Cheche No.43: JWTZ nayo imebinafsishwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Cheche No.43: JWTZ nayo imebinafsishwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 26, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kuna jaribio la hatari limefanyika ambalo hatuna budi kulikataa, jaribio la aidha kulibebesha Jeshi letu lawama isiyostahili au la kulitumia kufanya lisiyostahili. Yote mawili ni ya hatari kwa taifa. Majibu ya Waziri Mkuu Bungeni mwaka jana kuhusu Meremeta ambayo yamerudiwa tena hivi juzi na Naibu Waziri wa Fedha. Bw. Jeremiah Sumari kuwa suala la Meremeta linahusu "ulinzi" na "Usalama wa taifa" yanatulazimisha kujihoji kama Jeshi hili bado liko mikononi mwa wananchi.

  Swali hilo ni muhimu kwani wabunge wote wa CCM wamekubali wakiwa na akili timamu kutotaka kujua juu ya Meremeta na wamekubali hoja kuwa wao kama wawakilishi wa serikali hawawezi kujua kinachofanywa na serikali. Uamuzi wao huo ni kinyume na katiba na unawafanywa wasistahili kuwepo Bungeni kwani wanavunja Katiba ambayo waliapa kuilinda.

  Inabidi sasa kuanza kuandaa orodha ya wabunge wote ambao wanakasirishwa na neno "ovyo ovyo" na kukaa kimya wakati mambo ovyo ovyo yanafanywa; wabunge ambao ni wakali Bunge linaposhambuliwa lakini wako bubu wakati Bunge linafanywa kituko cha uongozi.

  Katika sehemu ya kwanza ya kulifunua suala la Meremeta tunaangalia kwanza hoja ya kisiasa na kisheria ya kwanini ni LAZIMA jeshi letu siyo tu liwe la "wananchi" kwenye vitabu na nembo, bali lazima liwe chini ya uangalizi wa wananchi (kupitia wawakilishi wao). Nje ya hapo tunalitakia taifa mabaya.
   

  Attached Files:

  Last edited: Jun 26, 2009
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji, bado naendelea kusoma toleo la Cheche, no 43. Ni mambo mazito kwa kweli. Ubarikiwe kwa kazi ngumu na iliyo ya kujitolea kulihabarisha Taifa letu la Tanzania katika mengi ambayo wengi wetu hatuna uwezo wa kuyajua wala uthubutu wa kuyafatilia jinsi ufanyavyo wewe.

  SteveD.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  it is a blessing and a curse mate.. I want to stop.. I can't.
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Wamefikia hatua ya kulitumia jeshi kwa maslahi binafsi, ni hatari
   
 5. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,841
  Likes Received: 1,102
  Trophy Points: 280
  Asante M.M.M na kikosi kizima cha cheche.

  Inasikitisha kwamba malalamiko ya msingi hayasikilizwi mbaya zaidi tunakosa channel ya ku-push na kuwaweka kona akina mhe. Pinda. Ni dhahiri kwamba kwa kupitia bunge almost imeshindikana.

  Hivi taratibu za kuunda pressure groups zipoje? i wish vijana waliopo Tz wawe-mobilized na kuunda pressure group ya kulinda mali asili. Group hiyo inaweza kuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko ktk sekta ya mali asili.

  Sometime, viongozi wa dini waliunda kamati, ikatembelea maeneo ya machimbo ya madini na wakatoa ripoti (Mpiganaji Tundu Lisu ndo alikuwa key player). Lakini kazi yao iliishia kwenye ripoti tu ambayo imesomwa na wachache na kusahaulika. Nadhani pakiwepo na activists group mapigano yatakuwa endelevu.
   
 6. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mwanakijiji!
  hii inasikitisha sana, kwani viongozi wetu na wabunge wetu wamepofuka akili na macho.
  Nakupongeza kwani unaachana na kasumba ya wengi ya kufunika kombe.Kidedea hiki kikiendelea bunge hadi bunge kikao hadi kikao kuna siku wataachia na tutakuwa washindi.Kwani ya Malawi hata Zambia ni ya kale ila leo kunachimbika na vumbi tunaliona.
  Bravo Mkj take five.
   
