Chato: Rais Magufuli ampokea Rais Museveni wa Uganda

Hivi hizi ziara za kibinafsi zimekuwa za kitaifa?
TBC badala ya kugharamia watu kusafiri kila siku kwenda Chato wafungue ofisi kabisa na kuhamisha staff was kutosha.
Usimlinganishe Rais na chairman wa chadema!
 
Hata ITV nao wameingia kwenye huu ukuda, inakera sana.
Nimeikuta ITV nayo kweli imeingia mkenge.
Ila maajabu ya huko, unampokea mgeni lakini nyimbo na mapambio yote unamsifu mwenyeji!
Haki ya nani jamaa ni noma kwa sifa
 
Nilikutana na Mkongomani mmoja akaniambia "kwetu Congo tungempata Magufuli na kisha tukawa na amani hakuna nchi ingetufikia kwa maendeleo Afrika. Watanzania hamna vision ndio maana hamjui thamani ya rais mliye naye" mwisho wa kunukuu!
Kongo DRC Wakongoman wameacha kusikiliza muziki wao, siku hizi wanatembea na simu zao huku wakisikiliza hotuba za Magufuli-JPM. Wasio mpenda watanuna tu hamna jinsi nyengine ya kuwa saidia.
 
Karibu TBC tufuatilie mapokezi ya Rais wa Uganda mh Yoweri Kaguta Museveni mjini Chato mkoani Geita.

Up dates;
Rais Museveni ameshawasili na nyimbo za taifa zinapigwa pamoja na ule wa Afrika ya mashariki.

Sasa ni wakati wa kuomba dua na anaanza kiongozi wa Bakwata na amefuatiwa na askofu Severini wa Kanisa Katoliki.

Rais Magufuli anamkaribisha mgeni wake ambaye ametokea Angola na kuja direct Chato aweze kuongea na watanzania.

Rais Museveni anaanza kuelezea maana ya neno Chato na anasema kuna chato cha zizi la ng'ombe, chato cha pombe na chato cha wavuvi.

Museveni anasema wakati waislamu wanaenda Hijja Mecca na wakatoliki wanaenda Roma yeye na wapigania uhuru wote kusini mwa Afrika Hijja yao ni Dsm nchini Tanzania.

Mwaka ule alipokuja alifadhiliwa ndege na KQ, nadhani kwake hana ndege hata moja, vipi this time amefadhiliwa na nani
 
Nilikutana na Mkongomani mmoja akaniambia "kwetu Congo tungempata Magufuli na kisha tukawa na amani hakuna nchi ingetufikia kwa maendeleo Afrika. Watanzania hamna vision ndio maana hamjui thamani ya rais mliye naye" mwisho wa kunukuu!
bullshhiit!,ubinafsi hana jipya,mara uwanja wa ndege,benki,mbuga for which purpose,?,pesa zetu
 
saa 24 inamtangaza yeye tu?

Mimi sio shabiki wa Magufuli kabisa, lakini kwa hili la kuwapokelea hao wageni wake huko porini namuunga mkono. Tumechoka na jam hapa mjini zisizo na tija kwa hao viongozi wa East Africa kuja kupiga porojo, huku waliyokubaliana yakiwa kwenye mikataba hayatekelezwi. Itapendeza sana kama kuanzia sasa kila akipata mgeni wakakutanie huko huko Chato sisi tuendelee kusaka mkate wetu hapa mjini. Sitaki hata kujua wameongea nini maana najua ni porojo ila nimeshukuru kwa kutuondolea adha hapa mjini ya jam. Magufuli hoyee kwa kufanyia mikutano huko porini.
 
Kongo DRC Wakongoman wameacha kusikiliza muziki wao, siku hizi wanatembea na simu zao huku wakisikiliza hotuba za Magufuli-JPM. Wasio mpenda watanuna tu hamna jinsi nyengine ya kuwa saidia.

Wacongoman wapi wa kumsikiliza Magufuli? Hao wanaoita risasi "masasi" ndio watamsikiliza?
 
Wacongoman wapi wa kumsikiliza Magufuli? Hao wanaoita risasi "masasi" ndio watamsikiliza?

Tatizo Tanzania investigative journalism bado. Wangeenda wakaja na documentary ungeshangaa JPM anavyo kubalika huko Africa na Duniani, Acha hapa Jf kwenye propoganda,uchwara za kumchafua za mafisadi na vibaraka wao.
 
Hata sisi tulikuwa tunamkubali Gaddafi maana habari zilizokuwa zinatolewa ndani ya nchi yake zilikuwa ni za kwake tu. Lakini ukweli halisi walikuwa wanaujua wananchi wake. Alipotolewa madarakani ndio ukweli ulikuwa wazi alichokuwa akiwafanyia wananchi wake hasa wale anaotofautiana nao. Huenda wengi huko nje wakawa wanamkubali kwakuwa wanalishwa habari za upande mmoja, lakini ukweli tunaujua sisi wananchi tulio hapa.
 
Lazima uwe na akili ya maiti kulinganisha Libya/Walibya na Tanzania/Watanzania. Lakini lazima uwe na akili ya kibudu/nyamafu kumlinganisha JPM na Khadaf
 
Lazima uwe na akili ya maiti kulinganisha Libya/Walibya na Tanzania/Watanzania. Lakini lazima uwe na akili ya kibudu/nyamafu kumlinganisha JPM na Khadaf

Tena kwa taarifa yako Gaddaf alikuwa bora kuliko JPM kwa kila kitu kuanzia maendeleo mpaka udictator. Lakini kipimo hicho ni iwapo tu watalinganishwa wao wawili basi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom