Chanzo cha ajali ya chopa iliyombeba Filikunjombe

Cardinal06

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2015
Posts
963
Reaction score
327
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe na wenzake watatu, akiwamo Kepteni William Silaa wamefariki dunia katika ajali ya helikopta, ambazo wataalamu wanasema husababishwa na kosa la kibinadamu la rubani.

Katibu wa Bunge, Thomas Kashilillah alisema jana kuwa walipata taarifa ya ajali hiyo na kuthibitisha kuwa watu wote wanne waliokuwa kwenye helikopta hiyo walifariki dunia.

Miili ya Marehemu Filikunjombe, Kepteni Silaa na wengine iliwasili jijini Dar es Salaam jana jioni kwa helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania, lakini hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu taratibu za mazishi.

Hii ni ajali ya sita ya ndege aina ya helikopta, maarufu kwa jina la chopa, katika kipindi cha miaka miwili huku Filikunjombe, ambaye alikuwa mbunge wa Ludewa kuanzia mwaka 2010, akiwa mgombea wa tano kupoteza maisha tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu uanze.

Mbali na ajali iliyomuhusisha Joshua Nasari mkoani Arusha, nyingine ilitokea Aprili mwaka jana ikimuhusisha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal na kamanda wa Kanda Maalumu ya ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Chopa nyingine ilianguka Februari mwaka jana mkoani Mwanza ikiwa imebeba wanajeshi ambao wote walifariki na nyingine ilianguka Kipunguni Novemba, 2014 ikiwa imebeba marubani watatu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao pia walifariki.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema waliiona chopa hiyo ikiwa umbali wa kilomita nne na baadaye wakaona imeshika moto kabla ya kusikia kishindo kikubwa.

-
Sababu za ajali za chopa

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuelezea chanzo cha ajali iliyochukua maisha ya Filikunjombe na wenzake, lakini Mwananchi iliongea na mtaalamu wa mambo ya ajali za anga kutaka kujua sababu za ajali za chopa.

"Hakuna chopa inayoanguka kwa sababu ya ubovu wake," anasema mtaalamu wa ajali za ndege, John Nyamwiura alipoulizwa na Mwananchi kuhusu chanzo cha ajali za chopa.

"Mara nyingi ajali hizo husababishwa na makosa ya rubani. Ubora wa chopa haujawahi kuwa chanzo cha ajali, chanzo kikubwa ni makosa ya rubani yanayochagizwa na hali ya hewa."

Silaa, baba wa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jiji la Dar es Salaam, Jerry Silaa, ndiye aliyekuwa rubani wa helikopta hiyo iliyoondoka jijini hapa jana jioni kuelekea Ludewa mkoani Iringa.

Hiyo ni ajali ya pili kwa rubani huyo wa kampuni ya General Aviation Services baada ya kunusurika katika ajali nyingine ya chopa iliyotokea mkoani Arusha, akiwa amemchukua mbunge wa Arumeru Mashariki, Nasari na watu wengine.

Katika ajali ya Arusha, rubani huyo alifanikiwa kuipeleka chopa hiyo hadi juu ya mti ambako ilinasa na hivyo kuokoa maisha ya wote waliokuwa kwenye chombo hicho.

Filikunjombe, ambaye alijipatia umaarufu wakati wa sakata la Akaunti ya Escrow mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa makamu mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC).

Alipata umaarufu kutokana na msimamo wake wa kutaka wahusika wote kwenye kashfa hiyo iliyohusisha uchotwaji wa zaidi ya Sh306 bilioni, wachukuliwe hatua, akiwamo Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, ambaye alikuwa wa kwanza kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo, alisema mapema jana kuwa chopa hiyo iliangukia sehemu ambayo si rahisi kuifikia na kuahidi kutoa taarifa zaidi baada ya watu waliotumwa eneo hilo kufika.

Chanzo: Mwananchi
 
Huyo anayejiita mtaalamu wa vyombo vya anga ni muongo,mzandiki na mnafiki wa hali ya juu,haiwezekani hata siku moja eti chopa haiwezi kuanguka kwa matatizo ya engine,kuna engine ambayo huwa haipati hitilafu? Huyu ni mshenzi na pumbavu wa hali ya juu,manina zake *¥§>¥&# anatumika na ccm huyu mtaalamu feki,nasema tena ni muongo na mzandiki mkubwa sana tena hafai,kama ni kosa la rubani huyo rubani anakosa gani la kuendesha ndege hadi ianguke? Wamekodi midege mibovu halafu inaua watu anakuja mshenzi mmoja eti ni kosa la rubani na siyo chopa,shenz zake mjinga huyu,kwa kuwa rubani amekufa na hawezi kujitetea ndo analeta huu ujinga hapa? Au anamaanisha ni kosa la rubani kwa kuwa alikubali kurusha chopa chakavu? Nyambafu ccm!
 
