Chanzo moto ulioteketeza maduka Njombe ni jiko la mkaa, walitumia kupunguza baridi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Baada ya moto kuteketeza maduka Matano na ghala za kuhifadhia bidhaa za maduka yaliyopo katikati ya Mji wa Njombe imebainika kuwa chanzo ni moto uliokuwa katika jiko la mkaa ambao ulitumika kwa ajili ya kupunguza baridi.

Inspekta Lotma Dauda ambaye ni Afisa Oparesheni la Zimamoto na Uokoaji Njombe amesema: “Kulikuwa na kigae cha moto walikuwa wakioa ndani sababu ya baridi, walipotoka wakasahau kuzima, hivyo, moto ukadaka pikipiki na ndiyo yakatokea yaliyotokea.”

Katika tukio hilo wamiliki wa baadhi ya maduka yaliyoteketea kwa moto wamesikitishwa na kitendo cha wananchi waliojitokeza kama waokoaji na badala yake kutokomea na bidhaa.

Chanzo: Azam TV
 
Moto kwenye jiko la mkaa hausambai unabaki ndani ya jiko. Hatari pekee ya kulala na jiko la mkaa ni kufa usingizini kwasababu ya CO tu.
 
Duuh, watu wamesepa na bidhaa, sasa hivi ni kusubiri tu watu wafe au waumie wahuni wa kutupwa wapite na ulichonacho.
 
Back
Top Bottom