 7. C

  Campana JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tunataraji kusikia kutoka kwa Zitto (kwa vile yumo humu) juu ya yale aliyoongea Nimrod kuhusu kazi 'mbofumbofu' iliyofanywa na kamati yao.
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  ..Kushuka na kupanda kwa Manka kanka Mussa aliyekuwa mtawala wa.....
   
 9. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mansa?!
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0

  Mali empire ... ambaye nusra aue uchmi wa Misri alipomwaga dhahabu za kutisha wakati anaenda kufanya Hijja Makka wenyewe walikuwa wakimwita MUSA maana mansa kikwao maanake mfalme

  huyu hapa:

  [​IMG]

  huyu aliishi miaka ya 1280 mpaka 1337...btw wazungu bado walikuwa wanaishi kwenye primitive life

  wewe nawe wankumbusha histori bwana!
   
 11. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #11
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280
  Namuomba Mh Zitto Kabwe afafanue kuhusu kauli hii ya Mh Nimrod Mkono:

   
 12. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kauli ya Mkono inahitaji majibu kutoka kwa wanakamati. Na maelezo ya Mkono inaonyesha kwamba yeye (mkono) alikuwa na imani sana na uwepo wa Mjumbe mbunge kutoka kambi ya upinzani kwamba asingeficha mbegu ila hakuona kitu. mjumbe toka hadharani na ufafanue nini mliambiwa msiseme na nini mlikijua. Tanzania itajengwa na wazalendo wa kweli.

  Hizi tume zote ni kanjanja na wajumbe wake wengi ni kanjanja.
  Tume ya Mwakyembe ilileta majibu ila iliacha maswali Mengi baada ya Mwakymbe kusema kuna baadhi aliyaficha.

  Tume ya Bomani pamoja na kupewa kitita cha fedha wajumbe wote wameyeyuka na hakuna majibu ya tume ile wala nini walikiona, wanakuja na mashairi ya mapendekezo, huwezi toa tiba bila ya kujua maradhi au kumwambia mgonjwa maradhi yake.

  Tume ya Jaji kisanga walitukanwa baada ya majibu. Mimi naona Tume ni ufisadi mkubwa sana kuliko ufisadi wowote. kwani hutumia fedha nyingi hazileti majibu wala tija. Na zimekuwani njia ya kunyamazisha ufisadi na utendaji mbovu.
   
 13. M

  Magezi JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  mimi napenda kujua ni nini msimamo wa askari wa kawaida kuhusu issues za meremeta na deep green? Naomba ufafanuzi kwa yeyote
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hilo la Mkono lisiwashtue sana;

  YEYE ni Mbunge ambako Buhemba ipo
  YEYE alikuwa wakili wa Benki Kuu wakati machafu haya mengi yanatokea


  Sasa leo iweje awe shujaa? Alichofanya kimsingi ni kuwathubutisha watu na kucheza na hisia za wapiga kura wake. Ni kujifanya hajui kilichotokea. Mbona mwaka huu yeye hayapiga kelele tena? Ile kamati ya Rais mimi niliikataa tangu mwanzo kwa sababu haikuwa ya lazima yoyote. Ilitakiwa iundwe kamati teule ambayo Mkono aliipendekeza.

  Lakini ukimya unaonishtua ni wa wale walio wengi Bungeni. Wabunge wa CCM.
   
