Charles Kitwanga atoweka ktk mazingira tatanishi, haonekani Bungeni wala Jimboni toka kutenguliwa

Atakuwa anapata bed rest. Akiricover atarudi tu mjengoni na jimboni. We unadhani kufukuzwa kazi ni kitu rahisi kuki accept moyoni?
 
Mbona nilisikia kafiwa na mwanaye kwa ajali ya gari Mwanza ebu fuatilieni??
 
Sio yeye tu, angalia wabunge wote waliopata kuwa mawaziri kisha wakavuliwa kama utaona wana michango yenye tija. Wengi ni kama hawakubaliani na ule usemi wa mpanda ngazi.
 
Mbona nilisikia kafiwa na mwanaye kwa ajali ya gari Mwanza ebu fuatilieni??

Mtoto alikufa siku nyingi..........

PG4A2820.jpg
 
Muacheni anahitaji kupumzika na kutafakari na kujipanga kwa maisha mapya! Atakuwa ameenda India kufanyiwa counselling ......aweze kuanza maisha mapya!
 
Ajali ilikuwa 2014 na sio 2015. Alafu ajali ya saa 9 usiku uliishuhudia vipi mkuu?
Haikuwa saa tisa usiku ilikuwa mchana kweupeeeee labda wewe ndie hujui kisa: ngoja nikuweke sawa ili upunguze ubishi. huyu Vedastus alikuwa na rafiki yake ambaye alipata kazi ya Maxmalipo hapa Mwanza akitokea Dar alifikia kwao pale mawe matatu, huyu mgeni akawa ametoka mjini ana drive alipofika eneo la TANESCO Igogo kulikuwa na mchanga mvua imenyesha akaparamia tuta na baadae akagonga lile dude la TANESCO, TANESCO wakaita traffic (WP), yule mgeni alivyoona ameshindwa kuelewana na traffic ndio akampigia Vedastus na Richard waje eneo la tukio wamsaidie, walifika fasta bila kusita ili kuongea na traffic, ghafla walipokuwa wanaongea na traffic gari nyingine tena ikagonga lile tuta la mchanga ikaruka hadi walipokuwa pembeni ya barabara, Vedastus alifia hapo hapo na Richard alifariki siku ya pili, traffic alivunjika shingo na yule mgeni wa Vedastus aliyekuwa amewaita hakuumia hata tone. HAYA SEME LINGINE KAMA KWELI WEWE NDIE UNAYEJUA HII ISSUE
 
Anaandaa MAPOKEZI makubwa jimboni kwake,sasa hivi Mipango ya kuandaa maelfu ya pikipiki inaendelea,kinamama wanapangwa kwa ajili ya vigelegele,magari,gambe,na hiyo ni kuanzia airport mwanza...

Baada ya hapo ni mbina ya wigashe bhagosha mpaka asubuhi

NB: kinachokwamisha ni ukosefu wa yale masufuria makubwa ya kupikia ugali na mwiko mkubwa kama kasia za mitumbwi,kwa wasukuma ugali mgumu sana wa dona ni wa muhimu,tahadhali ni kwamba usizue ugomvi siku hiyo,tonge la ugali huo ni gumu kama jiwe,kwa wale wenye nua ya kujifunza jinsi ya kuviringisha tonge na kutoboa kashimo kenye uwezo wa kuchukua robo lita ya mchuzi karibuni
 
Back
Top Bottom