Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34

Status
Not open for further replies.

yves

Member
Apr 9, 2016
17
21
WAZIRI WA MAGUFULI KTK KASHFA YA UFISADI NA POLISI

- Kampuni inayohusishwa naye ya Infosys ilikuwa mkandarasi

Yadaiwa Infosys inamilikiwa na Kitwanga na Mkurugenzi Mkuu NIDA

Ni mdau wa LUGUMI enterprises

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga atajwa kuhusika na kashfa ya ufisadi katika Jeshi la Polisi ya sh. bilioni 34, imeelezwa.

Kuhusika huko kwa Waziri Kitwanga imekuja siku moja, baada ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali(PAC) kueleza kuwa kuna ufisadi mkubwa kwenye mkataba ulioingia kati ya Jeshi la Polisi Nchini na Kampuni ya Lugumi Enterprises.

Taarifa za kuaminika ilizozipata gazeti hili, zimeeleza kuwa Waziri Kitwanga anahusika kupitia kampuni yake ya Infosys anayomiliki pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyo chini ya Wizara hiyo hiyo.

Jeshi la Polisi limekumbwa na kashfa kubwa ya manunuzi ya vifaa vya kuhifadhi alama za vidole ambapo Kamati ya PAC imegundua kuwa kampuni ya Lugumi Enterprises haikutekeleza mkataba ipasavyo.

Kampuni hiyo ililipwa sh. bilioni 34 na jeshi la polisi ili kusambaza vifaa hivyo nchi nzima katika vituo 138 vya polisi lakini ni vituo 14 vilivyopata vifaa hivyo.

Gazeti hili limegundua kuwa moja ya kampuni iliyopewa kazi hiyo ni Infsosys ambayo nakala za msajili wa makampuni inaonyesha kuwa inamilikiwa na Charles Kitwanga na Dk. Modestus Francis Kipilimba, ambaye ni Mkurugenzi wa NIDA.

Nyaraka za uchunguzi ikiwemo mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Infosys ambazo gazeti hili imeziona inaonyesha kuwa Kampuni hiyo ya Waziri Kitwanga ilifanya kazi ya kuunganisha internet kati ya vituo vya polisi na mkonga wa taifa.

Kazi ambayo haikufanyika kabisa kwani mpaka sasa ni vituo 14 tu vya polisi viliunganishwa, ambapo baadhi ya taarifa ilizozipata gazeti hili zilionyesha kuwa moja ya taarifa ya ukaguzi inaonekana Marijani Saleh alisaini kufikisha vifaa vya Infosys.

Vifaa hivyo, vinaelezwa vilifikishwa Machi 2, 2012. Katika Nyaraka hiyo upande wa Jeshi la Polisi alisaini ofisa mmoja wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Nestory Tagaya na mdau mwingine kutoka kampuni ya BioLink alikuwa Pierson J.

Taarifa iliyotolewa na PAC hivi karibuni ilionyesha kuwa kampuni ya Lugumi ilingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa kazi hiyo ya kufunga mitambo hiyo kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima na kulipwa fedha zote huku kazi ikiwa haijafanyika.
 
Hi ni shida sana lakini haistui maana mbea mwenyewe yupo karibu nae,kwahyo ni kuharibiana dili tu hii serikali ya magu nayo khaaar.!!!!@???
 
Kwa hiyo Waziri na DG wa Nida Ni maparter ndio maana Rahisi kaenda Kupumzika maana DG wa Nida na Waziri wa mambo ya ndani Wote majipu makubwa yaliyo hiva. Da masifa yote kumbe amnna lolote. Magazeti haliyo yatumia kuwachafua wafanyakazi wa Nida waliofukuzwa kama mbwa na kutopewa stahiki zao yamemchafua yeye. Da amakweli malipo hapa hapa Duniani mbinguni esabu.
 
Aisee ...hii ni hatari..sana hivi huyo kipilimba si ndo aliwafukuza wale vijana wa nida bila kuwalipa stahiki zao na uzi umeshatolewa humu ....au ndo hela na jasho la hao vijana ndo alikua anaendeshea kampun yake hio na mwenzie..Chozi la mnyonge haliendi bure.
 
Yetu macho na masikio. Kumpata mtu safi kwenye system ya Ccm ni sawa na kutaka mwanamume abebe ujauzito.

Tumeshindwa kwny Uchaguzi Mkuu kutokana na kukithiri vitendo cha Rushwa ndani ya Chama pamoja na ukosefu wa nidhamu-Freeman Aikael Mbowe Mwenyekit wa Chadema Taifa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom