#COVID19 Chanjo ya Corona Dar es Salaam na muitikio mdogo

nabiitz

Senior Member
Jan 29, 2014
157
32
Dar es Salaam ni kama imebeba picha ya Tanzania nzima wakati fulani ni kama pilot (case study) katika mikoa mingine.

Mkuu wa mkoa wa DSM alitangaza siku ya leo kuwa kutakua na chanjo ya UVIKO-19 katika uwanja wa taifa wa Uhuru, mimi nimekwenda na nimechanjwa hali nilioiona kwa leo hapana muitikio ni mdogo mno kuna sababu za msingi za kulipa nguvu jambo hili.

Mosi ni kwa wale waliokuwa viongozi wa awamu ya tano katika Wizara ya Afya wajipime,sio mpaka mama awabadilishie majukumu mengine.

Inawapa sana ugumu watanzania" jana waambiwe hivi na leo waambiwe hivi"(kiongozi anasema jana chanjo sio salama leo anasema chanjo ni salama).

Shaka kubwa sana imejengeka hapo kwa wananchi Rai yangu wapatikane viongozi wapya katika wizara hii kutuhamasisha juu ya uchanjwaji huu vinginevyo naona kabisa serikal inaenda kufeli katika jambo hili.

Sio mbaya kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akimuona RC mstaafu aliyegombea kule Mbutu ampe namna ya kuhamasisha watu anapokuwa na jambo lake kwa wananchi wa DSM, naona habari za ofisi yake zinaishia Bungoni tu sio Dar es Salaam yote.

Muwe na Jumapili njema, korona ipo.
 
hii hali ikiendelea na huu mkanganyiko watuchanje tusichanje basi wananchi hawatajitokeza kabisa kuchanja.

Mkuu wa mkoa kafeli mno katika kuhamasisha wanadsm wajitokeze ilitakiwa leo ndio iwe slama kwa taifa kua dsm watu wamejitokeza wengi
 
Nakumbuka wakati ule wa Mwendazake ilisemekana Eti watu wasipochukua tahadhari sijui hata wangechukua tahadhari Basi ilitarajiwa maiti za halaiki kuokotwa majiani!

Kukawa na shinikizo la lockdown jamaa akagoma kuruhusu mpaka ikakosa kueleweka!

Sasa wenye ushahidi watuoneshe hizo maiti je ziliokotwa za halaiki zitokanazo na ugonjwa wa korona?

Je pamoja na kutokuwepo kwa lockdown lakini tulivuka au hatukuvuka salama kwa rehema za mwenyezi Mungu?

Miili yetu sisi ni tofauti na ya wazungu!

Mzungu mafua ya kambaku yakimbana anapelekwa hospitali kwa ambulance wakati sisi tunafanya nayo kazi hadi iishe yenyewe!

Tusiogope tutakuwa salama!

Hili nalo litapita!

Kama nafsi inakusukuma kuchanjwa usisite tafadhali nenda kachanjwe na yule ambae nafsi inasita kwenda kuchanjwa asichanjwe na aionekane kuwa muasi!
 
angekua bashite leo ilikua ni habari watu wakanyagana wakitaka chanjo mkoa kasi huu
Kweli Kabisa hii kitu imkute Ruge na Bashite mbona wangekuwa wameagiza zingine ila pia huku kwenye vituo husika uchanjaji ni rahisi sana sioni haja ya kwenda taifa
 
Niliwahi kushauri hapa kuwa kabla ya nationwide roll out ya Vaccine mama asafishe kwanza mabaki haya ambayo jana yalisema ivi Na Leo wanasema vingine wananchi tunapatwa Na mkanganyiko mana Wataalamu wetu jana wakisema ivi Na Leo wanasema vile hata Mimi nimeamua kukaa pembeni kwanza nikiangalia sarakasi zao
 
Tozo za Simu, mara kodi ya jengo. Unaanzaje kupata utulivu wa Akili kwenda kuchanja.
Bora kwenda kutafuta pesa Au kwenda kwenye Ibada kuliko kwenda kuchanja.
Chanjo zenyewe ziaharibike tu.
hahahah afya muhim lakin kuliko izo tozo
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom