Cheka uongeza afya

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,736
4,252
SOMA HII NA CHEKA KWA KUONGEZA AFYA.

Mwelevu na Mjinga walienda ktk usaili, walipofika kabla hawajaingia wakakubaliana aanze Mwerevu kisha akitoka ampe majibu Mjinga ili wote wapate kazi.

Basi Mwelevu akaingia na maswali yakawa hivi:-
Msaili:- Tanzania ilipata Uhuru mwaka gani?
Mwelevu:- ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa mpaka 1961 kutokana na sababu mbalimbali..

Msaili:- Nani hasa alihusika na upatikanaji wa Uhuru huo?
Mwelevu:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J.K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia.

Msaili:- Inasemekana ktk sayari ya Mars kunaviumbe wanaishi, je ni kweli?
Mwelevu:- Watu wengi wanasema hivyo lakini haijathibitishwa na wanasayansi.

Baada ya Mwelevu kutoka basi Mjinga akapewa majibu yote..
Kuingia ktk usaili maswali yakawa hivi:-

Msaili:- Tuambie ulizaliwa mwka gani?
Mjinga:- Ilitakiwa iwe mwaka 1960 ila ikasogezwa mbele mpaka mwaka 1961 kutokana na sababu mbali mbali.

Msaili:- Mungu Wangu, BABA yako anaitwa nani?
Mjinga:- Kuna watu wengi walihusika ila Mwl. J. K. Nyerere ndiye alikuja kumalizia .

Msaili:- Hivi wewe ni chizi?
Mjinga:- watu wengi husema hivyo lakini haijathibitishwa na wanasayansi.
 
Back
Top Bottom