Channel Ten: Mchungaji Antony Lusekelo azungumzia Kuchinja!

Status
Not open for further replies.
Kwani LUSEKELO ni nani, na ana title gani kwenye ukristo mpaka awasemee wakristo. Nafikiri ni maoni yake na kanisa lake.

Mzee wa upako ni kiongozi wa kanisa. Anawafuasi ambao wanamuamini na kumkubali. Sio lazima awe amewasemea wakristo wote. Inawezekana Amewesemea wafuasi wake tu. Lakini wote tumepata faida.
 
Katika hili linahitaji hekima, busara na uvumilivu sana! Fikiria nini kitatokea kama wakristo au waislamu! Mmoja wapo akiruhusiwa kuchinja????????????
 
Ewe mktistu mwenzangu jiulize swali moja tu "je ukila nyama iliyochinjwa na muislam imani yako inaathirika?". Hata maandiko yanatuelekeza kiingiacho si haramu bali kitokacho ndani ya nafsi ya mtu.
Ni suala la busara tu kuwa hawa wenzetu imani yao imewabana katika hilo, basi tuwaheshimu na tuwaachie kazi hiyo iwe yao. Lakini vilevile nao waweke ustaarabu kutambua kuwa kuchinja sio haki yao bali ni utamaduni tu uliochangiwa na kuishi pamoja kwa kuheshimiana.

waislam imani yao inawaambia wasile kitimoto ila haiwakatasi kuchinja, sasa kwa nini hawataki kutuchinjia kitimoto?
Iweje kitimoto tuwe na mchinjaji wetu, ila kuku, mbuzi ng'ombe na nyingine tumchukue wakwao?

Pia huenda hujui kama kuchinja ni mojawapo ya ajira coz kuchinja ng'ombe mmoja unapewa kilo 3 za nyama au pesa zenye dhamani na kilo tatu, ukichinja kuku unapewa machinjo yako yani shingo, kichwa n.k

pia haina sababu yeyote na kumwachia achinje mtu ambae anaamini akikuua anapata thawabu, akiuliwa anakwenda peponi
 
amjaacha 2 mambo ya kuchinja wajameni? Nchi inamatatizo lukuki mnakomaa na kuchinja.

hoja ya kuchinja si imeibuka mwezi jana tu, kwani huko nyuma wakati hii hoja haipo nchi ilikuwa haina matatizo?
 
Kwenye kipindi kilicho rushwa na chaneli ten mzee wa Upako ameonyesha kushangazwa na viongozi wa kikristo wanao ng'ang'ania kuchinja. Amesema ""nawashangaa sana wachungaji wenye hoja za kipumbavu eti nani achinje"

"Wanamsumbua waziri mkuu eti kujadili nani achinje wakati nchi ina matatizo lukuki, kwani waislamu walipo kuwa wana chinja ilikuwaje?"

Akaendelea kusema "Tuombee amani tuache hoja za kijinga eti nani achinje nani asichinje".

Aliongea mengi kuonyesha namna ambavyo amani yetu inaweza kutoweka kwa ajili ya mawazo ya kijinga! Amewaomba wakristo kusoma Warumi 14 mstari 1 na 31.

Naomba mwenye biblia atuweke mstari huo unasemaje.

Mazee nataka ku prove a point.

Kabla ya kuusoma mstari huo wala kujua unasemaje, naweza kukwambia kuna mstari mwingine katika biblia hiyo hiyo unaopingana na huo, ambao mtu yeyote anayetaka kumpinga Lusekelo anaweza kuutumia kwani Biblia imesema "neno lolote la bwana ni zuri na lafaa kwa mafundisho"

Kwa hiyo biblia unaweza kuifinyanga vyovyote unavyotaka.Kama unataka shari unaipeleka kwenye shari na itaku support. Kama unataka heri unaipeleka kwenye heri na inaku support.

Haina tofauti na methali za Kiswahili.

I might as well use methali za Kiswahili for that matter, at least there is a cultural connection.

Go figure.
 
Hahahaa,

Nimeiangalia hiyo Romans 14.

Ukiilinganisha na sheria ya Musa ni contradiction tupu!

Halafu yesu kasema hajaja kuipangua torati, bali kuikamilisha!

Hizi dini ni usanii mdogomdogo mtupu, tunahitaji kupiga vita umasikini na ujinga.
 
Namsikiliza Mchungaji Antony Lusekelo Chanel Ten sasa hivi. Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.

Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.

Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tangu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".

Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.

Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wap namshangaa inae
 
nini maana ya kuokoka wacha ubabaishaji hubiri injili inayotakiwa kwasababu utatoa hesabu siku ya mwisho kwa roho ulizokabidhiwa na si kuhubiri watu wakupende kwa sababu unawaambia maneno yanayowafurahisha uwe kama kama mikaya ambaye alihubiri kweli kweli mbele mfalme bila kujali manabii wengine wa uongo wetabiri uongo ole wenu watu wote watakapowasifu
 
Kwa waislamu kuchinja ni sawa!!! Lakini hebu tujadili upande mwingine wa shilingi. Kwa hiyo haki ya Wakristo kuchinja inazuiwa na kifungu gani cha katiba? Ndio kusema ni marufuku kwa wakristo kuchinja? Hiyo sheria ilipitishwa na bunge mwaka gani?????
 
Ewe mktistu mwenzangu jiulize swali moja tu "je ukila nyama iliyochinjwa na muislam imani yako inaathirika?". Hata maandiko yanatuelekeza kiingiacho si haramu bali kitokacho ndani ya nafsi ya mtu.
Ni suala la busara tu kuwa hawa wenzetu imani yao imewabana katika hilo, basi tuwaheshimu na tuwaachie kazi hiyo iwe yao. Lakini vilevile nao waweke ustaarabu kutambua kuwa kuchinja sio haki yao bali ni utamaduni tu uliochangiwa na kuishi pamoja kwa kuheshimiana.

Hilo andiko hujalielewa wewe??
 
Namsikiliza Mchungaji Antony Lusekelo Chanel Ten sasa hivi. Nimemkubali huyu kweli ni kiongozi sahihi katika Imani ya Kikristo. Tukiwa na Viongozi wa kama hawa Amani yetu ya inchi haiwezi kutetereka.

Heshima kwako Mchungaji. Natamani Wachungaji, Mapdre na Maaskofu pamoja na Makidanali wote Muwe na upeo mkubwa wa kufikiria kama huyu Mchungaji. Huyu ni Tunu ya nchi.

Kwa ufupi tu, Mchungaji Antony Lusekelo Ameshangaa kulikoni leo Mashekhe na Maaskofu au Mapadre au Wachungaji wagombane wakati waliishi kwa amani tangu zamani. Kama ni suala la kuchinja, mbona suala hilo tangu enzi ya wazee wetu, walikua wanachinja waislamu wanakula wote. "Kama tukichinja sisi waislamu hawali, basi wachinje waislamu tule wote. Kuchinja isiwe ndio sababu ya kuvunja amani ya nchi yetu".

Ameeleza kwa kirefu suala hilo. Hiyo ndio ilikua mada ya kipindi.

Huyu nimekua nikifuatilia mahubiri yake, huyu kweli anawakilisha imani sahihi ya kikristo. Mimi sio Mkristo mimi ni Muislamu, ila hua tuna wapenda viongozi kama hawa katika jamii. Sio vizuri sisi watanzania kutengana kimisingi ya dini. Ni vibaya na hatari sana. Familia nyingi ni mchanganyiko.

Amerefer kitabu kipi? Anaongelea desturi na mazoea kwani mkuu hujui desturi yetu ni kuvaa vibwaya na magome? Kwani nani alitustua tukaacha nasasa tunajiona tulikuwa tuko nyuma ndio maana tukafanya tuliyofanya
 
Ewe mktistu mwenzangu jiulize swali moja tu "je ukila nyama iliyochinjwa na muislam imani yako inaathirika?". Hata maandiko yanatuelekeza kiingiacho si haramu bali kitokacho ndani ya nafsi ya mtu.
Ni suala la busara tu kuwa hawa wenzetu imani yao imewabana katika hilo, basi tuwaheshimu na tuwaachie kazi hiyo iwe yao. Lakini vilevile nao waweke ustaarabu kutambua kuwa kuchinja sio haki yao bali ni utamaduni tu uliochangiwa na kuishi pamoja kwa kuheshimiana.

Kasome Wakorintho wa kwanza sura ya kumi mstari wa 28 "Lakini kama mtu ye yote akikuambia, “Hiki kimetolewa kafara kwa sanamu,” basi usikile kwa ajili ya huyo aliyekuambia na kwa ajili ya dhamiri"
 
We mzimu, nimeelewa sababu ya wewe kumfurahia mzee wa upako katika hili la kuchinja. Na sababu hiyo imekufanya uweke wazi kuwa wewe ni muislamu.

Ulichokifanya ni cha kawaia sana duniani. Kila akidai kitu hapa duniani, bila kujali kama kitu hicho ni sawa au la, kila atakayemuunga mkono atakuwa rafiki yake. Hiyo ndo hulka ya binadamu.