 15. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #15
  Jun 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ingawa sijaweza kusoma cheche hii ya leo, lakini napenda kutanguliza pongezi kwa mkuu wewe Mzee Mwanajijiji kwa uzalendo wako usio na shaka. Mungu wa majeshi akubariki katika kazi yako na kikosi kizima cha CHECHE. hAKIKA SIKU MOJA TUTASHINDA UDHALIMU HUU MAANA MUNGU HAWEZI KUTUACHA MILELE. na wasomaji wote Mungu awabariki.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280

  Asante sana.. ila wakati mwingine huwa naona kana kwamba Mungu amekula njama dhidi ya Tanzania. Maana kila tukiwaombea baraka "viongozi wetu" ndio wanavyozidi kufanya madudu; inabidi tuanze kuimba

  Mungu Ibariki Tanzania
  Usiwabariki viongozi
  Wake kwa waume na watoto
  hizi ni ngao zetu
  Tanzania na watu wako

  Tubariki, Tanzania
  Tubariki, watoto wa Tanzania!
   
 17. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #17
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  • Kamba hukatika pembeni,
  • Mtumbwi huzama ukikaribia kufika (Obwato bufa a-magoba-from British Kingdom)
  • Wengi hukata tamaa wanapokaribia mafanikio
  Dont stop man, tupo pamoja hadi round ya 12. Wakiongeza pia tutaendelea
   
  Last edited: Jun 27, 2009
 18. M

  Moelex23 JF-Expert Member

  #18
  Jun 26, 2009
  Joined: Oct 8, 2006
  Messages: 497
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji pongezi maalumu kwako kwa kuquote na kukumbushia KATIBA throughout cheche la leo.

  Mh. Slaa, Mh. Zitto, Mh. Mama Kilango, Mh Seleli na wengine muanze kuanzia leo kushikilia katiba kila mnapoongea bungeni, na mkiletewa rasha rasha na hao wabunge maboga naomba defense ya kwanza iwe kunyanyua KATIBA na kusema nalinda hii na kuquote vifungu mbalimbali ambavyo nina uhakika 100% wabunge wengi na especially MAWAZIRI hawajui NGUVU YA BUNGE KIKATIBA.
   
 19. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #19
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mimi nadhani Mh. Nimrod Mkono ana nafasi nzuri ya kufafanua kuliko Mh Zitto Kabwe.

  Ila pia kauli kama hiyo kutoka kwa N. Mkono, ni matusi kwa tafsiri ya kupewa pipi, kwani yeye Mkono kapewa kiwanda cha pipi na hao Meremeta na BOT.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Jun 26, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Unajua Moelex, dhana ya utawala wa Katiba hapo kwetu haieleweki sana na hasa wale walioviongozi. Wanaposema kuwa nchi yetu ina utawala wa Katiba yawezekana wengi wanamaanisha kuwa "nchi ina Katiba". Hilo ni kweli lakini siyo maana hasa ya utawala wa Katiba.

  Utawala wa katiba ni hicho ulichosema. Kwamba, kunapotokea hoja, matatizo ya kisheria, dhulma n.k kimbilio letu ni kwenye Katiba. Katiba basi inakuwa ni mwamvuli wa usalama wa gharika la udhalimu, uvunjaji wa sheria, haki na usawa.

  Hivyo, Waziri anaposema "hili haliwezi kujadiliwa hadharani" badala ya Mbunge kusema "sawa" anatakiwa aulize "katiba inasemaje?", Waziri anaposema kuwa wabunge hawastahili kuuliza swali x,y mbunge anatakiwa kusema Katiba inasemaje?

  As a matter of fact, kwa vile Katiba yetu imeandikwa na iko kwenye kitabu, inatakiwa Mbunge anaposimama na kupigwa mkwara wa sheria au kanuni ya Bunge, ulinzi wake hakimbilii kwa Spika bali kwa Katiba hasa pale ambapo anaona Spika analeta matatizo.

  Matokeo yake ni kuwa kanuni ya Bunge inaposimamishwa na kutumika kama kinga ya kuzuia mijadala Bungeni, Wabunge wanatakiwa hata kwenda Mahakamani kuihoji uhalali wa kanuni hiyo.

  Hivyo, utawala wa Katiba kimsingi ni kuikimbilia Katiba na ndani yake kuomba ufafanuzi na kinga ya kisheria.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...