Changamoto za Dini,Elimu na Pesa kwenye uchumba

shangoo

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2015
Posts
325
Reaction score
362
Dini
Kwanza namchukia aloleta dini kwasababu zimetubagua na kututenga kwenye jamii,pili kama umekulia maadili ya dini flani ukitaka kuoa/kuolewa upande mwingine lazima washauri watajiinua sana kukushauri tena kwa mifano hadi ya wajomba na mashangazi jinsi dini ilivyonachangamoto kwenye uchumba

ELIMU
hapa napo pagumu wachumba wanaweza wasioane kisa mmoja anaelimu kubwa kuliko mwenzake sana kwa wanaume ndo inachangamoto kwenye familia zetu ukizidiwa elimu na mwanamke

PESA
hapa napo panachangamoto ila sio sanaaa kama kwenye DINI.

Hivi ni kweli dini inaweza kufanya umuonaye anafaa kuwa mke/mume akawa adui kisa ndugu Waislamu/wakristo na hii inachangia familia nyingi kukosa baraka manake unakuta hata ndugu wa karibu tofauti na wazazi wanakuona kama MUASII wa dini yenu endapo utaoa/kuolewa na mtu mwenye dini tofauti na yako,ndoa nyingi sinaishia bomani kwa (shekhe/mchungaji) DC.unaishia kufunga ndoa kwa baraka za DC na serikali yake badala Mwenyezi Mungu.
 
Dini kwangu ni kigezo kikubwa saana!!!!

Tutaanzaje maisha wakati tunapishana kiimani? Watoto watachukua dini gani? Si ndo kuwachanganya!!!
Napenda sote kama familia tunatoka pamoja kwenda kanisani/msikitini!!! Inaleta umoja.

Dini moja inaruhusu wake wengi na nyingine hairuhusu!!! Mtafuata lipi kwenye ndoa yenu? Na nna uhakika gani kama hatobadilika huko baadae na kuongeza mke wa pili na watatu?

Swala la elimu ni muhimu pia!!!

Kwa nilipofikia na ninapotarajia kufika kuna wanaume wa level fulani ya elimu siwezi kua nao... Sio kwamba wamepungukiwa kitu bali ni kuepuka migogoro tu!!! Mwanamke ukiwa na gape kubwa sana kielimu na mwenza wako inafanya ajisikie chini sana, anaweza dhani kila unachofanya unafanya kumdharau kwa sababu ya elimu yake!!! Hapa upendo uongoze tu ila kuna limits!!!
 
Hapo ndoniliposema naichukia dini,kwasababu kumpenda mtu hupangi wala huchagui ila kuoa/kuolewa unapanga na unachagua...kwa kigezo kikuu cha dini (imani)
 
Kweli kabisa!!! Na hii husababisha michepuko!!! Yaani watu wanapendana sana ila wanashindwa oana sababu ya dini!!! Kila mmoja anaenda oana na mtu mwingine, unadhani kuna kuachana hapo???
 
Kunatokea wapi huku dini imeshakuchagulia mke/mume...ni ngumu sanaa kwenye ndoa.na michepuko kufa inakuwa ngumu
 
Ya ukweli mtupu! Ila kwenye Elimu tunaweza kuongezeana "nyama" za uelewa kidogo.Kuna marekebisho ya hapa Na pale lakini umenena ukweli tu.

QUOTE="Paprika, post: 20461513, member: 418389"]Dini kwangu ni kigezo kikubwa saana!!!!

Tutaanzaje maisha wakati tunapishana kiimani? Watoto watachukua dini gani? Si ndo kuwachanganya!!!
Napenda sote kama familia tunatoka pamoja kwenda kanisani/msikitini!!! Inaleta umoja.

Dini moja inaruhusu wake wengi na nyingine hairuhusu!!! Mtafuata lipi kwenye ndoa yenu? Na nna uhakika gani kama hatobadilika huko baadae na kuongeza mke wa pili na watatu?

Swala la elimu ni muhimu pia!!!

Kwa nilipofikia na ninapotarajia kufika kuna wanaume wa level fulani ya elimu siwezi kua nao... Sio kwamba wamepungukiwa kitu bali ni kuepuka migogoro tu!!! Mwanamke ukiwa na gape kubwa sana kielimu na mwenza wako inafanya ajisikie chini sana, anaweza dhani kila unachofanya unafanya kumdharau kwa sababu ya elimu yake!!! Hapa upendo uongoze tu ila kuna limits!!![/QUOTE]
 
Ya ukweli mtupu! Ila kwenye Elimu tunaweza kuongezeana "nyama" za uelewa kidogo.Kuna marekebisho ya hapa Na pale lakini umenena ukweli tu.

