Chapisho la Mungu na Shetani

mcshonde

Member
Jul 15, 2022
66
152
Kuna chapisho linaitwa "satan the servant of God", wengi walitaka kujua mwandishi kaongelea nini humo ndani, ni mengi...ila point ni kwamba Shetani amekuwa akitumika na Mungu mara kwa mara ili kuwachambua walio wake na wasio wake.

Kwamba mwamba amekuwa akitumwa hapa na pale na anawekewa mipaka. Wengi wanauliza kwanini Mungu asimkatilie mbali tu mwamba na maisha yawe smooth?

Jibu linaendana na maisha yetu ya hapa duniani...kwamba hakuna anayependa kuwa na kundi kubwa la watu wasiomkubali..wasiompenda WANAFIKI.

Hata Nabii Yesu mwenyewe alitoa mfano wa mfalme na karamu yake alialika watu wakapotelea mitiniaakaamua aalike maskini...wa mtaani..wakapiga msosi na wakashukuru kinoma.

Sasa kulingana na teolojia, Mungu anamtumia shetani kuwachuja watu wale watakaoingia kula vinono na michuzi chuzi (joke) na wale wataokaa upande wa mbuzi na giza nene.
 
Kwanza ufahamu kuwa Mungu ameumba cause and effect....kila jambo huwa lina matokeo yake aidha yawe hasi ama chanya!!

Ukitenda jambo jema malipo yake yatakuwa si mengine bali ni mema.

Ukitenda maovu hutapata matokeo mengine ila uovu ulioupanda.

Huwezi ukapanda mbegu ya mahindi ukategemea uvune mapapai. Huo ndio utaratibu ambao Mungu ameuweka katika ulimwengu huu.

Nikija katika hoja yako ya kwanza inayosema

" Shetani amekuwa akitumika na Mungu mara kwa mara ili kuwachambua walio wake na wasio wake"

Mungu ni mmiliki wa elimu na ujuzi wote tunaoujua na tusioujua.Mungu anajua yaliyopita kabla ya mwanadamu kuumbwa na yajayo baada ya mwanadamu kuumbwa,kuzaliwa,kufa na mpaka kufufuliwa. Adui mkubwa wa mwanadamu ni nafsi yake mwenyewe. Yaani nafsi ndio inauwezo wa kuchagua mema au mabaya. Shetani huwa anaichochea tu nafsi ili ifanye mabaya kwa upesi ila asili kubwa ya nafsi ni kupenda mambo mabaya/ukaidi/uasi.

Mungu hapendi uasi na kufuru. Hilo lieleweke wazi.Ila katika ulimwengu huu ameacha haya yafanyike ili kila mtu alipwe kutokana na alichokichagua.Kama mwanadamu kwa hiari yako uliamua kumfuata na kumsikiliza shetani basi hutalipwa isipokuwa kwa yale uliyoyachuma na ikiwa uliamua kumfuata Mungu na kuyatenda anayoyapenda na kuyaridhia basi hutalipwa isipokuwa kwa yale uliyoyachuma..

Mungu hamtumi shetani kwenda kuchochea uasi au dhambi kwa wanadamu isipokuwa ninyi wanadamu wenyewe ndio huwa mnamualika shetani aje kuwachochea kufanya mabaya. Nafsi ovu ni mshirika wa Shetani.
 
"Kwamba mwamba amekuwa akitumwa hapa na pale na anawekewa mipaka. Wengi wanauliza kwanini Mungu asimkatilie mbali tu mwamba na maisha yawe smooth?"

Mwanadamu kupitia nafsi yako mwenyewe ndio unajiwekea mpaka kati yako na Shetani. Ili Mungu akulinde dhidi ya kazi za Shetani ni lazima nafsi yako kwanza imkatae shetani na imfanye kuwa ni adui. Pindi ukifanya hivyo ina maana kuwa umechagua kuwa upande wa Mungu. Hakuna namna ya kumzuia Shetani asiwe pamoja nawe kama hujachagua kuwa pamoja na Mungu. Ukiwa pamoja na Mungu ndio unaweza sasa ukapata ulinzi wa ziada kutoka kwa Mungu ili umzuie shetani.!!

Mungu hapendi uasi, kufuru, uovu na dhambi. Wala hamtumi shetani aje kuwapotosha watu ila watu wamekuwa wakijipotosha wenyewe na nafsi zao kwa kuamua kuwa pamoja na shetani.

Mungu ni mwema wakati wote.
 
Shetani ni mtihani miongoni mwa mitihani aliyoumbiwa mwanadamu hapa duniani.

Miongoni mwa mitihani aliyoumbiwa mwanadamu ukiachana na nafsi yake ni...

Wanawake
Watoto
Mali
Pombe n.k

Ili hivyo vitu vikupoteze ni lazima nafsi yako yenyewe ikubali kupotea.
 
Back
Top Bottom