Chanzo cha vifo vingi: Ajari ya wanafunzi wa Arusha

Chanzo cha vifo vingi: Ajari ya wanafunzi wa Arusha

Suala la uɓovu na tatizo la hao wanaosimamia watoto kwenye hizo school bus lishemwa sana humu ,ƙuwa magari mengi mabovu ,watoto wanajazwa sana ila wahusiƙa wakawa ƙimya

Ni kweli wahusika hujifanya wanawajibika pale tu yakitokea matukio ya namna hii, lakini kama ungekuwepo utaratibu wa kuwawajibisha kila litokeapo tatizo basi akili ya kuwajibika wakati wote ingewaingia kichwani, ila kwa sasa ni ngumu kwakuwa mfumo wa kuwajibishana haupo
 
Naunga mkona hoja! Haya magari nayo Trafiki wawe wanayakagua kama mabasi sasa,inauma sana.
 
Traffic wako busy kujisifia mapato yameongezeka kutokana na fine za barabara huko ajali kama hizi zikitokea...shame.
 
Kuficha nyuso ipogolo vifunikio vilikuwa havitoshi
Asante Baba mkubwa. Huku kwetu Iringa tunafanya kufunika mzoga wa mnyama uliokufa barabarani (sio mbwa lakini) kwa ishara ya kutoa nuksi au mkosi. Na ukisha weka majani kuna maneno unanuizia kuomba amani.
 
Wakuu,
Kabla ya yote, natoa pole kwa familia, Ndugu na marafiki waliofikwa na msiba huu katika ajari ya Bus.

Lakini pia nitoe pongezi kwa watanzania wenzangu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiki katika kuwatia moyo na kuwapa pole wafiwa.

Ni kweli tujuavyo kwamba ajari haiepukiki lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuna baadhi ya ajari zinaepukika.

Kwa utafiti mdogo niliyo ufanya nimegundua baadhi ya mambo ambayo yamepelekea kutokea kwa vifo vingi vya wanafunzi hawa.

1. SEAT BELT
Kuna kila dalili Bus haikuwa na seat belts, na hata kama ilikuwepo wanafunzi hawakufunga ile mikanda. Ukiangalia mwonekano wa Bus, sehemu kubwa iliyopondeka ni sehemu ya Mbele na karibia robotatu ya Bus halijapondeka Sana. Sasa kama kila mwanafunzi angekuwa kafunga mkanda wanafunzi waliokaa siti za nyuma wengi wangepona.

Kwa sababu hakukuwa na seat belt ilipelekea wanafunzi na walimu wao wote kulushwa mbele ya gari baada ya gari kukita kwenye kolongo.

2.UZEMBE WA DEREVA
Kuna kila dalili palikuwa na uzembe. Dereva alikuwa speed kubwa na gari likamshinda kwenye kona ukizingatia na ubichi wa barabara kutokana na mvua zinazoendelea.

OMBI LANGU:
wazazi/Waalimu tuwe makini muda wote na hawa watoto wetu hasa kwenye hizi School Bus, kuna ka tabia ka kulundika watoto, unakuta seat ya watu wawili watoto wamewekwa wanne. Inapelekea watoto kushindwa kufunga mikanda.

Mungu atusaidie!
8a011719fea1b973d9ac74c8002f2051.jpg
fe04d97ef12d6ec7e4ef29725cd21e07.jpg

Swala muhimu la kujiuliza.

Hili basi lilipita vituo vya traffic corps vingapi?
 
Huo ndio ukweli mchungu. Hili suala la seat belt ni la kuangalia kwa makini kuepusha vifo vya uzembe wakati mwingine.
 
Naunga mkono hoja.Kuna haja ya kuwa na umakini wa ziada katika kuajiri madereva wa school bus.Dereva inafaa awe na umri wa makamo kuanzia miaka 40 na kuendelea na awe na uzoefu.
Ila saa zingine hizi shule zinakodisha dala dala lolote zinapotokea school trips.Na tunajua wazimu wa madereva dala dala.

Na Pia itasaidia sana kama wazazi wataweka vipingamizi pale watakapo ona hao maderva hawafai. Yaani nguvu zitoke kila upande.
Hata mabasi ya mikoani inatakiwa abiria wasipande wanapo jua basi fulani linaendeshwa na vichaa
 
Trafic wanachoangalia ni mapato....hawakagui hizi gari waone kwann haina mkanda??? Nashauri trafic waliokua njian gari ilipopita wakamatwe....hawakagui magari wao wanajificha machakani tu na mikamera....ina mana wangekagua hii gari wangezuia safari bila mkanda...na haiwezekan gari itoke Arusha mpaka karatu haijakutana na trafic.
 
