Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 661
Una mwanamke sasa ni miezi kadhaa. Pengine una miaka kadhaa pamoja naye. Lakini kuna vitu anavifanya huelewi hujui ufanye nini. Hujui kama uko peke yako au la. Muda mwingi anakua na jeuri, anakudharau na kukupandishia sauti hadi unatamani umpige. Unajihisi huna uhuru tena ukiwa naye. Hutaki ata kuwa naye karibu. Mpaka unahisi anataka kukutawala yeye.
Chanzo kikuu ni kukosa mipaka.
Mipaka inaanzia kwako.
Jinsi unavyojiendesha wewe mwenyewe kama mwanaume. Hauwezi ukamfanya mtu aheshimu mipaka yako kama we mwenyewe huna/ hujui hiyo mipaka. Mipaka yako inaanza kwa kujijua wewe. Unapenda vitu gani, unataka siku yako iweje, unataka kuwa na marafiki aina gani, hutaki kumfanyia mtu kitu gani na yeye hutaki akufanyie kitu gani, nini chanzo cha amani yako, nini kinaondoa amani yako, na maswali kama hayo ndo yatakayoanza kukupa mwanga uwe na mipaka gani.
Mipaka yako ni thamani zako. Mipaka ni picha yako mbele ya jamii. Kama we unatukanwa na mkeo/ mwanamke wako/ na mwanamke yoyote. Picha yako ni mtu unayeburuzwa. Kama wanawake wakikuona wanaongea nawe kwa heshima. Picha yako ni ya mwanaume anayeheshimika.
Kama we hadi watoto wadogo wanakutania matani hadi ya nguoni. Picha yako ni mtu asiyeheshimiwa.
Mipaka pia inashushwa na we mwenyewe. Kwenye kuweka mipaka kuna kile kisauti kinakuambia “naweza nkampoteza huyu mwanamke/ atanionaje/ ataninyima kitu fulani”. Unajikuta unakausha. Unaendelea kuburuzwa lakini moyoni unaumia. Unavumilia. Kadri unavyozidi kuvumilia, ndivyo mipaka yako inavyozidi kuvamiwa.
Mwisho wa siku unajikuta huna mpaka, umeshatekwa na mwanamke. Umewekwa kiganjani. Mwanamke anakua hana wasiwasi na wewe, hakuogopi, anajua chochote anachofanya huwezi mfanya lolote. Japo anaweza kukuambia anahitaji uhuru, lakini haina maana usiweke mipaka.
Ubize, uoga, kukataliwa, au kuchukiwa kusiwe chanzo cha wewe kutokuweka mipaka. Jitahidi kuushinda woga wako. Jitahidi kuvuka mstari uliojiwekea ukiogopa kuharibu mapenzi. Mapenzi yoyote hayana maana kama ni ya kuumizana/ kurudishana nyuma. Hivyo huna sababu ya kuogopa kuchora mipaka yako. Ukisema kitu maanisha. Ukiweka mpaka maanisha.
Kuwa na msimamo. Sio umwambie mwanamke wako/ mkeo kitu alafu baadaye ubadilishe kisa umechuniwa. Au kisa umenyimwa penzi. Au kisa mwanamke ameanza kukuropokea na hutaki/ unaogopa kuzua gumzo. Huo ni ujinga na udhaifu. Wengi wanaoogopa wanawake waliofanikiwa hili ndo jambo linalowashinda. Wanajihisi wadogo mbele yao. Huwa inasikitisha mwanaume anatukanwa na mwanamke mbele ya umati, alafu anajichekesha tu.
Kama mtu hatokubali kuiheshimu mipaka yako basi hastahili muda wako. Na kama we mwenyewe huna mipaka ujue wewe ndiye uliyeruhusu kudharauliwa mana mwanamke wako ameona unamruhusu kufanya hivyo.