QUOTE="Paprika, post: 20461513, member: 418389"]Dini kwangu ni kigezo kikubwa saana!!!!

Tutaanzaje maisha wakati tunapishana kiimani? Watoto watachukua dini gani? Si ndo kuwachanganya!!!
Napenda sote kama familia tunatoka pamoja kwenda kanisani/msikitini!!! Inaleta umoja.

Dini moja inaruhusu wake wengi na nyingine hairuhusu!!! Mtafuata lipi kwenye ndoa yenu? Na nna uhakika gani kama hatobadilika huko baadae na kuongeza mke wa pili na watatu?

Swala la elimu ni muhimu pia!!!

Kwa nilipofikia na ninapotarajia kufika kuna wanaume wa level fulani ya elimu siwezi kua nao... Sio kwamba wamepungukiwa kitu bali ni kuepuka migogoro tu!!! Mwanamke ukiwa na gape kubwa sana kielimu na mwenza wako inafanya ajisikie chini sana, anaweza dhani kila unachofanya unafanya kumdharau kwa sababu ya elimu yake!!! Hapa upendo uongoze tu ila kuna limits!!!
[/QUOTE]
Hilo jina lako tu mkuu linaashiria mumeo atavyopata shida kukuelewa ulivyo!nataniaaa.....Kiukweli sio ndoa sio elimu uliyonayo tu kwani mume ni zaidi ya elimu unayotaka kuiongeza
 
Penye upendo wa kweli swala la dini, utofauri wa elimu, na pesa haiwezi kuwa kikwazo unless mtu anayo sababu ya kumpenda tuu coz true love has no reason
 
Hapo ndoniliposema naichukia dini,kwasababu kumpenda mtu hupangi wala huchagui ila kuoa/kuolewa unapanga na unachagua...kwa kigezo kikuu cha dini (imani)

Kuna uhai wa kimwili(kidunia).Ndo huu mwili toka kuumbwa kwake kwa Yai Na Mbegu ya kiume.Kuna uhai wa kiroho.Ni hii pumzi inayotuwezesha kuendesha uhai wa mwili.Na kishapo Kuna uhai wa Milele.Huu Ni baada ya maisha ya kimwili Na kiroho kukomeka hapa duniani.

Sasa uhai wa aina zote tatu unategemeana.Ili upate uhai wa milele sharti uhai wa kimwili Na kiroho ulelewe ipasavyo.Huwezi Kwa mfano kujiua au kuua kisha ukategemea kuzawadiwa uhai wa milele.
Kwa hiyo ukipata mchumba ambaye yeye anaamini tofauti Na ukweli huo wakati pengine Wewe unaelewa kama nilivyobainisha hapo juu basi jua zawadi ya uhai wa milele huna chako tena.Kwa hiyo Ndio maana wazazi wanaoelewa wanakuwa makini katika hilo Na wala si Kwa Lengo la kukuzibia ridhiki au roho ya korosho bali wanakuwa wanasukumwa na maslahi mapana juu ya maisha yako baada ya uhai wako wa kimwili Na kiroho kukomeka hapa duniani.
 
Hilo jina lako tu mkuu linaashiria mumeo atavyopata shida kukuelewa ulivyo!nataniaaa.....Kiukweli sio ndoa sio elimu uliyonayo tu kwani mume ni zaidi ya elimu unayotaka kuiongeza[/QUOTE]

Mimi Sio jinsia ya kike.Na hata kama ningekuwa wa jinsia ya kike bado mantiki katika hoja yoyote haina ujinsia.Angalia tu kama nilichokisema Ni cha kweli au la.
 
Mimi wazazi wangu walishawahi Nambia nikipata mchumba wa dini tofauti na yangu asifike nybani
Huyo mzee wako ana ongea tu sidhani kama ana uhakika na anacho kisema,huja pata kidume chenye pesa wewe,alafu mzee aonyeshwe jeuri ya pesa,kwa jinsi ninavyo ijuwa jeuri yake,trailer lina anza mzee Ana badili dini,movie kamili ina ishia ukoo mzima mna badili dini na kufuata dini ya upande wa kiumeni...
 
Aiseeh
 
Dini zimekuwa vyanzo vya kutenganisha watu dunani.

Mwanamke asipokuwa na pesa, elimu kwangu ni sawa....lakini akikosa akili ndo mwisho wa kila kitu.

Mkuu salama? Ndugu yako Kiranga "alivyosafiri" umebaki peke yako lakini bado umo tu huchoki; unapigana bado! Dini kama mahusiano kati ya Mwanadamu na Mungu Muumba hayaepukiki.Ukiwa Na dini ya kuamini kuwa Kuna watu wameumbwa Kwa madaraja (Brahmanism) toka daraja la lenye hadhi hadi daraja dhaifu hiyo;dini kama hiyo Huwezi kuifungamanisha Na mtu mwingine anayeamini kuwa binadamu wote tumeumbwa sawa Kwa kupewa sura Na mfano wa Mungu.Ukifanya hivyo utapanda Mbegu ya vurugu tu.Na ndio chanzo cha emotional conflicts sio substantive conflicts katika jamii.Tatizo letu ninaloliona Ni Kwamba Mungu wa kweli kupitia mwanaye Yesu Kristu Na Roho Mtakatifu wameweka kwetu kila kitu tunachohitaji Kwa ajili ya kuujua ukweli lakini tumekuwa wavivu wa kutafuta ukweli huo badala yake tumekuwa kama watoto wadogo wasioweza kujilisha Bali kuwekewa vijiko vinywani.
 
Niliwahi kuwa na binti wa Dini tofauti na yangu.
Kuna stage ilifika akanambia wazazi wake hawatakubali yeye kuolewa nami.
Tukaachana, akaolewa huko.
Siku za karibuni amekuwa akiniomba msamaha, yuko tayari hata kuwa mke wa pili.
Na Anajua siwezi kuoa wake wawili.
Alishateseka huko na mume wake na wameshatengana.
 
Dini, elimu na pesa kwangu siyo vigezo vikubwa ili mradi nimempenda kwa dhati mwenza wangu.

Nilimpata mchumba wa dini tofauti nikaamua kubadili wazazi wangu walinielewa ila babu, bibi na mashangazi mmh kidogo walitia ngumu ila mwishoni ilibidi wakubali matokeo.
 
Mkuu salama? Ndugu yako Kiranga "alivyosafiri" umebaki peke yako lakini bado umo tu huchoki; unapigana bado! Dini kama mahusiano kati ya Mwanadamu na Mungu Muumba hayaepukiki.Ukiwa Na dini ya kuamini kuwa Kuna watu wameumbwa Kwa madaraja (Brahmanism) toka daraja la lenye hadhi hadi daraja dhaifu hiyo;dini kama hiyo Huwezi kuifungamanisha Na mtu mwingine anayeamini kuwa binadamu wote tumeumbwa sawa Kwa kupewa sura Na mfano wa Mungu.Ukifanya hivyo utapanda Mbegu ya vurugu tu.Na ndio chanzo cha emotional conflicts sio substantive conflicts katika jamii.Tatizo letu ninaloliona Ni Kwamba Mungu wa kweli kupitia mwanaye Yesu Kristu Na Roho Mtakatifu wameweka kwetu kila kitu tunachohitaji Kwa ajili ya kuujua ukweli lakini tumekuwa wavivu wa kutafuta ukweli huo badala yake tumekuwa kama watoto wadogo wasioweza kujilisha Bali kuwekewa vijiko vinywani.
Mimi nipo salama mkuu, habari za siku?
Nilikutana na Kiranga JF lakini misimamo yangu ni tangu utotoni na hakuna cha kuibadilisha blindly.

Sii kweli kwamba dini ni mahusiano yasiyoepukika baina ya Mungu na Mwanadamu na ndio maana kuna Atheists.
Dini hata iwepo moja lazima itakuwa ni chanzo cha vurugu na uhalifu.Ukristo ulienezwa ulaya kwa ulazima, kwa kuua wapagani walioukataa. Uislamu una jihad inayoweza kuhusisha hata waislamu kwa waislamu.
Kitendo cha kuona kwamba dini flani ndio wanatenda makosa zaidi kuliko nyingine ni uhalifu tosha maana dini zote kwa namna moja au nyingine na kwa zama tofauti zimetenda uhalifu dhidi ya binadamu.
Kama Mungu ndiye aliyetuumba na kutupa dini ili tuhusiane naye, basi theism ingekuwa ni moja kati ya tabia za viumbe hai. Tungemjua na kumwabudu Mungu naturally bila kufundishwa wala kusoma vitabu.
 
Back
Top Bottom