Channel ya TBC ya Tanzania Safari ina mapungufu

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
3,052
4,075
Kila nikiangalia hii channel naona inamapungufu lakini naona wasimamizi wanafanya kazi kimazoea ikiwemo swala la kurudia mavipindi yani kipindi kimoja kinaweza kikaoneshwa hadi mara tatu kwa siku

==============

Maoni ya Mdau Mwingine

Hii channel ni ipuuzi tu na nahisi mpaka kufikia sasa imeshatelekezwa, nguvu zote zile kumbe ni zero tu!

Yaani mwaka mzima vipindi ni vile vile, mwaka mzima umeisha vipindi ndo vilevile vilivyorekodiwa,
Kila ukiangalia ni makala zile zile tangu mwaka jana, yaani kipindi kimoja kwa wiki kinarushwa zaidi ya mara10
Sasa kuna haja gani ya kukaa tunaangalia vipindi hivyo hivyo tu kila siku,

Yaani kila nikiangalia hii channel ma vipindi ni yaleyale tu, tangu mwaka jana ni yale yale tu linatoka hili linaingia hili

Upuuzi tu hi channel ufujaji wa kodi hamna cha maana,
Inaonekana mliweka dvd tu tangu chanel ianzishwe ni dvd hiyo hiyo mpaka leo!

Ujinga kabisa
 
Channels zote za wanyama hurudia documentaries zao wewe utakuwa mshamba wa haya mambo
 
Vipindi kurekodi ni garama, kama hawana fungu la kufanya hivyo waache kurudia? Hii TV ndio ilitakiwa ioneshe live ufunguzi wa mbuga ya Burigi lakini imebaki kuwa ya kuonesha historia.. Wamiliki waipe fungu.
 
TBC kama shirika linapaswa kujiongeza kikamilifu hususani katika safu ya watangazaji wake, inawezekana shirika linazuia ubunifu wa watumishi wake au watumishi hawana ubunifu hivyo tuilaumu safu ya human resource kwa kutokujua imsajili nani na kwann.
Tanzania safari channel tulitarajia management iweke mpunga mrefu kwa watu kama antonio nugaz wa clouds media, ije na cameramen wa nguvu, lakini mambo yamekuwa tofauti, mnaleta sura zilezile za tbc one kwenye mambo ya utalii. Vipindi havipo clear mara yoga, mara mkwawa, mara yoga tena.
Mkurugenzi vp bwana, eeh, ubunifu tafadhali, tafuta vichwa uweke hapo, private wanamudu vp? Ongea nao wakusaidie.
 
Channels zote za wanyama hurudia documentaries zao wewe utakuwa mshamba wa haya mambo
Kama zipi hizo channel mana hii cchannel mimi naona kama imeshindwa kujiendesha muda wote siku nzima tunashindia kuangalia historia ya mkwawa ni bora wangeandaa tu matangazo yawe yanarushwa kwenye tv zingine
 
Hii channel ni ipuuzi tu na nahisi mpaka kufikia sasa imeshatelekezwa, nguvu zote zile kumbe ni zero tu!

Yaani mwaka mzima vipindi ni vile vile, mwaka mzima umeisha vipindi ndo vilevile vilivyorekodiwa,
Kila ukiangalia ni makala zile zile tangu mwaka jana, yaani kipindi kimoja kwa wiki kinarushwa zaidi ya mara10
Sasa kuna haja gani ya kukaa tunaangalia vipindi hivyo hivyo tu kila siku,

Yaani kila nikiangalia hii channel ma vipindi ni yaleyale tu, tangu mwaka jana ni yale yale tu linatoka hili linaingia hili

Upuuzi tu hi channel ufujaji wa kodi hamna cha maana,
Inaonekana mliweka dvd tu tangu chanel ianzishwe ni dvd hiyo hiyo mpaka leo!

Ujinga kabisa
 
Jana nimeona historia ya chief Mkwawa!! Namna alivyoishi, leadership strategies zake; mapambano dhidi ya wajeruman, kifo chake kichwa chake kubebwa na kurudishwa, kaburi lake yeye na mlinzi wake...

Ilikuwa nzuri....kweli kabila la wahehe lina nembo!!

Majina ya kijeshi kama Kalenga, Lugalo yametokea huko!!
 
Back
Top Bottom