Alichotakiwa kufanya ni kupitia hoja zilizotolewa na wakristu wengine na aipangue moja baada ya nyingine kwa hoja. Hili suala la mazoea halitakiwi kupewa nafasi. Unaweza ukazowea kisicho sahihi, siku utakapogundua ubaya wa ulichokizowea, basi unabadilika toka hapo.
 
Kwa waislamu kuchinja ni sawa!!! Lakini hebu tujadili upande mwingine wa shilingi. Kwa hiyo haki ya Wakristo kuchinja inazuiwa na kifungu gani cha katiba? Ndio kusema ni marufuku kwa wakristo kuchinja? Hiyo sheria ilipitishwa na bunge mwaka gani?????
Yaani hapo ndo serikali ilipotokotea... Hata hiyo ya waislamu kuchinja kwamba ni sawa, ni kifungu kipi cha katiba ya nchi kinasema hivyo?
 
Mohamedi Mtoi mbona hakuna mstari hata mmoja unaoleta maana na uchinjaji hapo? Bali hiyo yote inazungumzia nyie mnaowabagua wenzenu wanaokula kila kitu nakusema ni makafiri na vivyovivyo wanaowabeza wenzao na kuona wajinga kisa wanajinyima. Ila kama kuchinja ni ibada ya muislamu kwani mkristu anashiriki ibada ya kiislamu? Tuko tayari kula kama sio ibada bali mnatuona tu wachafu lakini kama ni ibada kwakweli hapo chinjeni vyenu mle mkamilishe ibada zenu na hatutawaingilia nanyinyi msituingilie
 
Last edited by a moderator:
waislam imani yao inawaambia wasile kitimoto ila haiwakatasi kuchinja, sasa kwa nini hawataki kutuchinjia kitimoto?
Iweje kitimoto tuwe na mchinjaji wetu, ila kuku, mbuzi ng'ombe na nyingine tumchukue wakwao?

Pia huenda hujui kama kuchinja ni mojawapo ya ajira coz kuchinja ng'ombe mmoja unapewa kilo 3 za nyama au pesa zenye dhamani na kilo tatu, ukichinja kuku unapewa machinjo yako yani shingo, kichwa n.k

pia haina sababu yeyote na kumwachia achinje mtu ambae anaamini akikuua anapata thawabu, akiuliwa anakwenda peponi

Mkuu umesema kweli,Kinachowafanya wang'ang'anie ni ajira tu si vinginevyo.Kwani sehemu nyingi wananufaika na kichwa na shingo na hizo buku tatu.Hata mahakama ya kadhi wanachotaka ni ajira si vinginevyo.Kitu muhimu tuishi kizungu,bucha zieleze wazi kuwa hii imechinjwa kiislam na hii haijachinjwa kiislam na mtu iwe chaguo lake.Tena wakristu wao ni kula tu.kwani imeandikwa""KIMTOKACHO MTU NDIO HARAMU""
 
Kama kweli wewe ni mzee wa upako orijino mbona kipindi kile cha kuchomwa kwa makanisa mbagala hukutoa makavu laivu kama sasa unavyoongelea uchinjaji? Huoni kuwa wewe ni kinyonga unayebadilikabadilika kwa faida zako binafsi ila si kwa faida ya wote? Mbona hukusema laivu tena mbona hukutumia lugha uliyoitumia kuwa mkristo anayeng'ang'ania kuchinja huo ni upumbavu kwanini hukusema wanaochoma makanisa kwa itikadi za kidini huo ni upumbavu mbona ikifika hapo unamumunya maneno?
 
Tatizo hakuruhusu maswali. ningekutuma umwulize hili:

1kor 10:27 Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kila kitu kitakachowekwa mbele yako bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 28 Lakini kama mtu ye yote akikuambia, “Hiki kimetolewa kafara kwa sanamu,” basi usikile kwa ajili ya huyo aliyekuambia na kwa ajili ya dhamiri.

ndugu Mohamedi Mtoi shida ipo hapo kwenye red, na tatizo limekuwa kubwa baada ya waislam kutangaza wazi kuwa kuchinja ni ibada. Ibada ya namna hiyo kwa mkristo ilisha komeshwa na ujio wa YESU KRISTO. Thus kula nyama iliyochinjwa kwa minajili ya Ibada, ni sawa na wewe umeshiriki ibada ile. Hii hairuhusiwi pamoja na kwamba tumeagizwa upendo.

Onyo, Mohamedi Mtoi, wewe ni kati ya watu wanaoheshimika sana hapa JF. Angalia uzi huu ulioanzishwa usije kukushua heshima.

Hiyo red inazungumzia sanamu, sasa ni nani anaye endesha ibada ya sanamu kati ya Ukiristo na Uislaam ?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom