Chaza wa baharini yukoje?

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
7,924
8,174
Habari wadau,

Kuna msemo wa Kiswahili "amekushinda Chaza utaweza kumla Pweza?"

Pweza nafahamu muonekano wake na nimeshuhudia watu wakila vipande vyake. Je, huyu Chaza anaelinganishwa na Pweza kwenye huo msemo yukoje?

Nimejaribu kuuliza lakini napata majibu tofauti. Kuna mtu kashaniambia kuwa chaza ndie Kaa au Ngadu ni kweli?
 
Hapana sio kweli chaza hafanan hata kdogo na kaa wala ngadu...Chaza ni species flani hiv anaishi ndani ya Gamba lake gumu hivi,yy ypo ndani,anapo hitaj chakula hufungua gamba lake na kutafta rizk...Ni mdogo xn w umbo mfano wa kiganja cha mtt mdogo,gamba lake limemzunguka mwl wte tofat na kobe amba gamba lak lpo juu tu...Anaishi kweny mapang na vichuguu vdogo vy baharini huwa ni kitoweo kwa kwa wakaz wa baharin,na havuliwi kw ndoana wala nyavu Huwa watu wanakweny baharin maji ya kipungua(low tide) na hutafuta kweny hvy vipango vdogo vdogo...Kuhusu huo msemo kuwa "Amekushinda pweza utamuweza Chaza"Maana yake nu kwamba ikiwa pweza hana magamba anategemea tu mikia yak kumlinda Na amekushinda ,je utamuweza kumla chaza ambae anaishi ndani ya Gamba lake?Kumbuka ili umle chaza inabidi ulibandue lile Gamba lk tena kwa maji ya moto yanayo chemka....Nadhan kdog nmekupa pcha....
 
Ikhlas umeenda vzr, lkn hapo mwisho umechemka. Msemo uko hivi "umeshindwa kumla chaza pweza utamuweza wapi" kuwa kale kadodo chaza kanakoishi kwenye vipango vidogo dogo, utamuweza wapi pweza wa mikia minane anayeishi mapangoni na jasiri mwenye kujihami na wino"
 
Habari wadau,

Kuna msemo wa Kiswahili "amekushinda Chaza utaweza kumla Pweza?"

Pweza nafahamu muonekano wake na nimeshuhudia watu wakila vipande vyake. Je, huyu Chaza anaelinganishwa na Pweza kwenye huo msemo yukoje?

Nimejaribu kuuliza lakini napata majibu tofauti. Kuna mtu kashaniambia kuwa chaza ndie Kaa au Ngadu ni kweli?
Huya hapa Chaza
images

Ahsante ikhlas Shukran kutuelewesha!!
 
Natumai majibu yamejitosheleza.
Ukija pwani wambie watu wakutafutie uwaone na uwaonje.
Ila lazima ujue kuna Chaza na Makome,wanataka kufanana ila sema kome wakubwa na nyama nyingi
Ila Chaza havuliwi,ila utasikia mtu anakuambia naenda kuvuna Chaza,maana wanakuwa kwenye mawe unawashika kwa mkono tu.Na ndio maana husikii mtu anakuambia naeneda kuvua chaza ila anakuambia naenda kuvuna chaza.

Kichekesho kwa Chaza na Kunguru.
Chaza hupatikana kwenye Mawe yaliyopo pembezoni mwa Pwani yaani maji mafupi,na hupatikana kwa wingi wakati maji yakitoka yaani Low Tide state.Kwa mliopo Zanzibar mjini,chaza wengi hupatikana maeneo ya Buyu na Chukwani kwa ujumla,huko wapo wengi sana,mpaka fumba huko
Yaani chaza nje ni ganda gum saana,ila ndani ni nyama,sasa huwa yupo kama vile mkebe.
Kuna muda anajifungua,maana uhai ni wa ndani nje ni protector tu wakati wa hatari.
Sasa Kunguru huwa anamlia timing ile akifunguka tu jamaa anatua anamla,ila kuna baadhi ya mida na yeye inakula kwake,ile anatua tu jamaa anabana,basi burudani kwenda mbele.
Shell au ganda lake la nje aisee ni zaidi ya kisu,ukienda kuvuna chaza,kama ni mgeni basi mikono yote inajaa damu.
Hapo bado hujawachambua wakati wa kuwachemsha,aisee kazi hii ni ngum kweli.
Maana wale unawachemsha ili lile ganda lifunguke,sasa wakati wa kuwatoa kwenye ganda,aisee unalambwa vile visu balaa,maana ganda zake za nje kali saana,
 
Wadigo wanamwita kome/makome, maji ya kipungua ndo waenda chokoa huko mwambani kisha humchemsha kidogo nabkutoa nyama yake, kisha aungwa kwa nazi, waweza mla kwa bada au dona, ila kiboko ni manga wa kolekole aloungwa nazi ati. Odo ukuphi nije nile mababuji au mofa
 
Kweli jamii forum ni darasa la uhakika. Nimejifunza mengi kuhusu huyo kiumbe Chaza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom