Cheki pozi la mshangaoooo!

nzuri, lakini naona inafaa kule kwenye hbr mchanganiko au gossip and fun, hili ni jukwaa la hoja tu.
otherwise karibu sana JF, au wewe ni mwenyeji kwa ID mpya?
 
View attachment 34530Credit: Nathan Mpangala
Kuna cartoonists wachache sana ninaowakubali Nathan si mmoja wao, kwa umri wake kwenye game sio wa kutuletea vitu vya kitoto kama hivi, cartoon sio michoro na message tu, lazima iwe na humour (kichekesho). Kuna watu kama masoud kipanya, sammy (jo'une) Kwa maelezo zaidi nibishie.
 

Mkuu kila mtu ana mapenzi yake..., kuona kwako kwamba Nathan Hafai sio kwamba hafai mimi naona Kingo ndio mwisho wa maneno hakuna kama yeye Kwa maelezo zaidi nibishie.

Mkuu mleta mada nadhati hii ingefaa sana kwenye jukwaa la Photo (omba tuamishiwe huko ili tuendelee kuchangia vizuri)
 
Nimekusoma VoiceOfReason, kingo ni kiboko kwa sa babu ana uwezo wa kuchora picha bila maelezo na bado akaeleweka na akachekesha, cartoon ni elimu kwa njia ya burudani, na ndicho anachofanya kingo, ukiangalia cartoonists wengi wa bongo hawana qualities hizo. Ndo maana nasema nathan kama kweli ni msanii anayekua alipaswa kuwa beyond that long ago, anachofanya mtu yeyote can do apart from posing character. mfano unachora mtu anatembea unam-lable tz halafu mbele unaweka jiwe kubwa limeziba njia unali-label mgawo wa umeme, halafu mbele yake unaweka kibao kimeandikwa mafaniko hapo kuna ubunifu mkuu??? Acha nitulie niomne mada ihamishwe ili tuendelee kuijadili kwa manufaa ya wote. Kwa maelezo zaidi nibishie.
 
Sorry nimejibu swali la mleta mada hapo juu, lakini atakuwa amepata message na atalifanyia kazi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…