Chanzo cha vita ya India na Pakistan inayoendelea hivi leo katika eneo la Kashmir

Chanzo cha vita ya India na Pakistan inayoendelea hivi leo katika eneo la Kashmir

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,563
Reaction score
7,321
Mwezi wa huu wa Mei mwaka 2025, ulimwengu umetikiswa na mgogoro mpya kati ya mataifa mawili yenye historia ndefu ya mvutano – India na Pakistan. Tarehe 6 Mei, India ilitangaza operesheni kali iliyobeba jina "Operation Sindoor," ikilenga maeneo tisa ndani ya Pakistan na kipande cha eneo la Kashmir linaloendeshwa au kudhibitiwa na serikali ya Pakistan. Hii ilikuwa hatua ya kulipiza kisasi kufuatia shambulio baya la kigaidi lililotokea tarehe 22 Aprili 2025 katika eneo la Pahalgam, katika mji wa Kashmir, ambapo watu 26, wengi wao wakiwa watalii wa Kihindu, walipoteza maisha.

India iliamua kuchukua hatua kali dhidi ya makundi ya kigaidi kama Lashkar-e-Taiba na kundi la Jaish-e-Mohammed, yaliyoshutumiwa kwa kupanga mashambulizi hayo ambayo yaliua watu 26 katika mji huo. Ambapo Mashambulizi ya anga na makombora yalifanyika kwa lengo la kuharibu miundombinu ya kigaidi. Wizara ya Ulinzi ya India ilieleza kwamba operesheni hiyo ilikuwa "imepangwa kwa uangalifu, isiyolenga kusababisha vita vikubwa." Hata hivyo, taarifa kutoka Pakistan zilidai kuwa mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya raia, akiwemo wanawake na watoto, na kuharibu misikiti na majengo mengine yasiyo ya kijeshi.



Pakistan Yajibu kwa Hasira

Baada ya mashambulizi hayo, Pakistan haikusita kujibu. Jeshi la nchi hiyo lililipa kisasi kwa kushambulia maeneo ya mpaka wa Line of Control (LoC) yanayodhibitwa na serikali ya India kwa mizinga, na kusababisha vifo vya raia watatu wa India. Kwa upande mwingine, Pakistan ilidai kuwa imefanikiwa kuangusha ndege kadhaa za kivita za India, zikiwemo aina ya Rafale, Sukhoi Su-30, na MiG-29, pamoja na ndege isiyo na rubani. India ilikubali kupoteza ndege tatu lakini ilikanusha ukubwa wa madai ya Pakistan.

Wakati huo huo, serikali ya Pakistan iliita mashambulizi ya India kuwa ni "kitendo cha vita" na kuomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati haraka.

Kwa wasiojua labda maana ya Line of Control, huu ni mpaka uliotengwa kutenganisha mamlaka mbili zinazotawala eneo la Kashmir zisiingiliane kiutawala, yani wewe tamba mpaka hatua hizi, nami nitambe hatua hizi. Ikumbukwe eneo la Kashmir ni eneo linalopiganiwa na Nchi mbili. Na hakuna mmiliki rasmi wa eneo hilo. Lakini mamlaka ziliamua kukata katikati na kutenganisha ardhi kwa kila Nchi na eneo la upande wa kaskazini likipewa msaada na uongozi na msaada wa kijeshi chini ya serikali ya Pakistan na eneo la kusini likipokea misaada na uongozi chini ya serikali ya India. Hili kuondoa muingiliano wa kiuongozi, wakaweka mstari unaoonesha mipaka ya kila uongozi unapoishia ambapo ndipo mpaka huo ukaitwa jina la Line Of Control (LoC), ambapo utakiwi kuvuka mstari kwenda kwa mwenzako, kwa namna yoyote iwe kijeshi au kiutawala. Lakini mstari huu sio Mpaka rasmi wa Nchi na Nchi, ni zuio tu la kukataza tawala mbili zisiingiliane kwenye eneo moja, kwa sababu eneo hilo bado linapiganiwa na Nchi mbili, japo China nae anadai kipande kidogo cha ardhi katika eneo hilo hilo. Na kuna kipindi China na India walitunishiana vifua, kila mmoja kuonesha ubabe wake. Picha hapo chini inaonesha maeneo hayo yenye mgogoro wa ardhi.