Kila kukicha maajali, kuna kila dalili madereva wetu hawajui sheria za Bara Bara au wananunua leseni za udereva, rushwa ya kupindukia

I wish waandishi wa habari, wakafanya investigative journalism, kufuatia ajali hizi how easy it is, to buy a licence ?

It will be interesting to watch, I will tune in?

Tuanzie na gari za abiria..
 
Pamoja na kwamba sikuwepo kwenye tukio lakini nilikuwa pamoja na wafiwa kwa kuhuzuni pamoja na kulia pamoja kwa kuwa janga hili ni letu sote.
 
Kuna watu kila kitu wanasema ni mipango ya Mungu, Unaendesha gari umelewa ukianguka ni mpango wa mungu, una-overspeed ujafunga mkanda matairi mabovu ukipiga chini mpango wa mungu, unaendesha unatumia simu likitokea lolote MUNGU, Zingatia sheria barabarani tuache uswahili.
 
Ila kiukweli magari ya shule mie hua nayaona si mazima kiviile.kama mie nyumba ninaishi iko barabarani na mara nyingi utamuona dereva kapakiza watoto lkn anaendesha utadhani kapakia mizigo na mara nyingi hua ni vijana lkn watu wadereva watu wazima ni wastaarabu sana,japo ajali haiepukiki ila umri wa dereva wa mabas ya watoto pia uangaliwe.
 
Watu likishatokea tatizo mnakua na vimaneno sana, kwahiyo magari yote yanapopata ajari hua madereva ni vijana? Mambo mengine hutokea kwa bahati mbaya tu sema impacts zake ni kubwa kama hivyo
Ajali Haina MTU wa makamu, kijana, wala MTU mzima usipende kupotosha watu kwa point isiyo na mashiko..
Wakuu,
Kabla ya yote, natoa pole kwa familia, Ndugu na marafiki waliofikwa na msiba huu katika ajari ya Bus.

Lakini pia nitoe pongezi kwa watanzania wenzangu ambao kwa namna moja au nyingine wameshiki katika kuwatia moyo na kuwapa pole wafiwa.

Ni kweli tujuavyo kwamba ajari haiepukiki lakini kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia kuna baadhi ya ajari zinaepukika.

Kwa utafiti mdogo niliyo ufanya nimegundua baadhi ya mambo ambayo yamepelekea kutokea kwa vifo vingi vya wanafunzi hawa.

1. SEAT BELT
Kuna kila dalili Bus haikuwa na seat belts, na hata kama ilikuwepo wanafunzi hawakufunga ile mikanda. Ukiangalia mwonekano wa Bus, sehemu kubwa iliyopondeka ni sehemu ya Mbele na karibia robotatu ya Bus halijapondeka Sana. Sasa kama kila mwanafunzi angekuwa kafunga mkanda wanafunzi waliokaa siti za nyuma wengi wangepona.

Kwa sababu hakukuwa na seat belt ilipelekea wanafunzi na walimu wao wote kulushwa mbele ya gari baada ya gari kukita kwenye kolongo.

2.UZEMBE WA DEREVA
Kuna kila dalili palikuwa na uzembe. Dereva alikuwa speed kubwa na gari likamshinda kwenye kona ukizingatia na ubichi wa barabara kutokana na mvua zinazoendelea.

OMBI LANGU:
wazazi/Waalimu tuwe makini muda wote na hawa watoto wetu hasa kwenye hizi School Bus, kuna ka tabia ka kulundika watoto, unakuta seat ya watu wawili watoto wamewekwa wanne. Inapelekea watoto kushindwa kufunga mikanda.

Mungu atusaidie!
8a011719fea1b973d9ac74c8002f2051.jpg
fe04d97ef12d6ec7e4ef29725cd21e07.jpg
 
Trafic wanachoangalia ni mapato....hawakagui hizi gari waone kwann haina mkanda??? Nashauri trafic waliokua njian gari ilipopita wakamatwe....hawakagui magari wao wanajificha machakani tu na mikamera....ina mana wangekagua hii gari wangezuia safari bila mkanda...na haiwezekan gari itoke Arusha mpaka karatu haijakutana na trafic.
Wewe unashauri itolewe adhabu gani tofauti na kutozwa faini, maana hata wangekagua hilo gari likakutwa halina mikanda ya usalama kwa abiria, lingetozwa faini na safari ingeendelea hivyo hivyo.

Unakumbuka ya cityboy na tochi ya kuvuka spreed likatozwa faini, lakini mbele likaenda kuua watu???

Unaonaje faini ikiongezeka mpaka laki tatu hivi, au ukishikwa na kosa kama hilo au lingine dereva ufungwe tu mwaka au miezi kadhaa???
 
Back
Top Bottom