#COVID19 Chanjo za Corona Tanzania "zimedoda" kwasababu wanaosema tuchanje hawako "serious"

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Nchi yetu itapiga hatua kimaendeleo katika sekta zote siku pale viongozi wa serikali wataacha upuuzi wa ku "underestimate" uelewa wa sisi wananchi wa kawaida.

Imefika hatua viongozi waache ile dhana ya kwamba sisi wananchi wa kawaida hatuelewi lolote hivyo ni watu wa kuburuzwa. Hebu fikiria katika mazingira haya nani ataona umuhimu wa chanjo:-

1. Tunaambiwa tuvae barakoa lakini hizi barakoa zinatiliwa mkazo ukienda baadhi ya ofisi na hospitali tu! Tena hata ukiibeba mkononi au ukaivaa kidevuni unahudumiwa vizuri tu. Hapa najiuliza shida ni kubeba barakoa au kuivaa ipasavyo kujilinda?

2. Maeneo ya ibada na starehe Kama baa, kumbi za starehe, viwanja vya mpira na kwingineko hakuna haja ya barakoa isipokuwa hospital na ofisini tuu!?

3. Matamasha makubwa Kama ya kina Nandy festival na mikutano mikubwa ya injili na ya kisiasa Kama ya Rais na wabunge wake kusalimia wananchi njiani yenyewe Covid-19 inakaaga pembeni!? Mbona hatuoni barakoa?

4. Miezi imepita tangu tupokee chanjo dozi milioni moja za Covid-19 lakini hadi Jana tumeambiwa waliochanjwa ni laki 3+ (31% ya dozi zilizoletwa) halafu semaji la serikali anasema chanjo zimeisha na wanatarajia kupokea shehena nyingine hivi karibuni.

Hivi kweli kati ya 69% iliyobaki na 31% iliyotumika ni ipi kubwa!? Hapa sio kutufanya wananch mazuzu kweli!

Kwanini asiseme tu kuwa zoezi linaonekana kwenda taratibu sababu ya mwitikio mdogo wa wananchi!?

Mwitikio ni mdogo kwasababu wananchi tunaona maneno ya viongozi hayaendani na hali halisi!

Chanjo zimedoda kwasababu wananchi wanayo macho na ufahamu timamu, wanaona kinachoendelea. Hizi chanjo zinaweza kukushawishi uamini kwamba ziko kisiasa zaidi kuliko kitabibu
 
Nimependa hiyo ya kuvaa barakoa isivyo sahihi (km kidevuni) hasa na hao hao wanaohimiza zivaliwe. Huyo mhusika anahutubia kundi la watu, mojawapo ya agenda ikiwa kuhusu chanjo na kujikiga dhidi ya UVIKO-19 huku barakoa ameivaa kidevuni. Jasho lote, litokanalo na nguvu anayotumia kuhutubia, linajaa kwenye kidevu kisha anairudisha puani, LoL!
 
Wasipoangalia zitaharibika na kuleta madhara makubwa kwa binadamu kama wale ng’ombe
 
Back
Top Bottom