PRODA LTD
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,005
- 1,333
.
Chanzo kikubwa cha baadhi ya matatizo tuliyonayo leo kinaweza kuwa ni maneno tunayopenda kuongea ongea?
Unaweza kuwa unapambana kweli kwenye ndoa yako ila mambo hayaendi. Au unapambana kweli kuwatoa baadhi ya watu moyoni mwako ila umeshindwa. Au vitu kwenye maisha yako haviendi tu vile unataka viende.
Sasa, hivi unakumbuka maneno ulokuwa unakiri kwa kinywa chako kwenye mahusiano yote ulowahi kuwa nayo? Pale mapenzi yanapokuwa moto moto huwa ni wepesi mno kuacha vinywa vyetu vikiri maneno, tena hupenda kuongea kwa kingereza kabisa "I can't live without you" "I will love you forever" "I will never let you go" "You are my everything".
Na pale inapotokea mmeachana nini kinatokea? Bado unabaki unadaiwa ukiri wa maneno ya kinywa chako. Matokeo yake....hata ulimwengu wa roho unachanganyikiwa sasa....umewahi kuwa na wapenzi watano huko nyuma na wote ulikuwa ukiwaambia maneno hayo hayo... those words are following you my dear..unadaiwa. Those are soul ties bound by your own words.
Unauliza imeshatokea, nifanyeje?
Hujachelewa. Mungu ni wa rehema mno. Tubu....tubu... Na tena tubu => Nenda mbele za Mungu, jisafishe wewe mwenyewe na maneno yote unayodaiwa popote pale => Uwe mwangalifu na maneno yote yanayotoka kinywani mwako. Neno la Mungu linasema utatoa hesabu kwa kila neno likokalo kwenye kinywa chako. (Mathayo 12:36)
Na mwisho kabisa na muhimu mnoo.... Kuwa na mahusino ynayomtukuza Mungu. Kwenye njia zinazompendeza yeye..
Baraka za Bwana ziambatane na wewe