Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Status
Not open for further replies.
Napata kuunganisha dots! Wengi wa mawaziri na katibu wakuu wanafanya biashara na serikali na kuuiba juu! Kitwanga ndie atakuwa amemshauri JPM huyo best yake aingie NIDA pale! Amtoe BoT ampe NIDA!
Hapo umelonga! Si kitwanga naye alikuwa BOT?
Btw, Kitwanga hata kwa usoni, haonekani kama ni mtu mwenye akili ya maana kuweza kuwa waziri! Facial appearance yake ni ya mtu anayestahili kudhibitiwa, siyo tena awe ndo anadhibiti wengine.
 
Najiuliza infosy walikuwa wanawajibu gani katika huo mkataba, maana ulikuwa Kati ya LUGUMI na Serikali
 
WAZIRI WA MAGUFULI KTK KASHFA YA UFISADI NA POLISI

- Kampuni inayohusishwa naye ya Infosys ilikuwa mkandarasi

Yadaiwa Infosys inamilikiwa na Kitwanga na Mkurugenzi Mkuu NIDA

Ni mdau wa LUGUMI enterprises

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34, imeelezwa.

Kuhusika huko kwa Waziri Kitwanga imekuja siku moja, baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) kueleza kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye mkataba ulioingia kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

Taarifa za kuaminika ilizozipata gazeti hili, zimeeleza kuwa Waziri Kitwanga anahusika kupitia kampuni yake ya Infosys anayomiliki pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyo chini ya Wizara hiyo hiyo.

Jeshi la Polisi limekumbwa na kashfa kubwa ya manunuzi ya vifaa vya kuhifadhi alama za vidole ambapo Kamati ya PAC imegundua kuwa kampuni ya Lugumi Enterprises haikutekeleza mkataba ipasavyo.

Kampuni hiyo ililipwa sh. bilioni 34 na jeshi la polisi ili kusambaza vifaa hivyo nchi nzima katika vituo 138 vya polisi lakini ni vituo 14 vilivyopata vifaa hivyo.

Gazeti hili limegundua kuwa moja ya kampuni iliyopewa kazi hiyo ni Infsosys ambayo nakala za msajili wa makampuni inaonyesha kuwa inamilikiwa na Charles Kitwanga na Dk. Modestus Francis Kipilimba, ambaye ni Mkurugenzi wa NIDA.

Nyaraka za uchunguzi ikiwemo mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Infosys ambazo gazeti hili imeziona inaonyesha kuwa Kampuni hiyo ya Waziri Kitwanga ilifanya kazi ya kuunganisha internet kati ya vituo vya polisi na mkonga wa taifa.

Kazi ambayo haikufanyika kabisa kwani mpaka sasa ni vituo 14 tu vya polisi viliunganishwa, ambapo baadhi ya taarifa ilizozipata gazeti hili zilionyesha kuwa moja ya taarifa ya ukaguzi inaonekana Marijani Saleh alisaini kufikisha vifaa vya Infosys.

Vifaa hivyo, vinaelezwa vilifikishwa Machi 2, 2012. Katika Nyaraka hiyo upande wa Jeshi la Polisi alisaini ofisa mmoja wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Nestory Tagaya na mdau mwingine kutoka kampuni ya BioLink alikuwa Pierson J.

Taarifa iliyotolewa na PAC hivi karibuni ilionyesha kuwa kampuni ya Lugumi ilingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa kazi hiyo ya kufunga mitambo hiyo kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima na kulipwa fedha zote huku kazi ikiwa haijafanyika.

PESA KIFISADI ZILIZOFICHWA USWISSI-GENEVA, AZOSEMWA MH. ZITTO KABWE ZIMEFIKIA WAPI? ZINARUDISHWA LINI AU MHESHIMIWA MKUU WA KAYA HAJAKUMBUSHWA?
 
Kumpata kiongozi msafi ccm ni ngumu kama kumtafuta mwanamke bikra wodi ya akina mama wanaojifungua.
 
Nina uhakaika asilimia 100% Mkurugenzi wa NIDA siyo mmoja ya wamiliki wa infosys. Ndiyo, Kitwanga ni mmoja ya shareholder wa infosys IPS Ltd. Kampuni ya infosys IPS Ltd ni moja ya kampuni chache za IT zenye ufanisi mkubwa na uadilifu ktk utendaji. Ni kampuni ambayo hutimiza ahadi siku zote. Infosys IPS Ltd imewahi kufanya miradi mikubwa sana na wateja kama wizara ya fedha, TRA etc, na kote huko haikuwahi kuchelewesha kazi. Tusubiri naamini kukatakuwa na sababu za kwa nini Lugumi walichelewa au wamechelewa kutekeleza mradi. Hivyo infosys IPS Ltd na Charles Kitwanga ni kampuni safi na Mh. Charles Kitwanga ni muadilifu na mchapa kazi.