Ulimwengu Washangazwa, Wakati Hatari Ikiendelea Kuongezeka

Jamii ya kimataifa ilionyesha hofu kubwa kuhusu hali hiyo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alitoa wito wa kujizuia kwa hali ya juu kutoka kwa mataifa yote mawili. Marekani pia iliwasihi India na Pakistan kushiriki mazungumzo badala ya kuendeleza mgogoro. Kutokana na ukweli kwamba mataifa haya mawili yana silaha za nyuklia, hali ya hofu ilienea kote ulimwenguni, ikionyesha hatari ya vita kubwa zaidi.



Historia ya Mgogoro wa Kashmir


Kashmir imekuwa chanzo cha mvutano kati ya India na Pakistan tangu mwaka 1947, baada ya mgawanyiko wa India ya Uingereza. Eneo hili limekuwa likishuhudia vita mara kwa mara, mashambulizi ya kigaidi, na mapigano madogo madogo kati ya majeshi ya nchi hizi mbili. Matukio ya sasa yanafuatia mfululizo wa migogoro inayochochewa na shambulio moja au jingine la kigaidi au kiaskari. Ikumbukwe kuwa India na Pakistan zilikuwa ni eneo moja au kwa lugha rahisi zilikuwa ni Nchi moja iliyokuwa chini ya Miliki ya Koloni la Mwingereza. Mwaka 1947, tarehe 14 Agosti. Siku moja kabla ya Uhuru wa India kutoka kwa Muingereza, Pakistan ilifanikiwa kujitenga na kutengeneza Taifa lake la Pakistan ambapo pia baadae mwaka 1971 Pakistan kwa mara nyingine iligawanyika na kuzaa mataifa mawili, yani Taifa la Pakistan ambalo pia liliitwa Western Pakistan na Taifa la Bangladesh lililokuwa likiitwa Eastern Pakistan huku Taifa mama likiwa ni India. Kisababishi kikuu cha Pakistan kudai uhuru wake kutoka kwa India ni kwa Sababu ya Itikadi za Kidini, maeneo wanayoishi wapakistani na wabangladeshi wa leo yalikuwa yana waumini wengi wa dini ya Kiislamu, huku maeneo ya India yakikaliwa na wakazi wa dini ya Kihindu. Utofauti huu wa kiitikadi za kidini ambao uliathiri maamuzi ya kisiasa ulipelekea Pakistan kujitenga kutoka kwa India na kudai uhuru na kutengeneza taifa lake rasmi la Pakistan (Western Pakistan na Eastern Pakistan ambayo ndio Bangladesh). Sasa wakati wa kujitenga kuna maeneo ambayo ilikuwa ni ngumu kuyatengenisha na moja wapo ni eneo hili la Kashmir. Ambalo Nchi tatu ikiwemo Pakistan na India kama mahasimu wakuu na China kwa mbali wakitaka kusimika utawala kwenye eneo hili ambalo linapatikana kwenye Milima ya Nepal, unapopatikana mlima Everest.

Sasa baada ya India na Pakistan kupewa uhuru na kuwa Nchi huru, eneo la Kashmiri na maeneo jirani yalikuwa bado hayajakabidhiwa kwa nchi zilizopata uhuru. Waingereza wakazungumza na viongozi wa eneo la Kashmir na kuwapa machaguo matatu, ambayo ni wachague kujiunga na Nchi ya Pakistan, au wajiunge na Nchi ya India au wapewe Uhuru wao binafsi hili wawe Nchi huru kama nchi nyingine wajitegemee kila kitu. Viongozi wa eneo la Kashmir wakataka wapewe Uhuru hili wajitawale kama Nchi uhuru. Ambapo Waingereza wakaridhia, lakini baadae Wanamgambo wa kikabila waliokuwa na ushirikiano na Jeshi la Pakistan walivamia eneo hilo na kutaka liwe chini ya utawala wa serikali ya Pakistan. Baada ya vurugu za hapa na pale viongozi wa Kashmir wakaona hapa hatuwawezi hawa wanamgambo wa Pakistan, hivyo wakaenda kuomba msaada wa kijeshi na Silaha za kivita kutoka serikali ya India, ambapo wakasaini mkataba na Jeshi la India kwenda kusaidia Uongozi au Utawala wa eneo la Kashmir na eneo kwa ujumla lisichukuliwe na wanamgambo wa Pakistan. India ikaingilia kati na kichapo kikaanza, ambapo mpaka leo hii eneo hilo halijapata mmiliki halali. India ikiishutumu Pakistan kwa matukio ya kigaidi eneo hilo, huku India ikishutumiwa kwa kufanya mashambulizi ya kushitukiza katika ardhi ya Pakistan.



Mustakabali wa Mgogoro

Hali bado ni tete. Mataifa yote mawili yako katika hali ya tahadhari kubwa, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kuzuia hali kuzorota zaidi. Ingawa wito wa mazungumzo umekuwa ukitolewa, njia ya kufikia suluhu bado ni ngumu na yenye changamoto nyingi.

Kwa ulimwengu, hili ni somo kwamba amani ni jambo la thamani linalopaswa kulindwa kwa juhudi za pamoja. Mashariki ya Kusini mwa Asia inasimama kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa, lakini swali ni, je, amani itapata nafasi?

region-Kashmir-India.jpg
 
Mwezi wa huu wa Mei mwaka 2025, ulimwengu umetikiswa na mgogoro mpya kati ya mataifa mawili yenye historia ndefu ya mvutano – India na Pakistan. Tarehe 6 Mei, India ilitangaza operesheni kali iliyobeba jina "Operation Sindoor," ikilenga maeneo tisa ndani ya Pakistan na na kipande cha eneo la Kashmir linaloendeshwa na serikali yan Pakistan. Hii ilikuwa hatua ya kulipiza kisasi kufuatia shambulio baya la kigaidi lililotokea tarehe 22 Aprili 2025 katika eneo la Pahalgam, katika mji wa Kashmir, ambapo watu 26, wengi wao wakiwa watalii wa Kihindu, walipoteza maisha.

India iliamua kuchukua hatua kali dhidi ya makundi ya kigaidi kama Lashkar-e-Taiba na kundi la Jaish-e-Mohammed, yaliyoshutumiwa kwa kupanga mashambulizi hayo ambayo yaliua watu 26 katika mji huoo. Ambapo Mashambulizi ya anga na makombora yalifanyika kwa lengo la kuharibu miundombinu ya kigaidi. Wizara ya Ulinzi ya India ilieleza kwamba operesheni hiyo ilikuwa "imepangwa kwa uangalifu, isiyolenga kusababisha vita vikubwa." Hata hivyo, taarifa kutoka Pakistan zilidai kuwa mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya raia, akiwemo wanawake na watoto, na kuharibu misikiti na majengo mengine yasiyo ya kijeshi.



Pakistan Yajibu kwa Hasira

Baada ya mashambulizi hayo, Pakistan haikusita kujibu. Jeshi la nchi hiyo lilishambulia maeneo ya mpaka wa Line of Control (LoC) kwa mizinga, na kusababisha vifo vya raia watatu wa India. Kwa upande mwingine, Pakistan ilidai kuwa imefanikiwa kuangusha ndege kadhaa za kivita za India, zikiwemo aina ya Rafale, Sukhoi Su-30, na MiG-29, pamoja na ndege isiyo na rubani. India ilikubali kupoteza ndege tatu lakini ilikanusha ukubwa wa madai ya Pakistan.

Wakati huo huo, serikali ya Pakistan iliita mashambulizi ya India kuwa ni "kitendo cha vita" na kuomba Umoja wa Mataifa kuingilia kati haraka.

Kwa wasiojua labda maana ya Line of Control, huu ni mpaka uliotengwa kutenganisha mamlaka mbili zinazotawala eneo la Kashmir zisiingiliane kiutawala. Ikumbukwe eneo la Kashmir ni eneo linalopiganiwa na Nchi mbili. Na hakuna mmiliki rasmi wa eneo hilo. Lakini mamlaka ziliamua kukata katikati na eneo la upande wa kaskazini likipewa msaada na uongozi chini ya serikali ya Pakistan na eneo la kusini likipokea misaada na uongozi chini ya serikali ya India. Hili kuondoa muingiliano wa kiuongozi, wakaweka mstari unaoonesha mipaka ya kila uongozi ambapo ndipo ujapewa jina la Line Of Control (LoC), ambapo utakiwi kuvuka mstari kwenda kwa mwenzako. Lakini mstari huu sio Mpaka rasmi wa Nchi na Nchi, ni zuio tu la kujataza tawala mbili zisiingiliane kwenye Eneo moja, kwa sababu eneo hilo bado linapiganiwa na Nchi mbili, japo China nae anadai kipande kidogo cha ardhi katika eneo hilo hilo.



Ulimwengu Washangazwa, Wakati Hatari Ikiendelea Kuongezeka

Jamii ya kimataifa ilionyesha hofu kubwa kuhusu hali hiyo. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, alitoa wito wa kujizuia kwa hali ya juu kutoka kwa mataifa yote mawili. Marekani pia iliwasihi India na Pakistan kushiriki mazungumzo badala ya kuendeleza mgogoro. Kutokana na ukweli kwamba mataifa haya mawili yana silaha za nyuklia, hali ya hofu ilienea kote ulimwenguni, ikionyesha hatari ya vita kubwa zaidi.



Historia ya Mgogoro wa Kashmir


Kashmir imekuwa chanzo cha mvutano kati ya India na Pakistan tangu mwaka 1947, baada ya mgawanyiko wa India ya Uingereza. Eneo hili limekuwa likishuhudia vita mara kwa mara, mashambulizi ya kigaidi, na mapigano madogo madogo kati ya majeshi ya nchi hizi mbili. Matukio ya sasa yanafuatia mfululizo wa migogoro inayochochewa na shambulio moja au jingine la kigaidi au kiaskari. Ikumbukwe kuwa India na Pakistan zilikuwa ni eneo moja au kwa lugha rahisi zilikuwa ni Nchi moja iliyokuwa chini ya Miliki ya Koloni la Mwingereza. Mwaka 1947, tarehe 14 Agosti. Siku moja kabla ya Uhuru wa India kutoka kwa Muingereza, Pakistan ilifanikiwa kujitenga na kutengeneza Taifa lake la Pakistan ambapo pia baadae mwaka 1971 Pakistan kwa mara nyingine iligawanyika na kuzaa mataifa mawili, yani Taifa la Pakistan na Taifa la Bangladesh huku Taifa mama likiwa ni India. Kisababishi kikuu cha Pakistan kudai uhuru wake kutoka kwa India ni kwa Sababu ya Itikadi za Kidini, Maeneo wanayoishi wapakistani wa leo yalikuwa yana waumini wengi wa Kiislamu, huku maeneo ya India yakikaliwa na wakazi wa dini ya Kihindu. Utofauti huu wa kiitikadi za kidini ambao uliathiri maamuzi ya kisiasa ulipelekea Pakistan kujitenga kutoka kwa India na kudai uhuru na kutengeneza taifa lake. Sasa wakati wa kujitenga kuna maeneo ambayo ilikuwa ni ngumu kuyatengenisha na moja wapo ni eneo hili la Kashmir. Ambalo Nchi tatu ikiwemo Pakistan na India kama mahasimu wakuu na China kwa mbali wakitaka kusimika utawala kwenye eneo hili ambalo linapatikana kwenye Milima ya Nepal, unapopatikana mlima Everest.

