuundwa kwa taifa la Uturuki

5. Kiongozi aliyebadilisha Uchina kuwa jamhuri ni Mao Zedong mwaka 1949
 
Unatembea maili moja kusini, maili moja magharibi, na maili moja kaskazini. Unaishia hapo ulipoanzia. Uko wapi?
 
Unatembea maili moja kusini, maili moja magharibi, na maili moja kaskazini. Unaishia hapo ulipoanzia. Uko wapi?
Hili swala hakika kila mtu ana maoni yake lakini ishu ya kuwa flat ni changamoto sana kwakweli

Ila tunaheshimu maoni yenu wenye kuamini hivyo
 
CHEMSHA BONGO 005

1. Ni mji gani wa kale ulizuiliwa kwa ukuta wenye milango 7 kwa mujibu wa historia ya wagiriki,wamisri na waarabu?

2.Ni nani alipata heshima ya kugundua Amerika kwa upande wa wazungu mwaka 1492?

3. Ni mwanamke gani alikuwa wa kwanza kupata tuzo ya Nobel,na alishinda mara mbili
 
Wazee wa kusema dunia ni flat, ebu someni hoja zifuatazo:

Ushahidi wa kisayansi na wa kimaumbile unaoonyesha wazi kwamba dunia siyo flat (bapa) bali ni mviringo (spherical/oblate spheroid).


---

Ushahidi kwamba dunia siyo flat

1. Picha kutoka angani na satelaiti

Tangu safari za anga za mwaka 1961 na kisha kutumwa kwa satelaiti, dunia imepigwa picha nyingi kutoka angani. Zote zinaonyesha dunia ikiwa duara/mviringo, na hii ni ushahidi wa moja kwa moja.



2. Kutoweka kwa meli taratibu baharini

Ukiangalia meli baharini, haipotei mara moja kwa ghafla. Huonekana chini kwanza (sehemu ya chini ya meli) kisha juu yake – kwa sababu inazunguka kufuata mviringo wa dunia. Kama dunia ingekuwa flat, meli ingezidi kuwa ndogo tu ila isingefichwa polepole.



3. Kupishana kwa kivuli cha dunia wakati wa kupatwa kwa mwezi

Wakati wa kupatwa kwa mwezi (lunar eclipse), kivuli cha dunia huonekana juu ya mwezi. Kivuli hicho huwa daima na umbo la duara, ishara kwamba dunia ni mviringo. Dunia ikiwa flat isingeweza kutoa kivuli cha duara kila wakati.



4. Mabadiliko ya nyota unaposafiri

Ukiwa kaskazini au kusini, nyota unazoziona hubadilika. Mfano, nyota ya Kaskazini (Polaris) inaonekana vizuri kaskazini, lakini ukienda kusini haionekani. Hii hutokea kwa sababu dunia ni duara.



5. Kutofautiana kwa muda wa mchana na usiku

Sehemu moja ya dunia huwa na mchana wakati nyingine zina usiku. Ikiwa dunia ingekuwa flat, jua lingeangaza kila mahali kwa wakati mmoja. Lakini kwa kuwa dunia inazunguka na ni duara, mwanga wa jua hauwezi kufika pande zote kwa wakati mmoja.



6. Kutofautiana kwa kivuli (Jaribio la Eratosthenes, 240 BC)

Mwanasayansi Eratosthenes alipima kivuli cha miti katika miji miwili tofauti Misri (Alexandria na Syene). Aliona kivuli kilikuwa tofauti, kitu ambacho kingewezekana tu ikiwa dunia ni mviringo.



7. Kutofautiana kwa majira na hali ya hewa

Wakati kaskazini ni majira ya baridi (winter), kusini ni majira ya joto (summer). Hii ni kwa sababu dunia imeinama kwenye mhimili wake na ni mviringo. Kama dunia ingekuwa flat, kusingekuwa na majira ya aina hii.





---

Kwa kifupi, sayansi ya anga, fizikia ya mwanga, safari za meli na ndege, kupatwa kwa mwezi, na uchunguzi wa nyota vyote vinathibitisha kuwa dunia ni mviringo na siyo flat.
 
Haya majibu haya hapa:

1. Jerusalem

2. Christopher Columbus

3. Marie Curie
 
CHEMSHA BONGO 006

1. Ni kitu gani kina uzito lakini hakionekani

2. Ni sayar ipi inajilikana kama Sayar nyekundu

3. Nini kinacho wezesha ndege kuruka angani

4. Ni metali ipi nyepesi zaidi kuliko zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…