Nimeisoma hiyo story kwenye gazeti la Mwananchi. Nikajiuliza kwanini hawa wanaojiita wataalamu wanatufanye Watanzania wajinga kiasi hicho? Anasoma eti ndege haiwezi kuanguka kwa ubovu mbali makosa ya rubani. Shenz type na mjinga sana huyo mtalaamu
 
Huyo mtaalam aliyesema hivyo ni mzee nguri sana kwenye fani ya usafiri wa anga Afrika mashariki. Nina amini kwa asilimia milioni hajatamka hayo maneno bali ni ule ule umaandazi wa waandishi wetu kushindwa kuhoji wataalam wa fani mbalimbali.
 
Huyu mtaalamu vp afafanue rubani alikuwa spidi kali au anamaanisha nini?kosa lake
 
Nimeisoma hiyo story kwenye gazeti la Mwananchi. Nikajiuliza kwanini hawa wanaojiita wataalamu wanatufanye Watanzania wajinga kiasi hicho? Anasoma eti ndege haiwezi kuanguka kwa ubovu mbali makosa ya rubani. Shenz type na mjinga sana huyo mtalaamu
Hakuna mtaalam hapo ile ya Mwigulu kule Kahama kidogo imfanye kama kaka Njombe na ile ya Lusinde iliyogoma ni rubani?au marubani hawajalipwa!!Kwani ndugu zangu kwa kuwarusha walala hoi hawajambo
 
Mkuu mara nyingi vyombo vya anga huwa havina hitilafu kama za magari. Sio hii tu nishawahi kusoma makala moja ili prove hilo jambo. unaweza usimuelewa lakini endelea kufuatilia. uzembe wa rubani,hali ya hewa,kutunguliwa ama kuhujumiwa.
 
Huyo mtaalam aliyesema hivyo ni mzee nguri sana kwenye fani ya usafiri wa anga Afrika mashariki. Nina amini kwa asilimia milioni hajatamka hayo maneno bali ni ule ule umaandazi wa waandishi wetu kushindwa kuhoji wataalam wa fani mbalimbali.

Hahahahaha eti umaandaz.....kwa hyo kosa ni la mwandish kuandika kwa usahihi alichokisikia au ni mtaalam??
 
Kwa kweli.kusema chopa haiwezi kuanguka kwa hitilafu ya engine ni kujidhalilisha. Kitu kama hujui ni bora kunyamaza. Ina mana engine za chopa zimetoka mbinguni? Huyu atakuwa mtaalamu wa makoroboi. Anataka kumlaumu marehemu. Duh! Ona aibu.
 
Huyo mtaalamu ametoa majibu ya kisiasa. Kwanza kwa uelewa WA kawaida huwezi kuconclude sababu za ajali ya ndege kabla uchunguzi wa kina haujafanyika. Ngoja wataalamu waende eneo la ajali wachunguze na wataleta detailed report ya ajali ambayo itaonyesha chanzo cha ajali.
 
Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe na wenzake watatu, akiwamo Kepteni William Silaa wamefariki dunia katika ajali ya helikopta, ambazo wataalamu wanasema husababishwa na kosa la kibinadamu la rubani.

Hii ni ajali ya sita ya ndege aina ya helikopta, maarufu kwa jina la chopa, katika kipindi cha miaka miwili huku Filikunjombe, ambaye alikuwa mbunge wa Ludewa kuanzia mwaka 2010, akiwa mgombea wa tano kupoteza maisha tangu mchakato wa Uchaguzi Mkuu uanze.

Mbali na ajali iliyomuhusisha Joshua Nasari mkoani Arusha, nyingine ilitokea Aprili mwaka jana ikimuhusisha mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharib Bilal na kamanda wa Kanda Maalumu ya ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.

Chopa nyingine ilianguka Februari mwaka jana mkoani Mwanza ikiwa imebeba wanajeshi ambao wote walifariki na nyingine ilianguka Kipunguni Novemba, 2014 ikiwa imebeba marubani watatu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao pia walifariki.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema waliiona chopa hiyo ikiwa umbali wa kilomita nne na baadaye wakaona imeshika moto kabla ya kusikia kishindo kikubwa.

Sababu za ajali za chopa

Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuelezea chanzo cha ajali iliyochukua maisha ya Filikunjombe na wenzake, lakini Mwananchi iliongea na mtaalamu wa mambo ya ajali za anga kutaka kujua sababu za ajali za chopa.

"Hakuna chopa inayoanguka kwa sababu ya ubovu wake," anasema mtaalamu wa ajali za ndege, John Nyamwiura alipoulizwa na Mwananchi kuhusu chanzo cha ajali za chopa.

"Mara nyingi ajali hizo husababishwa na makosa ya rubani. Ubora wa chopa haujawahi kuwa chanzo cha ajali, chanzo kikubwa ni makosa ya rubani yanayochagizwa na hali ya hewa."

Silaa, baba wa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jiji la Dar es Salaam, Jerry Silaa, ndiye aliyekuwa rubani wa helikopta hiyo iliyoondoka jijini hapa jana jioni kuelekea Ludewa mkoani Iringa.

Hiyo ni ajali ya pili kwa rubani huyo wa kampuni ya General Aviation Services baada ya kunusurika katika ajali nyingine ya chopa iliyotokea mkoani Arusha, akiwa amemchukua mbunge wa Arumeru Mashariki, Nasari na watu wengine.

Katika ajali ya Arusha, rubani huyo alifanikiwa kuipeleka chopa hiyo hadi juu ya mti ambako ilinasa na hivyo kuokoa maisha ya wote waliokuwa kwenye chombo hicho.

Chanzo: Mwananchi

Thanks for this info!.
K
wa ruhusa yako, naomba kuitumia sehemu ya bandiko hili kurutubisha hoja yangu.

P
asco

Huyo mtaalam aliyesema hivyo ni mzee nguri sana kwenye fani ya usafiri wa anga Afrika mashariki. Nina amini kwa asilimia milioni hajatamka hayo maneno bali ni ule ule umaandazi wa waandishi wetu kushindwa kuhoji wataalam wa fani mbalimbali.

Hana cha unguri wala nini!wataalam wa ukweli wanakuambia chopa hyo ilikuwa bomuuu
 
Huyo anayejiita mtaalamu wa vyombo vya anga ni muongo,mzandiki na mnafiki wa hali ya juu,haiwezekani hata siku moja eti chopa haiwezi kuanguka kwa matatizo ya engine,kuna engine ambayo huwa haipati hitilafu? Huyu ni mshenzi na pumbavu wa hali ya juu,manina zake *¥§>¥&# anatumika na ccm huyu mtaalamu feki,nasema tena ni muongo na mzandiki mkubwa sana tena hafai,kama ni kosa la rubani huyo rubani anakosa gani la kuendesha ndege hadi ianguke? Wamekodi midege mibovu halafu inaua watu anakuja mshenzi mmoja eti ni kosa la rubani na siyo chopa,shenz zake mjinga huyu,kwa kuwa rubani amekufa na hawezi kujitetea ndo analeta huu ujinga hapa? Au anamaanisha ni kosa la rubani kwa kuwa alikubali kurusha chopa chakavu? Nyambafu ccm!

Huyo anayejiita mtaalam ni mpumb@v kabisa
 
It is too early kuweza kusema chanzo cha ajali... Hata tungekua na uwezo kiasi gani wa kiuchunguzi na kisayansi

Huyo aliyetoa hiyo taarifa ni mtu wa ajabu sana... Sijui lini tutakua serious
 
Huyo anayejiita mtaalamu wa vyombo vya anga ni muongo,mzandiki na mnafiki wa hali ya juu,haiwezekani hata siku moja eti chopa haiwezi kuanguka kwa matatizo ya engine,kuna engine ambayo huwa haipati hitilafu? Huyu ni mshenzi na pumbavu wa hali ya juu,manina zake *¥§>¥&# anatumika na ccm huyu mtaalamu feki,nasema tena ni muongo na mzandiki mkubwa sana tena hafai,kama ni kosa la rubani huyo rubani anakosa gani la kuendesha ndege hadi ianguke? Wamekodi midege mibovu halafu inaua watu anakuja mshenzi mmoja eti ni kosa la rubani na siyo chopa,shenz zake mjinga huyu,kwa kuwa rubani amekufa na hawezi kujitetea ndo analeta huu ujinga hapa? Au anamaanisha ni kosa la rubani kwa kuwa alikubali kurusha chopa chakavu? Nyambafu ccm!
Matusi yooote uliyotukana umekuja kujijibu mwenyewe mwishoni
 
Back
Top Bottom