Sasa baada ya India na Pakistan kupewa uhuru na kuwa Nchi huru, eneo la Kashmiri na maeneo jirani yalikuwa bado hayajakabidhiwa kwa nchi zilizopata uhuru. Waingereza wakazungumza na viongozi wa eneo la Kashmir na kuwapa machaguo matatu, ambayo ni wachague kujiunga na Pakistan, au wajiunge na India au wapewe Uhuru wao binafsi hili wawe Nchi huru kama nchi nyingine. Viongozi wa eneo la Kashmir wakataka wapewe Uhuru hili wajitawale kama Nchi uhuru. Ambapo Waingereza wakaridhia, lakini baadae Wanamgambo wa kikabila waliokuwa na ushirikiano na Jeshi la Pakistan walivamia eneo hilo na kutaka liwe chini ya utawala wa serikali ya Pakistan. Baada ya vurugu za hapa na pale viongozi wa Kashmir wakaenda kuomba msaada wa Jeshi na Silaha za kivita kutoka serikali ya India, ambapo wakasaini mkataba wa Jeshi la India kwenda kusaidia Uongozi wa Kashmir na Eneo kwa ujumla lisichukuliwe na wanamgambo wa Pakistan. India ikaingilia kati na kichapo zikaanza, ambapo mpaka leo hii eneo hilo halijapata mmiliki halali. India ikiishutumu Pakistan kwa matukio ya kigaidi eneo hilo, huku India ikishutumiwa kwa kufanya mashambulizi ya kushitukiza.



Mustakabali wa Mgogoro

Hali bado ni tete. Mataifa yote mawili yako katika hali ya tahadhari kubwa, huku juhudi za kidiplomasia zikiendelea kuzuia hali kuzorota zaidi. Ingawa wito wa mazungumzo umekuwa ukitolewa, njia ya kufikia suluhu bado ni ngumu na yenye changamoto nyingi.

Kwa ulimwengu, hili ni somo kwamba amani ni jambo la thamani linalopaswa kulindwa kwa juhudi za pamoja. Mashariki ya Kusini mwa Asia inasimama kwenye ukingo wa mabadiliko makubwa, lakini swali ni, je, amani itapata nafasi?

View attachment 3326669
Haki haiki haki ndio huzaa Amani
 
Mmmh mbona hapa kuna ukakasi pakistani kugawanyika na kuzaa Pakistani na Bangladesh.ukiangalia kwenye raman Pakistani na Bangladesh hawana mpka wowote wanaoshare basi kuna bahari so inawezekana vipi hapo
😀😀nimewaza sana hili
 
Mmmh mbona hapa kuna ukakasi pakistani kugawanyika na kuzaa Pakistani na Bangladesh.ukiangalia kwenye raman Pakistani na Bangladesh hawana mpka wowote wanaoshare basi kuna bahari so inawezekana vipi hapo
Shida yako wewe utaki kutafuta Maarifa, Pakistan sio nchi moja ya kwanza kuwa hivyo.... kwani mbona Palestina ambayo inaunganishwa na Gaza na West Bank ni nchi moja lakini maeneo ya Gaza na West Bank hayajaungana kujiografia... au Ramani ilikupita Kushoto....

Maeneo mawili yaliyombali yanaweza kuwa chini ya Nchi moja au kutawaliwa na Nchi moja bila kujali katikati kiunganishi ni kipi, inaweza kuwa Bahari au Nchi nyingine... hiyo hapo picha inayoonesha Pakistan ikiwa eneo moja na Bangladesh

DS-3a-08-04-2023.jpg


Au angalia hii ya Palestina ambayo West Bank na Gaza hazijaungana ila ni Nchi moja

palestine_en.png
 
Shida yako wewe utaki kutafuta Maarifa, Pakistan sio nchi moja ya kwanza kuwa hivyo.... kwani mbona Palestina ambayo inaunganishwa na Gaza na West Bank ni nchi moja lakini maeneo ya Gaza na West Bank hayajaungana kujiografia... au Ramani ilikupita Kushoto....

Maeneo mawili yaliyombali yanaweza kuwa chini ya Nchi moja au kutawaliwa na Nchi moja bila kujali katikati kiunganishi ni kipi, inaweza kuwa Bahari au Nchi nyingine... hiyo hapo picha inayoonesha Pakistan ikiwa eneo moja na Bangladesh

View attachment 3327056

Au angalia hii ya Palestina ambayo West Bank na Gaza hazijaungana ila ni Nchi moja

View attachment 3327062
lakini alichouliza mdau tofauti na mfano uliotoa Gaza na westbank mwanzo zilikuwa zimeungana kabla ya muisrael kutwaa maeneo na kuzitenganisha mipaka inayo tambuliwa na umoja wa mataifa zimeungana
 
Back
Top Bottom