Hii kazi uliyopewe utaiweza kweli, mbona Kama wamekutwisha gunia la misumari ukimbie nalo.?
 
~~>Jipu litaweza kutumbua Jipu¿¿¿¿¿

Hii nchi inahitaji kuRestart.....
 
Sasa hivi ni muda muafaka Bunge kuonyesha Meno yake...ujinga wa kutetea serikali ufe kabisa .
 
Yaani hii nchi! Kumbe sasa Magu anasikiliza Kitwanga kwenye teuzi zake, ndio amemshauri jamaa wa NIDA ambae ni partner wake......ili aje atoe tender kwenye kampuni yao tena! Na Kitwanga azibe mianya yote ya info kuvuja kuhusu ile project ya vituo vya polisi! Daaaaa Magu una kazi sana! Sasa utabadilisha baraza mapem hivi! Maana sababu zinaongezeka! JM na Kitwanga! Haiwezekani awepo pale tena!
 
WAZIRI WA MAGUFULI KTK KASHFA YA UFISADI NA POLISI

- Kampuni inayohusishwa naye ya Infosys ilikuwa mkandarasi

Yadaiwa Infosys inamilikiwa na Kitwanga na Mkurugenzi Mkuu NIDA

Ni mdau wa LUGUMI enterprises

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34, imeelezwa.

Kuhusika huko kwa Waziri Kitwanga imekuja siku moja, baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) kueleza kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye mkataba ulioingia kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

Taarifa za kuaminika ilizozipata gazeti hili, zimeeleza kuwa Waziri Kitwanga anahusika kupitia kampuni yake ya Infosys anayomiliki pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyo chini ya Wizara hiyo hiyo.

Jeshi la Polisi limekumbwa na kashfa kubwa ya manunuzi ya vifaa vya kuhifadhi alama za vidole ambapo Kamati ya PAC imegundua kuwa kampuni ya Lugumi Enterprises haikutekeleza mkataba ipasavyo.

Kampuni hiyo ililipwa sh. bilioni 34 na jeshi la polisi ili kusambaza vifaa hivyo nchi nzima katika vituo 138 vya polisi lakini ni vituo 14 vilivyopata vifaa hivyo.

Gazeti hili limegundua kuwa moja ya kampuni iliyopewa kazi hiyo ni Infsosys ambayo nakala za msajili wa makampuni inaonyesha kuwa inamilikiwa na Charles Kitwanga na Dk. Modestus Francis Kipilimba, ambaye ni Mkurugenzi wa NIDA.

Nyaraka za uchunguzi ikiwemo mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Infosys ambazo gazeti hili imeziona inaonyesha kuwa Kampuni hiyo ya Waziri Kitwanga ilifanya kazi ya kuunganisha internet kati ya vituo vya polisi na mkonga wa taifa.

Kazi ambayo haikufanyika kabisa kwani mpaka sasa ni vituo 14 tu vya polisi viliunganishwa, ambapo baadhi ya taarifa ilizozipata gazeti hili zilionyesha kuwa moja ya taarifa ya ukaguzi inaonekana Marijani Saleh alisaini kufikisha vifaa vya Infosys.

Vifaa hivyo, vinaelezwa vilifikishwa Machi 2, 2012. Katika Nyaraka hiyo upande wa Jeshi la Polisi alisaini ofisa mmoja wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Nestory Tagaya na mdau mwingine kutoka kampuni ya BioLink alikuwa Pierson J.

Taarifa iliyotolewa na PAC hivi karibuni ilionyesha kuwa kampuni ya Lugumi ilingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa kazi hiyo ya kufunga mitambo hiyo kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima na kulipwa fedha zote huku kazi ikiwa haijafanyika.
Kwa hali hii Prezida Magu ana kazi ya ziada kupata watu safi ndani ya serikali yake. Kupata mtu safi ndani ya ccm ni sawa na kutafuta bikira kwenye wodi ya wazazi!
 
ccm hakuna msafi,,na kama tunategemea kuna jipya litaletwa na ccm chini ya magufuli tunajidanganya
 
Kuamini kuwa walioteuliwa kulisukuma gurudumu la serikali ya awamu ya tano ni wasafi tunanajidanganya. Hawa wana nafuu au yao bado yapo nyuma ya pazia. Tuwaacha wafanye kazi, hakuna mbadala. Kumpata asie na doa ndani ya system iliyokuwepo ni sawa na kumpa daktari kazi ya kumtafuta bikira kwenye foleni ya dada poa walionaswa usiku wa manane.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom