Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Katika kipindi cha leo asubuhi, kinachoongozwa na Nd. Albert kilimkaribisha mtu aliejitambulisha kama Sheikh wa dini ya Kislamu, katika mdahalo uliobatizwa jina la TOBA NA AMANI. Lakini kimuonekano ni mkereketwa wa siasa asie na sumile.
Inasikitisha kumuona Sheikh bila ajizi, uwongo iliofurutu ada, wala woga wa dini akiikoroga (Quran) kwa kutumia aya za kiarabu na kuzistafiri atakavyo kwa malengo yake ya kisiasa na ya upotoshaji.
Katika jitihada ya kupotosha na kuwachanganya watu kwa manufaa yake na kisiasa, aliseama hata hili jina la mji wa Dar es salaam limetokana na kutajwa kwenye Quran na ndio maana Tanzania imebaki salama licha ya kuzungukwa na nchi zenye mizozo (mapigano) ya kisiasa.
Alisema, licha yaliotokea Zanzibar, nchi imeendelea kubaki salama kwa sababu tu Tanzania imebarikiwa jina hilo katika Quraan.
Ukweli ni kuwa Jina la Daressalaam, ambalo lilijuulikana kama Mzizima ( mji uliochangamka) hapo awali, limetolewa na Sultan Majid bin Said wa Zanzibar katika mwaka 1866 ambae nyumba yake alioijenga mpaka leo ipo (imegeuzwa kuwa ofisi ya jiji)
Nilipokuwa nasoma madrasa 1960 mjini Zanzibar, tulionywa kuwa tuwe macho kuwa bara hakuna Wanazuoni wa kiislamu, ila kuna masheikh "KAMBA" tu. Leo nimeamini!